Kabila la miluzi ambalo limeanza kufufuka baada ya kuonekana kuangamia

Mtu anayepiga miluzi

Chanzo cha picha, RICHARD FRANKS

Iliyochapishwa

Watu katika kisiwa kidogo cha La Gomera, kilichopo ndani ya bahari ya Atlantiki cha taifa la Uhispania, hutumia miluzi kama njia ya mawasiliano . Mbinu hii nusura itoweke na sasa imejumuishwa katika mtaala wa masomo ya shule. Je ni vipi wakazi wa eneo hilo waliweza kuhifadhi mtindo huu wa kipekee wa mawasiliano?

Juu ya majabali ya miamba ya Barranco de valo, katika kisiwa cha La Gomera, watoto wawili wa miaka 12 wanawasiliana kwa mtindo wa Silbo Gomero, lugha ya miluzi inayotumiwa na wenyeji wa kisiwani humo.

Kwa dakika chache, wimbo wa miluzi wa vijana hao - Irún Castillo Perdomo na Angel Manuel Garcia Herrera inapaa angani mithili ya tai wanaopaa angani.

Walikuwa wamesindikizwa na mwalimu mstaafu mwenye umri wa miaka 70 Silbo Gomero, Eugenio Darias, ambaye babu yake alikuwa anamiliki ardhi na kufanya kazi katika kisiwa hiki hiki.

Aliniambia kuwa mawasiliano ya miluzi waliyokuwa wanayafanya wavulana yanafanana na mawasiliano waliyokuwa nayo kuhusu jumbe au katika uwanja wa michezo.

Lakini lengo la kuzingatiwa ni kuhusu sauti sita za kipekee zinazotofautiana ambazo ndizo zinazounda lugha ya La Gomera ya miruzi inayolindwa.

Lugha ya kupiga miluzi inapatikana katika takribani "maeneo 70 ", kulingana na mwandishi wa habari wa eneo hilo Francisca Gonzalez Santana.

"Nchini Uturuki, kwa mfano, upigaji wa miluzi ulianza miaka 500 iliyopita wakati wa himaya ya Ottoman ," alisema.

"Halafu ikasambaa katika kanda yote ya Bahari nyeusi ; na katika Mexico, tunaweza kupata mawasiliano kwa njia ya miruzi katika Uhispania - Chinantec."

Silbo Gomero, ambayo ni mojawapo ya lugha za miluzi ambazo zilizotangazwa rasmi kama urithi wa utamaduni usiogusika na Shirika la Umoja wa Mataifa la Unesco mwaka 2009.

Luha ya Silbo Gomero hutumia sauti sita zilizofupishwa katika mawasiliano.

Silbo Gomero ni eneo lenye mandhari ya milima

Chanzo cha picha, RICHARD FRANKS

Maelezo ya picha, Silbo Gomero ni eneo lenye mandhari ya milima

Miruzi miwili inayotofautiana huwakilisha irabu tano katika lugha ya Kihispania, huku miluzi minne pekee ikiwakilisha konsonati 22.

Sauti ya mruzi hufanywa kuwa ndefu au fupi kuigiza maneno.

Kuna mbinu kadhaa za kupiga miruzi katika kisiwa hiki, ingawa labda utamaduni zaidi huoneshwa na mchonga sanamu José Darías.

Watu wenye uzoefu hutumia mbinu tofauti za kupiga miruzi kwa kutumia vidole na mara kwa mara unaweza kujua ni nani anaita kwa kusikia "lafudhi" ya mruzi-ingawa wengi watajitambulisha wenyewe na kuita jina la mpokeaji wa ujumbe.

Wakati ujumbe unapoeleweka, wanaujibu "bueno bueno". Kwa kifupi na kwa urahisi kabisa.

Hatahivyo, kile ambacho sio kifupi ni kuhusu historia ya asili ya lugha yenyewe.

Vitabu vya historia vinaonesha kwamba lugha ya miluzi ilianza takriban mwaka 1402 wakati Uhispania ilipochukua udhibiti wa visiwa vya Canary, ingawa urithi wa lugha ya Gomero Silbo ulibishaniwa.

Katika kisiwa kidogo cha Canary , lugha ya miluzi ambayo ilikuwa iankaribia kutoweka imeanza kufufuka

Chanzo cha picha, RICHARD FRANKS

Maelezo ya picha, Katika kisiwa kidogo cha Canary , lugha ya miluzi ambayo ilikuwa iankaribia kutoweka imeanza kufufuka

Kutoka katika eneo la miamba katika picha hapo juu, wenyeji hupiga miluzi kutangaza matukio, kuomba mifugo iletwe, kutoa onyo juu ya hatari, au hata kutangaza kifo cha mtu wa familia. " Husaidia sana kuwaepusha wakazi kupanda miamba," Darias anasema.

Katika miaka ya 1950, Silbo Gomero ilikuwa ikizungumzwa mara kwa mara kwamba, ambapo wengi walikuwa wakisubiri kutuma maagizo bondeni kote.

"Ni eneo gumu kulifanyia kazi-hakuna hata mmoja anayetaka kwenda pale juu na kushuka kufikisha ujumbe kwa walengwa. Kutokana na hilo, kwahivyo mawasiliano mengi hufanyika kwa njia ya miruzi wakati huo huo, na tulilazimika kusubiri muda wetu," anasema Darias.

"Ilikuwa kama kelele za magari!" aliendelea

Katika eneo hilo kuna sanamu inayomuonesha mtu akipiga miluzi

Chanzo cha picha, RICHARD FRANKS

Maelezo ya picha, Katika eneo hilo kuna sanamu inayomuonesha mtu akipiga miluzi

"Upigani wa miruzi umehifadhiwa kwa uangalifu zaidi katika visiwa vya Canary Islands," anasema Santana, "kwasababu ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu: sanaa yam domo ya kisiwa, chenye maeneo ya milima na makorongo , na uchumi wetu ambao umehusishwa na kilimo na mifugo."

Huku upigajii wa miruzi kwa sasa unasikika kwa nadra nje ya shule au mipango rasmi, mara chache hutumiwa katika kisiwa ambako hakuna mawasiliano ya simu.

"Ninafahamu wafugaji wa mbuzi ambao bado wanapiga miluzi ," anasema Darias.

"Ni wapwa na wajukuu wanaoishi kusini mwa kisiwa. Mifugo yao huzunguka katika maeneo yasiyofikiwa na mitandao wa simu na hiyo ndio maana wanatumia miluzi ."

"Ungependa kutumia lugha ya Silbo Gomero leo kama simu yake imeisha betri?" Nauliza.

"Bila shaka!" anasema. " Kwanza bado tunawasiliana kana kwamba hakuna simu pale ."