Vita vya Afghanistan: Miili yatapakaa barabarani huku vita vikiwazunguka wakazi wa Lash Gar

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Bismillah Khan Mohammadi hakuwepo nyumbani siku ya Jumanne usiku ambapo wapiganaji walililipua bomu na kufyatua risasi karibu na eneo hilo linalolindwa sana.

Familia yake iliondolewa huku wapiganaji wanne wakiuawa, maafisa wamesema.

Kundi la wapiganaji wa Taleban limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Wakati huohuo wakazi wa Lashkar Gah kusini mwa Afghanistan ni miongoni mwa maelfu ya watu waliokwama au kukimbia kwa ajili ya kunusuru maisha yao huku mapigano ya kudhibiti mji huo yakishika kasi baina ya wanamgambo na vikosi vya serikali.

BBC haiwataji baadhi ya watu waliohojiwa katika makala hii kwasababu za usalama wao.

"Kuna maiti kwenye barabara. Hatujui kama ni raia au ni Taliban," mwanaume mmoja aliiambia idhaa ya BBC ya Afghan katika mahojiano kwenye Whatsapp. "Makumi ya familia wametoroka nyumba zao na kukaa karibu na mto Helmand."

Wenyeji wengine wenye hofu kubwa waliiambia BBC kuwa wameona miili ya wafu ikiwa imetapakaa kwenye mitaa.

Kutekwa kwa mji mkuu wa jimbo la Helmand itakuwa ni ishara kubwa ya thamani kwa wapiganaji wa Taliban huku wakiendelea kusonga mbele kwa kasi baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni. Mji wa Helmand ulikuwa ni kituo cha amani cha harakati za kijeshi za Marekani na Uingereza

Umoja wa Mataifa na mashirika mengine wanaonya juu ya hali mbaya zaidi ya mzozo wa kibinadamu. Takriban raia 40 wameuawa katika eneo la Lashkar Gah kwa kipindi cha siku moja iliyopita. Ulisema Umoja wa Mataifa Jumanne.

Jeshi la Afghanistan limewataka raia kuondoka Lashkar Gah kabla ya mashambulio makubwa dhidi ya Taliban, ambacho ni kikundi chenye itikadi kali za Kiislamu ambacho kilifurushwa madarakani na vikosi vilivyoongozwa na Marekani miaka 20 iliyopita.

Kwingineko kusini,Taliban wanajaribu kuiteka tena Kandahar, ambayo ni ngome yao ya zamani, na makabiliano pia yameshika kasi katika eneo la Herat magharibi mwa nchi.

Mapigano yamekuwa yakiendelea katika Lashkar Gah kwa siku kadhaa, huku wanamgambo wakiripotiwa sasa kudhibiti nyingi kati ya wilaya za jimbo hilo.

"Tunapitia siku ngumu ," mwanafunzi mmoja katika mji huo aliiambia BBC. "Taliban waliwasha moto ardhini huku vikosi vya serikali vikipiga makombora angani."

Mwanaume mwingine alisema Jumapili kwamba: "Taliban wanaweza kuonekana katika barabara za jiji. Uwepo wa Taliban umewatisha na kuwashangaza watu hapa.

"Maduka yamefungwa, na magari ya majeshi ya serikali yameharibiwa na kuachwa katikatika ya barabara. Vita vinaendelea katika mita chachekutoka kwenye ofisi ya gavana na Makao makuu ya usalama.

"Serikali kuu hivi karibuni ilisema wamepeleka makomandoo wapya Lashkar Gah, lakini hatukuwaona."

Mamia ya wanajeshi wa Afghanstan wameripotiwa kupelekwa katika mji huo kwa sasa.

Mwishoni mwa juma, Attaullah Afghan, mkuu wa baraza la jimbo la Helmand, alikiri kuwa mapigano yanaonekana "kutoweza kudhibitiwa".

Taliban wamesonga mbele zaidi wiki hii, licha ya mashambulio ya anga ya Afghanstan na Marekani yanayowalenga.

Kuna ripoti kwamba wapiganaji wa Taliban wamejificha kwenye nyumba, maduka huku mapigano yakiendelea kwenye mitaa.

Wanamgambo huwaonya watu kwa ujumla kwa njia ya vipaza sauti kuondoka lakini mara nyingine huingia ndani ya nyumba-wakazi wanakuwa na dakika chache za kutoroka au kukabiliwa na hatari ya kujipata katika mapigano ya risasi kwani nyumba zao zinakuwa sehemu ya uwanja wa mapigano.

"Taliban walituambia kama hatutaondoka nyumbani katika kipindi cha nusu saa,tutahesabiwa kuwa miongoni mwa polisi na jeshi la Afghanstan,''alisema mwanafunzi aliyezungumza na BBC Idhaa ya Afghanstan.

Wakati wa utawala wao katika miaka ya 1990. Taliban waliwauwa watu wazi wazi na kuwazuia wanawake kupata ellimu na ajira.

Taliban wanasema wamebadilika na hawawezi kufanya ghasia za aina hiyo-lakini Waafghanstan wengi hawana imani na kauli hiyo.

Shirika la kutetea haki za binasamu la kimataifa -Human Rights Watch limerekodi visa vya mashambulio mabaya ya wanamgambohao dhidi ya raia ambao walionekana kuiunga mkono serikali.

Umoja wa Mataifa unasema raia wanalipa garama ya vita na umezitaka pande zote husika kufanya juhudi za kuwalinda raia la sivyo athari itakuwa janga.

Maelfu ambao walikimbia mapigano sasa wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, maji ya kunywa na dawa.

Video za maasi yaliyoripotiwa kufanywa na Talibanzinasambazwa kwneye mitandao ya kijami, na kusababisha hofu zaidi ya uwezekano wa kurejea kwao.

Marekani na Uingereza zinasema kundi hilo huenda lilitekeleza uhalifu wa kivita, zikiwashutumu waasi hao kwa mauaji ya makumi kadhaa ya raia kulipiza kisasi katika Spin Boldak, kwenye mpaka na Pakistan.

Kuna ripoti pia kwamba watu 40 wa jamii ya Hazaras wa madhehebu ya Shia Waislamu walio wachache walilengwa na kuuawa katika eneo la Malistan lililopo katika jimbo la mashariki la Ghazni.

Taliban wamepuuzilia mbali shutuma hizo wakizitaja kama zisizokuwa na msingi, na wanatuma picha zao za raia wanaosema wamejeruhiwa katika mashambulio ya anga ya ndege za Afghanstan na Marekani.

Mashirika ya misaada hayawezi kuwafikia wengi wa watu waliosambaratishwa na vita, na vituo vya afya na hospitali hazina uwezo wa kukabiliana na idadi ya majeruhi. Baadhi ya vituo vya afya vimeangamizwa, huku vingine vikiwa havifanyi kazi.

Daktar aliyepo Lashkar Gah, Masood Khan, alisema ongezeko la wakati wote la wagonjwa waliojeruhiwa vibaya wanaowasili katika hospitali, na ana hofu wengine hawawezi kuifikia. Alisema bidhaa za matibabu zinapungua.

"Tunapokea majeruhi wengi wa vita…Kuna mapigano kila mahali," Dkt Kahn, mtaalamu wa matibabu ya dharura katika hospitali inayosimamiwa na shirika la msaada wa matibabu MSF, aliiambia BBC Jumatatu

Wale waliokwama katika mapigano yanayoendelea kuwa mabaya wana fursa chache.

"Hatuna mkate wala maji katika nyumba zetu, na umeme umekatwa kabisa ," mfanyabiashara mkazi wa Laskhar Gah aliiambia BBC.

"Sijui pa kwenda, kuna mapigano katika kila kona ya mji "

Mkalimani Muafghanstan anayeishi katika mji huo anasema maisha yake yamo hatarini kwasababu ya vitisho vya Taliban kutokana na kwamba alikuwa akifanyia kazi vikosi vya Uingereza.

"Nimebadilisha anuani mara tatu. Nyumba yangu imechukuliwa na Taliban na wanaishi pale na walikuwa wananiulizia ," alisema.

"hatujui ni nini kitakachotokea siku zijazo kama wanasaka nyumba kwa nyumba kuwatafuta watu waliokuwa wafanyakazi wa NATO ."