Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afghanistan: Wakaazi wa Lashkar Gah watakiwa kuhama mji huo huku mapambano na Taliban yakiendelea
Jenerali mmoja wa Afghanistan ameonya kuhusu kutokea kwa madhara makubwa ya kiusalama kimataifa iwapo kundi la Taiban litashinda vita dhidi ya majeshi ya serikali ya nchi hiyo. Afisa huyo wa jeshi amewahimiza raia kuhama mji huo huku jeshi likiendelea na oparesheni dhidi ya Taliban
Jenerali Sami Sadat anaongoza mapambano dhidi ya kundi hilo la Taliban huko Kusini mwa jimbo la Helmand, ambapo mapigano makali yameibuka katika makao makuu yake ya mji wa Lashkar Gah.
Kundi la Taliban linashikilia wilaya kadhaa za katikati ya jiji hilo.
Lakini Jenerali Sadat alisema alikuwa na uhakika kwamba kundi hilo halitaweza kulidhibiti jiji lote.
Hata hivyo ameiambia BBC kwamba, kundi hilo linapewa usaidizi na wapiganaji wa kiislamu na kuonya kwamba hatua hiyo si tishio kwa Afghanistan bali hata kwa mataifa mengine ya nje.
"Hii itaongeza matumaini kwa vikundi vidogo vidogo kujiunga katika majiji ya nchi za Ulaya na Marekani na hivyo kuwa tishio kwa uslama wa dunia, " alisema.
"Hivi sio vita vya Afghanistan, vita hivi ni kati ya uhuru na ubabe".
Mashambulizi yanayofanywa na Taliban katika jimbo la Helmand ni sehemu ya mashambulizi makubwa yanayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Afghanistan.
Helmand ilikuwa kitovu cha kampeni za kijeshi kwa majeshi ya kigeni ya Marekani na Uingereza ushindi wowote wa Taliban utakuwa pigo kubwa kwa serikali ya Afghanistan.
Kama Taliban watautwaa mji wa Lashkar Gah, itakuwa mara ya kwanza kwa kundi hilo kudhibiti makao makuu ya mji tangu mwaka 2016. Makao makuu hayo ni moja kati ya matatu yanayoshambuliwa na kundi hilo.
Mapigano Helmand
Mapigano makali yanaendelea katika mji mkubwa wa Afghanistan, huku kukiwa na hofu kuwa huenda ukawa mji wa kwanza kuangukia mikononi mwa Taliban.
Lashkar Gah katika mji wa kusini mwa jimbo la Helmand liko mwenye mashambulizi makali kutoka kwa wanamgambo, licha ya mashambulio ya angani ya Marekani na Afghanistan.
Taliban wanasemekana kukidhibiti kituo cha runinga. Maelfu ya watu waliokimbia maeneo ya vijijini walikimbilia katika majengo.
"Kuna mapigano pande zote," daktari aliiambia BBC kutoka kwenye hospitali yake.
Mamia ya wanajeshi wa Afghanistan waepelekwa kupigana na wanamgambo hao. Taliban wamedhibiti haraka maeneo kadhaa katika miezi ya hivi karibuni wakati vikosi vya Marekani vikiondoka baada ya miaka 20 ya operesheni za kijeshi nchini humo.
Helmand kilikuwa kitovu cha kampeni ya jeshi la Marekani na Uingereza, na mafanikio ya Taliban huko yangekuwa pigo kwa serikali ya Afghanistan.
Kama Lashkar Gah ikianguka mikononi mwa Taliban, itakuwa mji wa kwanza kunyakuliwa na Taliban tangu mwaka 2016. Ni moja kati ya miji mitatu iliyokumbwa na mashambulizi.
Kamanda wa jeshi la Afghanistan katika mji huo alitahadharisha kuwa ushindi wa Taliban ungekuwa ''athari mbaya kwa usalama wa dunia''.
''Hivi si vita vya Afghanistan, hivi ni vita kati ya uhuru na udikteta,'' alisema Meja Jenerali Sadaat alipozungumza na BBC.
Jumatatu, wizara ya habari nchini Afghanistan ilitangaza kuwa redio 11 na televisheni nne katika jimbo la Helmand ziliacha kutangaza kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ''mashambulizi na vitisho'' vya Taliban.
Majaribio ya wanamgambo kudhibiri Kandahar, mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, yameendelea baada ya mashambulizi ya roketi kupiga uwanja wa ndege wa mji huo Jumapili.
Kuunyakua mji wa Kandahar itakuwa ishara kubwa ya ushindi wa Taliban, na kuwapa nguvu kusini mwa nchi hyo.
Katika mji wa tatu uliozingirwa wa Herat, upande wa magharibi, makomandoo wa serikali wanapambana na wanamgambo. Vikosi vya serikali vimechukua maeneo kadhaa kutoka mikononi mwa waasi baada eneo la majengo ya Umoja wa Mataifa kushambuliwa Ijumaa.
Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha wakazi kwenye mitaa na waliokuwa juu ya paa wakitamka kwa ngungu ''Allahu akbar'' (Mungu ni mkubwa) wakiunga mkono mafanikio ya serikali.
Wakati vikosi vya serikali vikipambana kurejesha maeneo yanayodhibitiwa na Taliban, Rais Ashraf Ghani amelaumu kuondoka kwa vikosi vya Marekani ambako kumezidisha mapigano nchini humo.
''Sababu ya hali tulionayo sasa ni kuwa uamuzi ulichukuliwa ghafla, '' aliliambia bunge.
Bw. Ghani amesema aliipa angalizo Washington kuwa kuondoka kutasababisha ''madhara''.
Ingawa karibu vikosi vyote vya kijeshi vimeondoka, Marekani imeendelea na mashambulizi ya anga kuyasaidia majeshi ya serikali. Mashambulizi yanayolenga mji wa Lashkar Gah yaliendelea mpaka usiku wa Jumatatu.
Utawala wa Rais Biden ulitangaza siku ya Jumatatu kuwa kwasababu ya ongezeko la machafuko, itawachukua maelfu ya wakimbizo wa Afghanistan waliofanya kazi na vikosi vya Marekani.
Marakani na Uingereza zimeshutumu Taliban kwa kutekeleza uhalifu wa kivita kwa ''kuwaua raia'' katika mji ulio mpakani na Pakistan.
Waziri wa Mambo ya nje Antony Blinken amesema ameona ripoti za ''kutamausha na ambazo hazikubaliki'' za ukatili wa Taliban.
Video za kutisha ambazo zilitoka kwenye mji wa Spin Boldak zilionesha mauaji ya kulipiza kisasi. Taliban wamekana shutuma hizo.