Bill Cosby: Wajue watu wengine maarufu waliofungwa na kuachiwa

BILL

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Wanaweza kuwa ni matajiri wa kutupwa, warembo kupitiliza na maarufu kila pembe ya dunia, lakini watu maarufu ni binadamu tu kama walivyo binadamu wengine, wanaingia kwenye matatizo kama wanavyoingia watu wengine wa kawaida.

Si kila mashitaka wanayopewa yanakuwa ya kweli kuna wakati mwingine kwa umaarufu wao wanajikuta matatizoni na kusingiziwa kesi mbalimbali hasa za ubakaji ili baadhi ya watu waweze kunufaika na kesi hizo.

Hivi majuzi mchekeshaji maarufu wa Marekani, Bill Cosby ameachiwa huru na Mahakama Pennsylvania baada ya hukumu yake ya unyanyasaji kingono kutenguliwa. Bwana Cosby, 83, alitumikia miaka zaidi ya miwili ya kifungo chake cha miaka 10 katika gereza la serikali huko Philadelphia.

Hii linaongeza idadi ya kesi zenye utata na viashiria vya kubabimbikiziwa zinazowahusu watu maarufu hasa weusi wenye asili ya Afrika.

Hilo linatoa nafasi kwa BBC kukuletea orodha ya angalau watu wanne maarufu weusi, ambao walikumbana na mashitaka ya yaliyozungumzwa sana na kujikuta matatani gerezaji lakini baadae kuachiwa huru.

THE SNOOP DOGG

Snoop

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Snoop, rapa na muigizaji wa siku nyingi

The Snoop Dogg ambaye anapendwa mpaka leo na mashabiki alikuwa mtu tofautri kabisa miaka hiyo ya enzi za ujana wake. Alikua sehemu ya magenge yenye kujaa uhalifu na vurugu za kila aina.

Akiwa kwenye maandalizi ya albamu yake nyota huyu wa hip hop akafikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji, ilikuwa mwaka 1993.

Kwa mujibu wa gazeti la The Washington Post, miezi michaze kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza, Doggystyle, Snoop na mlinzi wake binafsi walitajwa kuhusika kwenye vurugu dhidi ya genge lingine huko California , vurugu zilizosababisha kifo cha Phillip Woldemariam, aliyekuwa na miaka 20.

Shuhuda akawaeleza Polisi kwamba Snoop wakiwa garini na mlinzi wake, McKinley Lee, walishiriki vurugu hizo ambazo zilimuhusisha pia Woldemariam.

Ingawa ushahidi wa mashahidi ulitofautiana , ilielezwa kwamba Woldemariam alikuwa na bunduki wakati wa majibizano ya risasi.

Hakuna ushahidi wa moja kwa moja ulioonyesha Snoop kuua lakini aliwekwa jela. Snoop ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus Jr. na mlinzi wake Lee waliwekwa ndani kwa makosa ya mauaji lakini mwaka 1996 waliachiwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa za wakili wa utetezi, Donald Re aliyeeleza kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times), ni kwamba, kosa kubwa walilofanya Polisi kwenye kesi hiyo ni kufumbia macho ukweli.

OJ SIMPSON

OJ

Chanzo cha picha, Google

Alikuwa mmoja wa watu mashuhuri sana nchini Marekani, mbali na soka la Marekani, alikuwa muigizaji mkubwa akijijengea umaarufu wake kwenye filamu ya Dragnet 1967, ambapo aliigiza nafasi ya mtu ambayo hajazungumza neon hata moja.

Mwaka 2008 alihukumiwa miaka 33 jela kwa tuhuma za unyanganyi wa kutumia silaha na utekaji huko Las Vegas, lakini miaka tisa baadae yaani mwaka 2017 aliachiwa huru. Masuala ya rangi yalitajwa kuwa sehemu kubwa suala lililochukua nafasi kubwa.

Heka heka na matatizo ya Simpson yalianza kitambo, mfano mwaka 1994 alishitakiwa kwa mauaji ya watu wawili, lakini baada ya kesi kusikilizwa kwa miezi 11, Simpson aliachiwa huru. Kesi yake inatajwa kuvutia watu zaidi ya milioni 100 ambao walifuatilia siku ya hukumu.

BRIAN BANKS

BANKS

Brian Banks alikua mwanafunzi na mmoja wa vijana waliotarajiwa kughara sana kwenye ligi ya soka ya la Marekani (NFL miaka ya 2000, lakini tuhuma za ubakaji zilizotolewa na mwanafunzi mwenzake zikaua ndoto zake za kufanikiwa kwa haraka.

Kwenye kesi hiyo, alipaswa kuchagua kesi kwenda mahakamani na iwapo angekutwa na hatia angefungwa miaka 41, ama kuigia kwenye makubaliano 'plea deal' ili adhabu yake iwe na haueni. Kwa sababu ilikuwa kesi kubwa kwa umri wake, aliamua kuchukua njia ya pili, alikaa jela miaka 5, huku aliyemshitaki akijipatia dola milioni 1.5 kutoka kwenye Mamlka za shule aliyokuwa anasoma Banks.

Lakini mwaka 2012, yule aliyemshitaki alijitokeza na kumfuata Banks na kukiri kwamba alitunga tu uongo kuhusu ubakaji. Pamoja na hilo, miaka aliyokaaa jela haiwezi kurejeshwaIn 2012, lakini angalau ndoto zake za kucheza NFL zilitimia. Mwaka 2013 alisajili na Atlanta Falcons,

Mwanamke aliyemtuhumu kumbaka alitakiwa na Mhakama kulipa dola milioni $2.6 kwa Mamlka za shule kwa kuiingiza kwenye kesi hiyo ya uongo.

DEWEY BOZELLA

Moslye

Chanzo cha picha, ABC

Maelezo ya picha, Kocha Howard Mosley (kulia) akimbusu Bozella kufuatia ushindi wake dhidi ya bondia Larry Hopkins. likuwa mchezo wa kwaza kwa Bozella tagu atoke kifungoni.

Mwanamasumbwi Dewey Bozella aliachiwa kutoka jela mwaka 2009, baada ya kutumia miaka 26 akiwa jela. Alifungwa akiwa kijana mdogo tu kufuatia mashtaka ya mwaka 1977 yaliyohusu kifo cha bibi kizee mwenye umri wa miaka 92. Bibi huyo alidaiwa kupigwa, kuteswa na kukabwa wakati akirejea nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, Bozella alihukumiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1983, lakini baadae mashtaka hayo yalifutwa baada ya kubainika yalikuwa na chembe ya uongo. Lakini mwaka 1990 alihukumiwa tena kwa kesi hiyo hiyo, baada ya watu wawili kubadilisha maelezo ya ushahidi wao.

Mwaka 2009, Jaji alitengua uamuzi wa awali akisema amhukumiwa kimakosa na kumuachia huru Bozella. Jaji alisema, uliachwa ushahidi muhimu wa jirani aliyesema alisikia kelele, na Polisi baadae wakabaini kukuta alama za mtu anayeitwa Donald Wise aliyehukumiwa kwa kosa la kumuua bibi kizee huyo. Mwkaa 2015, Mwanamasumbwi huyo alipewa kifuta machungu cha dola milioni $7.5 kwa kubambikiziwa kesi ya uongo na kufungwa.