Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Burna Boy awashinda Diamond Platinumz na Wizkid tuzo za BET Marekani
Mwanamuziki wa Nigeria Burna boy ndiye mshindi wa tuzo za BET kitengo cha kimataifa mwaka huu.
Burna Boy ambaye jina lake kamili ni Damini Ebunoluwa Ogulu alitawazwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuibuka mshindi 2019, 2020, na 2021.
Mwanamuziki huyo wa wimbo 'Omo' aliwashinda wapinzani wake kutoka Afrika akiwemo mwanamuziki maarufu wa Tanzania Naseeb Abdul Juma maarufu Diamond Platinumz na Wizkid wa Nigeria.
Wengine waliokuwa wameteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na mwanamuziki wa Brazil Emicida, Headie One kutoka Uingereza, Aya Nakamura kutoka Ufaransa ,Young T & Bugsey kutoka Uingereza na mwanamuziki Youssopha Kutoka Ufaransa.
Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platinumz aliyekuwa katika nafasi nzuri mwaka huu kushinda taji hilo hakufanikiwa kwa mara nyengine.
Hatahivyo msanii huyo ameweka chapisho katika mtandao wake wa Instagram akiwapongeza Watanzania kwa umoja wao wakati wa Tuzo hiyo.
Tangazo hilo linajiri huku baadhi ya raia wa Tanzania wakianzisha kampeni ya kutaka atimuliwe katika tuzo hizo kwa madai kwamba amekuwa akiunga mkono utawala wa kiimla.
Zaidi ya Watazania 20, 000 walitia saini pingamizi dhidi yake mtandaoni wakitaka nyota huyo wa muziki wa bongo fleva kutimuliwa katika tuzo hizo.
Mada kuu ya tuzo hiyo mwaka huu ilikuwa ''Mwaka wa Mwanamke Mweusi'' ambapo nyota wa filamu ambaye pia ni mshindi wa tuzo mbalimbali Taraji P Henson ndiye aliyekuwa mwenyeji wake.
Tuzo hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Microsoft mjini Los Angeles ambapo umati mkubwa wa watu ulihudhuria licha ya kuwepo kwa mlipuko wa corona..
Mwanamuziki mkongwe wa Rap na Muigizaji Queen Latifa alikabidhiwa tuzo ya Maisha mwaka huu kutokana na ufanisi wa kazi yake .
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Rap DMX, aliyefariki kutokana na mshtuko wa Moyo alipatiwa heshima kubwa katika tuzo hiyo ambapo wanamuziki Busta Rhymes, Method Man, Swizz Beatz, Griselda walimkumbuka kwa kumuimbia.
Je Burna boy ni nani?
Damini Ebunoluwa Ogulu ni mwanamuziki maarufu kutoka nchini Nigeria anayefahamika kwa jina la Burna Boy.
Alizaliwa Julai 2, 1991.
Ameweza kutunukiwa tuzo kadhaa katika uimbaji wake, kuandika nyimbo na umahiri wa kucheza.
Anatajwa kuwa mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa barani Afrika.
Katika tuzo za mwaka huu, za BET zimemtunuku tena Burna Boy ushinda.
Mashindano hayo ambayo yalifanyika usiku wa kuamkia Jumapili, yalimfanya Burna Boy kupata tuzo katika kipengele cha The best International act .
Mapema mwaka huu, Burna Boy alishiriki kwa mwaka wa pili mfululizo na kushinda katika albamu yake ya Twice As Tall .
Burna Boy, mwenye miaka 29, aliwashinda wengine wanne ikiwemo bendi ya Malian, Tinariwen.
Tuzo za BET zimeielezea albamu yake ya Twice As Tall kuwa muziki uliotengenezwa kwa kiwango cha juu cha kimataifa, na imemfanya Burna Boy kuingia katika kiwango hicho cha kimataifa".
"Aliendelea kusema kuwa albamu hiyo imechanganya miondoko mbalimbali kama midundo ya pop, Afrobeat, dancehall, reggae na miondoko mingine mingi," walieleza.
Albumu yake ilishirikisha wanamuziki wengi duniani wakiwemo Stormzy, Youssou Ndour, Naughty By Nature, na Chris Martin wa Coldplay, na vilevile Sean Combs akiwa muandaaji mkuu.
Burna Boy amechaguliwa katika kipengele kile kile cha mwaka 2019 - kinachojulikana kama 'Best World Music Album' - lakini Angelique Kidjo aishinda katika tuzo za mwaka 2020.
Ingawa Kidjo aliamua kutoa ushindi wake kwa Burna Boy, alisema: "Burna Boy ni miongoni mwa wasanii wachanga ambao wanatoka Afrika ambao wanabadili mtazamo wa muziki wa Afrika."
Mwanamuziki huyu aliyezaliwa Nigeria, alizindua albamu yake ya kwanza ya LIFE, mwaka 2013.
Na baadae alizindua albamu ya Redemption mwaka 2015 na Outside mwaka 2018 ambayo ilijumuisha ngoma iliyovuma kimataifa ya , Ye.
Lakini ilikuwa katika albamu yake ya mwaka 2019 ya African Giant ambapo Burna Boy alipata umaarufu zaidi kimataifa na kupata tuzo yake ya kwanza ya BET.
Akiwa analinganishwa na mwanamuziki wa Nigeria Fela Ransome-Kuti na kupata umaarufu barani Afrika.
Wakati wa mgogoro wa ubaguzi Afrika Kusini mwaka 2019, alitishia kutoenda katika taifa hilo kama serikali ya nchi hiyo haitachukua hatua dhidi ya xenophobic.
Pia alijumuishwa katika maandamano ya #EndSARS ya kupinga unyanyasaji wa polisi, alitoa wimbo wa wahanga ambao waliuawa katika maandamano hayo Oktoba 20,2020 katika geti la Lekki Toll Gate mjini Lagos.
Vilevile ameandika katika kurasa yake ya tweeter kuunga mkono waandamanaji wa Senegal ambao walijitokeza barabarani baada ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko kukamatwa.
Ifuatayo ni orodha za washindi wa tuzo hizo.
Albamu ya Mwaka
- "Heaux Tales" Jazmine Sullivan — Mshindi
- "Ungodly Hour" — Chloe x Halle
- "King's Disease" — Nas
- "Good News" — Megan Thee Stallion
- "Blame it on Baby" — DaBaby
- "After Hours" — The Weeknd
Mwanamuziki bora wa kike wa R&B / Pop
- H.E.R. — Mshindi
- Beyoncé
- Jazmine Sullivan
- Jhené Aiko
- Summer Walker
- Sza
Mwanamuziki bora wa kiume wa R&B / Pop
- 6LACK
- Anderson .Paak
- Chris Brown
- Giveon
- Tank
- The Weeknd
Kundi Bora la muziki
- Bruno Mars, Anderson .Paak and Silk Sonic — Mshindi
- 21 Savage & Metro Boomin
- Chloe X Halle
- Chris Brown & Young Thug
- City Girls
- Migos
Ushirikiano bora wa muziki{ Collabo}
- "WAP" — Cardi B ft. Megan Thee Stallion
- "Rockstar" — DaBaby ft. Roddy Ricch
- "Popstar" — DJ Khaled ft. Drake
- "What's Poppin (Remix)" — Jack Harlow ft. DaBaby, Tory Lanez and Lil Wayne
- "Cry Baby" — Megan Thee Stallion ft. DaBaby
- "For the Night" — Pop Smoke ft. Lil Baby and DaBaby
Mwanamuziki Bora wa kiume wa Hip Hop
- Lil Baby — Mshindi
- DaBaby
- Drake
- J. Cole
- Jack Harlow
- Pop Smoke
Mwanamuziki bora wa kike wa Hip Hop
- Megan Thee Stallion — Mshindi
- Cardi B
- Coi Leray
- Doja Cat
- Latto
- Saweetie
Video bora ya Mwaka
- "WAP" Cardi B ft. Megan Thee Stallion — Mshindi
- "Up" — Cardi B
- "Do It" — Chloe x Halle
- "Go Crazy" — Chris Brown and Young Thug
- "Laugh Now Cry Later" — Drake ft. Lil Durk
- "Leave the Door Open" — Bruno Mars, Anderson .Paak and Silk Sonic
Muelekezi bora wa Video mwaka huu
- Benny Boom
- Bruno Mars & Florent Déchard
- Cole Bennett
- Colin Tilley
- Dave Meyers
- Hype Williams
Msanii Bora mpya
- Giveon — Mshindi
- Coi Leray
- Flo Milli
- Jack Harlow
- Latto
- Pooh Shiesty
Dr. Bobby Jones Best Gospel / Inspirational Award
- "In Jesus Name" — Bebe Winans
- "Never Lost" — Cece Winans
- "Hold Us Together" — H.E.R.
- "Strong God" — Kirk Franklin
- "Thank You For It All" — Marvin Sapp
- "Touch From You" — Tamela Mann
Tuzo ya BET Her Award
- "Good Days" Sza — Winner
- "So Done" — Alicia Keys ft. Khalid
- "Baby Mama" — Brandy ft. Chance the Rapper
- "Anti Queen" — Bri Steves
- "Baby Girl" — Chloe x Halle
- "Rooted" — Ciara ft. Ester Dean
Tuzo ya Kimataifa
- Burna Boy, Nigeria — Mshindi
- Aya Nakamura — France
- Diamond Platnumz — Tanzania
- Emicida — Brazil
- Headie One — United Kingdom
- Wizkid — Nigeria
- Young T & Bugsey — United Kingdom
- Youssopha — France
Tuzo ya watazamaji
- "Savage (Remix)" Megan Thee Stallion ft. Beyoncé - Mshindi
- "WAP" - Cardi B ft. Megan Thee Stallion
- "Go Crazy" - Chris Brown & Young Thug
- "Rockstar" - DaBaby ft. Roddy Ricch
- "Popstar" - DJ Khaled ft. Drake
- "Laugh Now Cry Later" - Drake ft. Lil Durk
- "The Bigger Picture" - Lil Baby
- "Leave the Door Open" - Silk Sonic
Filamu Bora
- "Coming 2 America"
- "Ma Rainey's Black Bottom"
- "One Night in Miami"
- "Soul"
- "The United States Vs. Billie Holiday"
- "Judas and the Black Messiah"
Muigizaji Bora wa kike
- Andra Day — Mshindi
- Angela Bassett
- Issa Rae
- Jurnee Smollett
- Viola Davis
- Zendaya
- Best Actor
- Aldis Hodge
- Chadwick Boseman
- Damson Idris
- Daniel Kaluuya
- Eddie Murphy
- Lakeith Stanfield
Tuzo ya vijana :
- Alex R. Hibbert
- Ethan Hutchison
- Lonnie Chavis
- Marsai Martin
- Michael Epps
- Storm Reid
Mwanariadha bora wa kika mwaka huu:
- Naomi Osaka — Mshindi
- A'ja Wilson
- Candace Parker
- Claressa Shields
- Serena Williams
- Skylar Diggins-Smith
Mwanariadha bora wa kiume mwaka huu :
- Lebron James — Mshindi
- Kyrie Irving
- Patrick Mahomes
- Russell Westbrook
- Russell Wilson
- Stephen Curry
Chaguo la watazamaji kimataifa
- Bree Runway, United Kingdom — Mshindi
- Arlo Parks — United Kingdom
- Bramsito — France
- Elaine — South Africa
- MC Dricka — Brazil
- Ronisia — France
- Tems — Nigeria