Ajabu! Gari lililoegeshwa latumbukia na kupotea ndani ya shimo

Iliyochapishwa

Gari moja lililokuwa limeegeshwa limetumbukia na kupotea ndani ya shimo moja mjini Mumbai

Katika tukio lisilo la kawaida katika mji wa Mumbai ulionyeshewa na mvua kubwa gari hilo liliingia ndani ya shimo hilo.

Shimo hilo ambapo lilikuwa limezibwa juu kwa kumwagiwa zege na lami lilibomoka, polisi walisema siku ya Jumapili.

Mmiliki wa gari hilo alisema : Sikuwahi kufikiria kitu kama hiki kitafanyika, na sikujuwa kwamba kulikuwa na kisima chini ya eneo la kuegesha magari.