Canada yaomboleza baada ya mabaki ya watoto 215 kupatikana katika shule moja

A new classroom building at the Kamloops Indian Residential School is seen in Kamloops, British Columbia, Canada circa 1950

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Shule ya Kihindi ya British Columbia wakati mmoja ilikuwa na watoto 500
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Kaburi la pamoja lililokuwa na mabaki ya watoto 215 limepatikana nchini Canada katika shule ya zamani ya makazi iliyobuniwa ili kuwajumuisha watu wa asili

Watoto hao walikuwa wanafunzi wa shule ya makazi ya Kihindi ya Kamloops ya Waingereza wa Columbia ambayo ilifungwa mnamo 1978

Uvumbuzi huo ulitangazwa siku ya Alhamisi na mkuu wa First Nation, Tk'emlups te Secwepemc .

Waziri Mkuu Justin Trudeau alisema ilikuwa "kumbukumbu ya machungu" ya "ukurasa wa aibu katika histori aya nchi yetu".

First Nation inafanya kazi na wataalamu wa makavazi na ofisi ya habari kubaini chanzo na muda wa vifo hivyo, ambao kwa sasa haijulikani.

Rosanne Casimir, mkuu wa jamii ya Waingereza wa Columbia katika mji wa Kamloops, alisema uchunguzi wa awali unaashiria upotevu wa kusikitisha ya waendeshaji wa shule hiyo ambao hawakunakiliwa.

Shule za makazi nchini Canada zilikuwa shule za mabweni za lazima ambazo zilikuwa zikiendeshwa na serikali na mamlaka za kidini katika karne 19 na 20 ka lengo la kuwajumuisha na kuwaleta pamoja vijana wa asil.

Shule ya Kihindi ya Kamloops ilikuwa kubwa sana katika mfumo wa shule za makazi. Ilifunguliwa chini ya utawala wa Wakatoliki wa Roma mwaka 1890, ilikuwa na wanafunzi 500 wakati wa kilele cha usajili miaka ya 1950.

Serikali Kuu ilichukuwa usimamizi wa wa shule hiyo mwaka 1969, kuendesha kama makazi ya wanafunzi wa eneo hilo hadi mwaka 1978, wakati ilipofungwa.

Tunafahamu nini kuhusu mabaki hayo?

Tk'emlups te Secwepemc ya First Nation imesema mabaki hayo yalipatikana kwa msaada wa rada inayopenya ardhini wakati wa uchunguzi wa shule hiyo.

"Kwa ufahamu wetu, watoto hawa waliopotea ni vifo visivyo na hati," Bu Casimir alisema. "Baadhi yao walikuwa watoto wa miaka mitatu."

"Tulitafuta njia ya kudhibitisha kwa kuzingatia heshima na upendo wa dhati kwa wale watoto waliopotea na familia zao, tukifahamu kuwa Tk'emlups te Secwepemc ndio mahali pa kupumzika pa watoto hawa."

The main administrative building at the Kamloops Indian Residential School is seen in Kamloops, British Columbia

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Uchunguzi wa mabaki bado unaendelea

Kabila hilo lilisema limefikia jamii za nyumbani ambazo watoto wao walisoma shule hiyo. Walitarajia kuwa na matokeo ya awali katikati ya Juni.

Taarifa hii imepokelewaje?

Taarifa ya ugunduzi huo imepokelewa kwa mshutuko na majonzi makubwa.

"Habari za mabaki ya miili ya watoto zilizopatikana katika shule ya zamani ya makazi ya Kamloops zinavunja moyo wangu," Bwana Trudeau aliandika kwenye tweet.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Waziri wa uhusiano wa asili wa Canada, Carolyn Bennett, alisema shule za makazi ni sehemu ya sera ya "aibu" ya kikoloni. Serikali ilijitolea "kuwakumbuka wale waliopoteza roho wasio na hatia", alisema.

Terry Teegee, mkuu wa bunge la eneo la Waingereza wa Columbia la First Nations, ametoa wito wa kutafuta makaburi kama hayo kuwa "shughuli ya dharura" ambayo "inatonesha na kuibua upya majonzi " ya jamii ya eneo hilo.

Maoni hayo pia yameungwa mkono na makundi asilia,pamoja na Mamlaka ya Afya ya Mataifa ya Kwanza (FNHA).