Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi gari la walinzi lilivyokwepa kutekwa, hofu yatanda usalama wa dereva
Video ya kamera za ndani ya gari hilo inamuonesha Leo Prinsloo akiwa anaendesha lori lililobeba bidhaa ghali katika mji mkuu wa Pretoria.
Video hiyo ilisambazwa sana mtandaoni, na wengi wakisifu jinsi alivyokuwa mtulivu wakati shambulio hilo likiendelea.
Lakini Bwana Prinsloo - ambaye anaamini amepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa genge hilo - sasa ana anajihami na walinzi wenye silaha nje ya nyumba yake.
Picha zinaonesha wakati risasi zinaanza kulipiga gari, zikilenga madirisha ambayo ni maalumu kwa kutopitisha risasi.
Bwana Prinsloo, 52, ambaye ni afisa wa zamani wa udunguaji wa polisi anaendelea baki mtulivu wakati anageuza gari na kumwambia mwenzake Lloyd Mtombemi atoe achukue bunduki yake.
"Wanakuja kwetu hao," bwana Prinsloo anasema wakati harakati za mapigano zinaendelea.
Wawili hao, ambao walikuwa kwenye gari lenye silaha lililobeba simu za mkononi zenye thamani ya maelfu ya Randi za Afrika Kusini, hawakujeruhiwa wakati wa shambulio hilo mnamo Aprili 22.
Video imeenea mtandaoni, lakini Bwana Prinsloo sasa anahofia maisha yake baada ya kupokea vitisho kutoka kwa watu wanaodai kuwa wanachama wa genge la wahalifu wanaotaka kulipiza kisasi.
Bwana Prinsloo alipokea ujumbe wa maandishi - ambao BBC iliuona - ukisema: "Utalipa". Ujumbe mwingine uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii unasoma: "Utalipa na damu [kwa] pesa ambazo hatukuzipata".
BBC imeshindwa kuthibitisha ukweli wa vitisho hivyo.
"Tunalichukulia tukio hili kwa uzito unaotakiwa " Deon Coetzee, mkurugenzi mkuu wa Fortis Pro-Active Defense Solutions, kampuni ya usalama ambayo Bwana Prinsloo anafanya kazi, aliiambia BBC.
Kampuni hiyo imeweka walinzi nje ya nyumba ya Bwana Prinsloo kumlinda ikiwa atashambuliwa.
"Tunachukua tahadhari juu yake kila wakati - kwa kuwa, mara genge linapojua wewe ni nani inakuwa hatari sana," Bwana Coetzee alisema.
Bwana Prinsloo, ambaye huko nyuma ameshawahi kuwalinda Nelson Mandela, Mwanamfalme Charles na wanafamilia ya Kardashian, anasema sasa yuko tayari kila wakati kwa lolote baya linaloweza kutokea.
"Mara ya kwanza nilijua kuwa wapo ni pale risasi zilipoanza kufyatuliwa ," alimwambia mtangazaji wa runinga ya Afrika Kusini ya eNCA.
"Nilipiga pich kichwani mapema ya kile nitakachofanya na kwa uwezo wangu wote nilifanya kile ambachoakili yangu iliniambia nifanye, na hilo lilinisaidia siku ile."