Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu mataifa ambayo wabakaji wanaweza kuepuka mkono wa sheria kwa kufunga ndoa na waathiriwa
Amina Filali alikuwa na umri wa miaka 15 alipowaambia wazazi wake kwamba alikuwa amebakwa.
Familia yake kulingana na ushauri aliopewa na maafisa wa mahakama , kulingana na babake ilimlazimisha kumuoa mtu aliyembaka , mwanamume mwenye umri wa miaka 25.
Miezi kadhaa baadaye , baada ya kuripoti kushambuliwa na kunyanyaswa , msichana huyo alijitoa uhai akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kunywa sumu ya panya.
Amina alifariki 2012 katika Kijiji kimoja kidogo nchini Morocco na kesi yake ikazua maandamano na kampeni zilizofanywa na wanawake kote duniani.
Mwaka 2014 Bunge la Morocco hatimaye lilibadilisha sheria iliyoruhusu mbakaji kuepuka haki iwapo angemuoa mwathiriwa.
''Iwapo mtu atachochea ghasia polepole utajua ni wakati gani ambapo uchochezi huo ulisababisha madhara yaliotokea''?
Lakini sheria kama hizo bado zinatumika katika maeneo mengi ya dunia, ikiwemo Ouidah Marekani ya kusini, kulingana na ripoti ya hivi majuzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu UNFPA kwa jina ''Mwili wangu ni wangu''
Ripoti hiyo inasema kwamba takriban ya wanawake katika mataifa 57 yanayoendelea hawana haki na miili yao , na hunyimwa haki ya kuamua iwapo wanataka kushiriki tendo la ngono , kutumia njia za kujikinga ama kutafuta matibabu.
''Hili linafaa kutushangaza sisi sote'', alisema Mkurugenzi wa UNFPA Natalia Kanem .
Ukweli ni kwamba mamia ya mamilioni ya wasichana hawana haki ya miili yao. Maisha yao yanadhibitiwa na wengine.
Amina Filali, in the black and white image, committed suicide at the age of 16 after being forced to marry her rapist. His sister Hamida participated in the protests that led to a change in the law in Morocco.
Ubakaji na sharia zinazsomsamehe mbakaji ni mifano miwili ya ukiukaji wa mjuda mrefu ambao unashirikisha ukeketaji na vipimo vya ubikira.
Na hata mataifa yaliobadilisha sharia ya kumsamehe mabakaji iwapo angemuoa mwathiriwa nyenginezo zingesalia kuwa na matukio kama hayo.
Je ni mataifa gani ya kimataifa yenye sheria kama hizi?
Ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa inanukuu shirika moja lisilo la kiserikali mjini Washington.
Katika Ripoti yake 2017, shirika hilo linasema kwamba usawa umeangazia mifano ya mataifa katika eneo la mashariki ya kati na Afrika Kaskazini ambapo wabakaji wanaweza kuepuka haki kupitia kufunga ndoa na waathiriwa .
Mataifa hayo ni Iraq, Bahrain, Libya , Kuwait, Palestina, Tunisia, Jordan na Lebanon.
"Baadaya ya ripoti yetu na kampeni nyengine Tunisia, Jordan and Lebanon walipiga marufuku sheria hizo mwaka 2017 huku Palestina pia ikifanya hivyo 2018, Barbara Jimenez , wakili ambaye ni mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu na uwakilishaji wa usawa Marekani ya kusini..
Mifano mingine ilioonekana na Ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa ni Angola, Algeria, Cameroon , Equitorial Guinea, Eritrea, Syria na Tajikistan.
Waathiriwa wanaofunga ndoa na wabakaji wao wanajipata wamekwama katika ndoa ambazo zinawafanya kuendelea kubakwa na kunyanyaswa maishani mwao.