Moto uliozuka katika hospitali ya corona Iraq: Watu 82 wafariki baada ya 'tangi la Oksijeni kulipuka'
Takriban watu 82 wamefariki katika moto uliozuka katika hospitali ya kutibu wagonjwa wa Covid 19 katika mji mkuu wa Iraq Baghdad.
Zaidi ya watu 100 walijeruhiwa katika moto huo uliozuka katika hospitali ya Ibn Khatib siku ya Jumamosi usiku.
Ripoti zinasema kwamba ajali ilisababisha tangi la oksijeni kulipuka na kusababisha moto huo.
Kanda za video zinaonesha wazima moto wakijaribu kuuzima moto huo huku watu wakitoroka jumba hilo.
Waziri mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimi alitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa haraka kuhusu chanzo cha kile alichokitaja kuwa ajali mbaya.

Chanzo cha picha, Reuters
Mkuu wa ulinzi wa umma Jenerali Kadhim Bohan, alisema kwamba moto huo ulianzia katika chumba cha wagonjwa mahututi katika ghorofa iliotengwa kuwasaidia watu kupumua.
Takriban wagonjwa 30 walikuwa katika chumba hicho cha wagonjwa mahututi kilichotengewa watu waliokuwa hatarini na corona mjini Baghdad, chanzo kimoja cha hospitali kiliambia chombo cha habari cha AFP.
Wagonjwa wote wamehamishwa katika hospitali iliopo karibu.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Moto huo ulidhibitiwa mapema siku ya Jumapili , alisema mkuu wa ulinzi wa umma nchini humo.
Gavana wa mji wa Baghdad Mojammed Jaber aliunga mkono wito wa waziri mkuu kuhusu kufanyika kwa uchunguzi wa haraka ili kubaini iwapo kuna mtu yeyote anayepaswa kuchukuliwa hatua.
Katika taarifa , tume ya haki za kibinadamu inayomilikiwa na serikali imesema kuwa tukio hilo ni uhalifu dhidi ya wagonjwa waliochoshwa na ugonjwa wa corona.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hospitali za Iraq zimezidiwa na idadi ya wagonjwa wa Covid 19 wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo, ukiongezewa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kupuuzwa na ufisadi.
Maambukizi ya Covid yamekua yakiongezeka kwa kasi tangu mwezi februari nchini Iraq na idadi hiyo imepitisha kiwango cha wagonjwa milioni moja wiki hii.
Wizara ya Afya imerekodi wagonjwa 1,025,288 na vifo 15,217 .
Taifa hilo limezindua kampeni yake ya chanjo mwezi uliopita na imepokea dozi 650,000, nyingi zikitoka kwa mpango wa WHO wa Covax, ambao ni wa kusambaza chanjo duniani.













