Hata wanasayansi wameshindwa kujua ni nini knaochofanya chokoleti kuwa tamu

Chokoleti

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Iwe imeokwa, imeyeyushwa na kuwa kinywaji kitamu bado chokoleti ni moja ya vinavyopendwa zaidi duniani.

Hata wapenzi wakubwa zaidi wa chokoleti wanaweza wasijue viambato vinavyotumika, ladha yake inatokana na utengenezaji wake ambayo ni uchachishaji.

Ladha yake nzuri inatokana na vijidudu vinavyosaidia kubadilisha chokoleti mbichi na kuwa jinsi ilivyo.

Bado wanasayansi kutoka sehemu mbalimbali kama vile Peru, Ubelgiji hadi Ivory Coast wanafanya utafiti kujua kwanini uchachishaji unabadilisha ladha ya chokoleti.

Wakati mwingine huwa wanafanya uchachishaji kwa njia isiyo ya asili katika maabara. Wanachukua kakao ambayo mfano wake ni maharagwe kutoka kwa waliochachisha kwa njia halisi.

Wanafanya majaribio yao na kutaka watu kuonja ladha yake.

Mkulima wa cocoa

Chanzo cha picha, AFP

Baada ya majaribio hayo ya miongo kadhaa, watafiti wamefikia mengi ikiwemo kujua ni vijidudu gani hasa vinavyohusika na uchachishaji wa chokoleti, ladha yake na thamani yake.

A plantation owner in Ivory Coast checks the pods on one of his cacao trees. Issouf Sanogo/AFP via Getty Images

Kuanzia mbegu hadi chokoleti

Unachokijua kama chokoleti huanza kama mbegu kutoka kwa mti wa kakao. Lakini ni mchakato mrefu kuibadilisha hadi kuwa chokoleti

Ndani ya tunda

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwanza, wafanyakazi hutoa mbegu hiyo ambayo ipo kama maharagwe, na kukaushwa kwa kipindi cha siku 3 hadi 10 kabla ya kuwekwa chini ya jua. Kisha mbegu hiyo inachomwa, na kusagwa na sukari na wakati mwingine maziwa ya unga hadi mchanganyiko huo utakapokuwa laini kabisa.

Kipindi cha ukaushaji ndio uchachishaji unatokea kwa njia ya asili. Ladha ya chokoleti inajumuisha mengi wakati huo. Uchachishaji ndio kipindi ambapo thamani yake huimarishwa kupitia vijidudu, na hapo ndio kakao ambayo ni chungu kawaida hubadilika na kuwa yenye ladha.

Kazi inayofanywa na vijidudu

Uchachishaji wa kakao ni mchakato mrefu. Vijidudu ndio vinavyojitokeza ambavyo vinabadilisha ladha ya mbegu hiyo na kuifanya kuwa yenye ladha.

Hatua ya kwanza huenda ikawa maarufu kwa watengenezaji pombe nyumbani kwasababu inajumuisha hamira - baadhi ya hamira ikiwa ile ile inayotumika kutengeneza bia na mvinyo. Na kama ilivyo kwa bia zinazopendwa, hamira nyengine kwenye kakao iliyochachishwa inatengeneza pombe kwa kuchanganya sukari kwenye maharagwe.

Mchakato huo hutengeneza molekuli zenye ladha. Na hujichachisha kwenye mbegu na baadaye zinajitengeneza kuwa chokoleti.

Mchakato huo ukiwa unaendelea, oksijeni inaingia kwenye uchachishaji huku idadi ya hamira ikiendelea kupungua wakati bakteria zinachukua usukani.

Chokoleti

Chanzo cha picha, Getty Images

Na hatimaye, asidi iliyojitengeneza inaanza kuwa mvuke taratibu.

Kakao ni njia ya uchachishaji isiyo ya kawaida - ambapo wakulima wanategemea vijidudu vya sili kutengeneza ladha tamu.

Na mchakato huo wa uchachishaji: ndio kakao ya kawaida inabadilika, inatenngenezwa na kufanya kitu cha kawaida, kuwa kisicho cha kawaida ambapo miujiza ya vijidudu ndio inayotegemewa.