Prince Philip: Famili ya Ufalme yaomboleza huku Mtawala akizikwa

Iliyochapishwa

Mtawala wa Edinburg amezikwa katika mazishi ya kifamilia katika yaliyofanyika katika kanisa la St George .

Kiongozi wa kidini wa Windsor alitoa risala ya kuuenzi "ukaribu, ucheshi na utu " wakati wa sherehe.

Waombolezaji walivaa barakoa na walikaa mbali na hawakukaribiana kwa mujibu wa masharti yaliyotolewa ili kuzuia kueneakwa virusi vya corona, huku Malkia akiketi peke yake.

Kabla ya misa hiyo, watoto wa mtawala huyo walitembea nyuma ya msafara wa jeneza lake na kulikua na dakika moja ya kukaa kimya kote nchini.

Jeneza lake lilibebwa kwa mwendo mfupi hadi kanisa la St George kwa kutumia gari aina ya Land Rover, ambalo mtaalamu huyo alichangia katika kulifanyia marekebisho ya muundo wake.

Bintimfalme Anne na Mwanamfalme Charles walikua mstari wa mbele nyuma ya gari, wakifuatiwa na Mwanamfalme Edward na Mwanamfalme Andrew.

Mstari wa tatu, Mwanamfalme William na Prince Harry walitembea sambamba na binamu yao Peter Phillips.

Zaidi ya wanajeshi 730 walishiriki katika tukio hilo, lakini kulikuwa na ukomo wa waombolezaji 30 ndani ya Kanisa dogo la St George, kulingana na sheria za kukabiliana na virusi vya corona.

Mwanamfalme Philip alifariki katika Kasri la Windsor Ijumaa tarehe 9 Aprili, akiwa na umri wa miaka 99.

Msafara wa magari kuanzia kwenye kasri hadi katika kanisa dogo uliongozwa na bendi ya ufalme ya Grenadier Guards, Mameja Jenerali , na wakuu wa huduma za kijeshi.

Makamu wa Admiral Sir Timothy Laurence na Earl wa Snowdon pia walitembea nyuma ya jeneza , wakiwa na watu wa Familia ya Ufalme.

Malkia Elizabeth wa II, mwenye umri wa miaka 94, wasafiri na mpambe wa kike wa Bentley akiwa mwisho wa msafara.

Prince Philip alifariki dunia katika kasri la Windsor Ijumaa 9 Aprili, akiwa na umri wa miaka 99.

Msafara wa mazishi kutoka kasri hadi kanisani yaliongozwa na Bendi ya Walinzi wa Grenadier, chama cha Meja Jenerali, na wakuu wa huduma za jeshi.

Makamu wa Admiral Sir Timothy Laurence na Earl wa Snowdon pia walitembea nyuma ya jeneza, wakifuatwa na waanafamilia wa mtawala wa Duke na wafanyikazi wake .

Malkia, mwenye umri wa miaka 94, alisafiri na mama-mkwe katika gari la Bentley mwisho wa msafara huo .

Kufyatuliwa kwa saluti ya risasi katika maeneo tisa kote Uingereza, na huko Gibraltar, kuliashiria mwanzo na mwisho wa kimya cha dakika moja kote Uingereza

Hakuna ndege zilizotua au kupaa Heathrow kwa dakika sita kuwiana na kimya cha kipindi cha mazishi na hafla zote kuu za michezo ziliahirishwa ili kuepusha mgongano na mazishi.

Ibada ya mazishi ilifanywa na Mkuu wa Windsor, na Askofu Mkuu wa Canterbury alitangaza baraka zake .

Askari maalumu wa Royal Marines walipiga viashiria ili kuonyesha Utekelezaji - ishara kwamba mikono yote inapaswa kuwa tayari kwa vita - wakati jeneza lilipoteremshwa ndani ya Royal Vault mwisho wa misa hiyo ya mazishi .

Mkuu wa Windsor alitoa pongezi kwa "fadhili, ucheshi na ubinadamu" wa Prince Philip na "njia nyingi ambazo maisha yake marefu yamekuwa baraka kwetu".

"Tumehamasishwa na uaminifu wake usioyumba kwa Malkia wetu, na huduma yake kwa taifa na Jumuiya ya Madola, kwa ujasiri wake na imani," alisema wakati akitoa risala ya kumuaga.

Uhusiano wake na jeshi la Royal Navy na kupenda bahari pia ilikuwa angazio kubwa la misa hiyo lakini hakuna mahubiri yoyote yaliyotolewa, kulingana na matakwa yake.

Muziki ulijumuisha wimbo wa 1860 Baba wa Milele, Nguvu ya Kuokoa, na William Whiting, ambazo zinahusishwa na mabaharia na huduma za jeshi la baharini.

Kulikuwa na kwaya iliyopunguzwa ya waimbaji wanne lakini waombolezaji hawakuimba, kulingana na masharti ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Makao makuu ya Ufalme ya Buckingham Palace yalisema kuwa mipango ya mazishi ilirekebishwa kwa kuzingatia miongozo ya afya ya umma.

Lakini mambo ya sherehe vimesalia sambamba na matakwa ya Prince Philip na ibada yake imeonesha uhusiano wake wa karibu na jeshi na mambo ya kibinafsi ya maisha yake.

Kabla ya mazishi, Malkia alitoa kwa umma picha anayopenda mwenyewe na Duke wa Edinburgh, ikionyesha wakiwa huko Aberdeenshire.

Picha hiyo ilipigwa na Countess wa Wessex mnamo 2003, picha inaonyesha Malkia na mumewe wakipumzika katika uanja mdogo wa nyasi kwenye eneo la kuvutia Coyles of Muick, karibu na nyumba ya kibinafsi ya Malkia ya Balmoral.

Wageni 30 katika mazish hayo walivalia makoti ya kuomboleza na medali, au gauni la kawaida, lakini sio majwanda ya kijeshi.

Wanandoa wa watoto wao pamoja na wajukuu wao walikua miongoni mwa msafara wa waombolezaji wakiwemo wawili ambao wamefunga ndoa na wanawafalme katika miaka ya hiviri karibuni - Jack Brooksbank na Edoardo Mapelli Mozzi, waume za wanawafalme Eugenie na Beatrice.

Unaweza zaidi kusoma:

Lakini mkewe Mtawala wa Sussex, Duchess wa Sussex, yni mjamzito na ameshauriwa na madaktari kutosafiri kutoka Marekani.

Waombolezaji wengine ni watoto wa dada yake Malkia Princess Margaret, na jamaa watatu Wajerumani wa Prince Philip - Bernhard, Mrithi wa kifalme wa Baden; Donatus, Prince na Landgrave wa Hesse; na Prince Philipp wa Hohenlohe-Langenburg.

Unaweza pia kutazama: