Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Prince Philip: Malkia aitoa kwa umma mojawapo ya picha zake anazozithamini
Malkia Elizabeth ameitoa kwa umma moja ya picha zake anazozipenda sana akiwa pamoja na mume wake wa miaka 73 , Mtawala wa Edinburgh, katika siku ya mazishi yake.
Wanandoa hao wa ufalme wa Uingereza walipigwa picha hiyo wakiwa wamepumzika kwenye majani katika eneo zuri la Aberdeenshire katika picha iliyochukuliwa na mkuu wa kaunti ya Wessex mwaka 2003.
Philip anaonekana akiwa amelala nyuma, huku akiwa ameegemea kiwiko, huku kofia yake ikiwa imetundikwa kwenye goti lake.
Mazishi yake yatafanyika katika kasri la kifalme la Windsor Castle saa tisa kwa saa za Uingereza(15:00 BST) Jumamosi.
Watoto wa Mtawala huyo watatembea nyuma ya jeneza lake wakati wa matembezi ya kuusindikiza mwili wake.
Unaweza pia kusoma:
Katika picha hiyo iliyopigwa katika siku iliyokuwa ya jua karibu na mji wa Aberdeenshire wa Ballater, Malkia na Mwanamfalme Philip walionekana watulivu na walimtazama kwa tabasamu mkwe wao Sophie ambaye alipiga picha hiyo.
Malkia - alikua amevalia sketi, blauzi na sweta pamoja na shanga shingoni-huku wakiwa wameketi na mume wake.
Wakati huo huo , Mike Tindall, ambaye amemuoa mjukuu wa Malkia na Mwanamfalme Philip Zara Tindall, ametoa salamu zake za rambi rambi kwa baba mkwe wake Mtawala wa Edinburgh ambaye amemtaja kama "mwanaume aliyejitolea kwa familia yake ambaye hatakumbukwa tu bali atakayependwa daima ".
Mchezaji wa zamani wa timu ya raga ya Uingereza alituma picha kwenye mtandao wa Instagram kutoka katika albamu ya picha za kibinafsi ya Familia ya ufalme ya Mwanamfalme Philip akiwa pamoja na mtoto mkubwa wa kike wa Tindall Mia.
Picha hiyo iliyochukuliwa na Wanamfalme wa Cambridge, inamuonesha Mia na babu yake mzaa baba wakila chakula pamoja kwenye benchi mbele ya nyumba ndogo iliyojengwa kwa mbao.
Nusu glasi ya bia inaonekana nyuma ya Mwanamfalme upande wa mkono wake wa kulia.
"Imekua ni wiki ya huzuni sana lakini imetupatia muda wa kutafakari kuhusu kumbukumbu nzuri na hadithi za kibinafsi na tulizoshirikishana ," Bw Tindall alisema.
Mke wa Tindall aijifungua mtoto wake wa tatu wiki tatu tu zilizopita na akamuita Lucas Philip, ambapo jina lake la kati kati alipewa kwa heshima ya Mtawala wa Edinburgh, baba yake Bw Tindall.
Katika wiki tangu alipofariki Mwanamfalme Philip akiwa na umri wa miaka 99, wanafamilia kadhaa wa familia ya ufalme wamekuwa wakichapisha picha ambazo awali hazikuwahi kuonekana.