Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Prince Philip: Kila rais aliye hai wa Marekani atoa salamu za rambi rambi
Kila rais wa zamani wa Marekani ametoa heshima zake kwa Prince Philip wa Uingereza, ambaye alifariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 99.
Rais wa sasa Joe Biden pia alitoa taarifa ambayo alimpongeza Duke wa Edinburgh kwa "maisha ya huduma kwa Uingereza". Marais 18 walichaguliwa katika maisha ya Prince Philip .
Malkia Elizabeth II amekutana na marais 12 wa Marekani wakati wa utawala wake, mara nyingi na mumewe kando yake.Joe Biden
Akiongea kutoka Ikulu ya White House, Bwana Biden alimuelezea mkuu huyo kama "mtu mashuhuri".
"Maisha yake ya huduma kwa Uingereza na Jumuiya yote ya madola ilionekana kwa kila mtu kwa muda mrefu sana," alisema.
"Nadhani atakosekana, haswa Uingereza. Umri wa miaka tisini na tisa, hakuwahi kupungua kabisa...'
Bwana Biden anaripotiwa alitarajiwa kukutana na Malkia katika Ikulu ya Buckingham mnamo Juni.
Siku ya Ijumaa, katibu wa vyombo vya habari wa Ikulu Jen Psaki alisema bado haijabainika ikiwa rais atahudhuria mazishi ya mtawala huyo.
Yeye na mkewe, Jill Biden, pia walitoa taarifa ya pamoja wakisifu "Miongo kadhaa' Philip ya kujitolea kwa utumishi wa umma.
Urithi wake "unaonekana wazi kwa sababu kampeini za mazuri ambazo aliziinua kama mlinzi, katika juhudi za mazingira alizotetea, katika wanachama wa Vikosi vya Wanajeshi ambavyo aliviunga mkono, kwa vijana aliowapa msukumo , na mengi zaidi," wawili hao waliandika.
Donald Trump
Donald Trump, ambaye alitembelea familia ya kifalme kwa mara ya mwisho mnamo 2019, alielezea Prince Philip kama "mtu aliye na roho tukufu na roho ya kifahari ya Uingereza na Jumuiya ya Madola".
Alielezea kifo cha Prince Philip kama " Msiba mkubwa usioweza kubadilishwa kwa Uingereza, na kwa wote ambao wanathamini sana ustaarabu wetu".
"Prince Philip alikuwa kifafanuzi cha heshima na neema ya Uingereza," alisema "Aliweka mfano wa hifadhi tulivu, ushupavu mkali, na uadilifu usiobadilika wa Uingereza."
Aliongeza: "Katika miaka michache iliyopita, mimi na Melania tuliheshimiwa kupata nafasi ya kutembelea Uingereza.
"Tuliona wenyewe jinsi ufalme unavyojitokeza na kutekeleza fadhila za watu wa Uingereza - na hakuna mtu aliyefanya hivyo zaidi ya Prince Philip."
Barack Obama
Barack Obama na mkewe Michelle walisema Prince Philip na Malkia walikuwa "tayari wamekaa kwenye ulingo wa ulimwengu kwa zaidi ya nusu karne" wakati wa mkutano wao wa kwanza.
"Kama Wamarekani wawili hawajazoea majumba na fahari, hatukujua nini cha kutarajia. Hatupaswi kuwa na wasiwasi," walisema.
"Malkia na Prince Philip mara moja walitufanya tukatulia kwa ukarimu waao, wakibadilisha hafla ya sherehe kuwa kitu cha asili zaidi, hata vizuri. Prince Philip haswa alikuwa mwema na mwenye ucheshi mzuri.
Obama na mkewe walisema ''watamkosa sana''
Ilikuwa ni mara ya kwanza kutambulishwa kwa mtu wa jina na taji lake na katika miaka tangia hapo tumezidi kumuenzi.
Wakati wa ziara yake mnamo 2016, Prince Philip, mwenye umri wa miaka 94 wakati huo aliwasafirisha Obama na mkewe kwa chakula cha mchana huko Windsor Castle.
George W Bush
George W Bush alisifu kujitolea kwa mtawala huyo kwa utumishi wa umma.
"Katika maisha yake yote marefu na ya kushangaza, alijitolea kwa sababu zinazostahiki na kwa wengine. Aliwakilisha Uingereza kwa heshima na alileta nguvu na msaada mkubwa kwa familia ya kifalme," alisema.
Aliongeza kuwa yeye na mkewe Laura walikuwa "na bahati ya kufurahiya haiba na utani wake, na tunajua ni kiasi gani tutamkosa'
Bill Clinton
Bill Clinton na Katibu wa zamani wa mashauri ya kigeni Hillary Clinton walisema walijiunga na watu "kutoka pande zote za ulimwengu kutoa shukrani kwa maisha yake ya utumishi".
Walikutana na Prince Philip na Malkia mara kadhaa kwa miaka, taarifa ya wanandoa hao ilisema.
"Tulifurahia kila fursa tuliyokuwa nayo ya kumtembelea kwa miaka yote na tutashukuru sana kila wakati kwa fadhili aliyotuonyesha."
Jimmy Carter
Rais wa zamani wa Marekani aliye na umri mkubwa zaidi , Jimmy Carter, alikuwa katika dhifa ya chakula na Prince Philip na Malkia mnamo 1977.
Ujumbe kutoka akaunti ya twitter ya maktaba ya rais huyo mwenye umri wa miaka 96 ulisema : "Tunasikitika kusikia kwamba Prince Philip, Duke wa Edinburgh, amefariki dunia "