Pacha wa Liverpool waliotengenashwa baada ya kuzaliwa wakumbatiana na kushikana mikono

Pacha hao wakikumbatiana baada ya kutengwa

Chanzo cha picha, PICHA YA FAMILIA

Maelezo ya picha, Pacha hao wakikumbatiana baada ya kutengwa
Iliyochapishwa

Mama yao alisema '' alilia machozi ya furaha'' wakati mapacha wake walipoungana tena wiki mbili baada ya kutenganishwa.

Laura Hough alisema kuwa alionywa kuwa binti yake , Neve, ambaye alizaliwa na uzito wa gramu 652, huenda asiishi.

Lakini ni pacha wake, kaka yake Louie, ambaye alikuwa na uzito wa mwili wa kilo moja na nusu , ambaye alipelekwa kwa daktari bingwa ambaye aliwatenganisha

Bi Hough, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Liverpool, alisema hisia za kukutanishwa tena kwa wanae zilikuwa ''nzuri sana'' walikuwa wamekumbatiana na kushikana mikono ".

"Sio wa kawaida. Ni wenye nguvu sana.

''Najivunia sana kuwa nao'', alisema.

Neve na Louie walizaliwa kwa njia ya upasuaji wa dharura walipokuwa wametimiza wiki ya 30 katika Hospitali ya Wanawake ya Liverpool tarehe 8 Machi.

Mama huyo ambaye alikuwa anajifungua kwa mara ya kwanza alisema alikuwa mwenye "uoga" kwasababu " aliambiwa wiki mbili za mwisho za uja uzito wake kwamba mwanae wa kike [Neve] huenda asiweze kuishi lakini alikuwa".

Neve alikuwa na tatizo la damu yake kutembea mwilini kwa kurudi nyuma na hakuwa anapata virutubisho vya mwili vya kutosha alipokuwa tumboni lakini licha ya kuwa ''mdogo sana'' wa mwili hakuhitaji Oksijeni, Bi Hough alisema.

"Ni wa ajabu. Madaktari walisema hawajawahi kumuona mtoto mchanga mwenye umbo dogo kama yeye ambaye hakuhitaji usaidizi ,"alisema.

Wazazi waliona furaha Chris Carey na Laura Hough wanasema wanajivumnia watoto wao

Chanzo cha picha, PICHA YA FAMILIA

Maelezo ya picha, Wazazi waliona furaha Chris Carey na Laura Hough wanasema wanajivumnia watoto wao

Hatahivyo, mapacha hao walilazimika kutunzwa katika vitengo tofauti vya huduma za watoto wachanga baada ya Louie kupata matatizo na mapafu yake kushindwa kufanya kazi.

Bi Hough alisema alikuwa na "hali nzuri zaidi kwa sasa" na pacha hao hatimaye wamekutanishwa tena Jumanne.

"Ilikuwa inatisha walipotenganishwa wakati wa kuzaliwa lakini ninilia machozi ya furahawakati walipokutanishwa tena ,"alisema.

"Walikua wamewekeana miguu na kukumbatiana, hata kushikana mikono wakati mmoja. Walikua wanapendeza sana."

Bi Houghalisema kuwa madaktari wanatumaini kuwa pacha hao wanaweza kwenda nyumbani mwezi Mei .

"Kila mtu ana hamu nao. Tunawasubiri kwa hamu kuwakaribisha nyumbani ,"alisema.