Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Msaidizi Mwandamizi afutwa kazi baada ya video za ngono bungeni kuishangaza Australia
Mgogoro ulioenea katika siasa za Australia umeendelea kuongezeka kufuatia kuibuka kwa video zinazoonyesha wafanyikazi wakifanya vitendo vya ngono bungeni, na kusababisha msaidizi mmoja mwandamizi kufutwa kazi.
Video moja ilionyesha msaidizi akifanya tendo la ngono kwenye dawati la mbunge wa kike.
Waziri Mkuu Scott Morrison alielezea video hizo kuwa "za aibu".
Hilo linajiri baada ya mfanyikazi wa zamani kufichua jinsi aliogopa kupoteza kazi kufuatia madai ya unyanyasaji wa kingono.
Brittany Higgins anadai alibakwa na mwenzake mwandamizi ofisini mnamo Machi 2019, lakini anasema alihisi kushinikizwa kutoripoti tukio hilo kwa polisi.
Ilizua wimbi la madai, na wiki iliyopita, maelfu walishiriki katika maandamano kupinga unyanyasaji wa kingono na unyanyasaji wa wanawake huko Australia.
Video hizi mpya ni zipi?
Video hizo zilitolewa kwa vyombo vya habari vya Australia na mfanyikazi wa zamani wa serikali, ambaye alisema alikuwa "amepata kinga " kwa picha hizo kwa sababu ya picha nyingi alizopokea.
Pamoja na video - zilizochukuliwa miaka miwili iliyopita - alisema watu walikuwa wakitumia chumba cha maombi kufanya ngono na hata walileta makahaba bungeni.
Mfichuzi huyo alieleza kwamba "utamaduni wa wanaume kufikiria kuwa wanaweza kufanya chochote watakacho", akielezea kwamba kuna 'wenzake wasiokuwa kabisa na madili'
Je watu wameuchukulia vipi ufichuzi huu?
Bwana Morrison aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba alikuwa "ameshtuka", na kuongeza: "Lazima tuinyooshe nyumba hii. Lazima tuweke siasa kando juu ya mambo haya, na lazima tutambue shida hii na ni lazima tuirekebishe."
Hapo awali alikuwa amekosolewa kwa namna alivyoshughulikia sakata hiyo pamoja na kukataa kukutana na viongozi wa waandamanaji wiki iliyopita.
Alikuwa amewaalika viongozi wa waandamanaji kukutana naye bungeni lakini walikataa ofa hiyo wakisema hawatakutana "faraghani".
Maswali juu ya jinsi serikali inavyoshughulikia mgogoro huo yalizungumzwa tena baada ya mbunge wa upinzani Michelle Landry kusema "alimhurumia' msaidizi aliyefukuzwa kazi.
Lakini waziri Karen Andrews aliwaambia waandishi wa habari kwamba "hilo halitaniruhusu kunyamaza' kuhusu unyanyasaji wa kijinsia katika siasa za Australia, akisema kwota za idadi ya kijinsia kwa wawakilishi wa kisiasa unapaswa kuzingatiwa - jambo ambalo Bwana Morrison ameashiria kwamba hatoliunga mkono.
"Tulijaribu kwa njia nyingine na haitupatii matokeo kwa hivyo ningependa kuona tunafanya vizuri ka njia mbadala ," aliwaambia waandishi wa habari.
Chama cha upinzani cha Labor tayari kina kwota hizo za uakilishi.
Je madai ni yepi?
Kumekuwa na madai ya uonevu na unyanyasaji kwa muda mrefu katika siasa za Australia. Walakini, madai ya Bi. Higgins yametoa mwanga juu ya unyanyasaji wa kijinsia nchini humo.
Siku chache baada ya kutoa ufichuzi wake na kusimulia masaibu yake hadharani madai zaidi yalizuka - na Mwanasheria Mkuu Christian Porter akafichua kwamba alikuwa mtuhumiwa wa madai ya ubakaji mwaka wa 1988.
Anakanusha madai hayo, na polisi walifunga uchunguzi kwasababu ya ukosefu wa ushahidi.
Bosi wa zamani wa Bi. Higgins, Waziri wa Ulinzi Linda Reynolds, pia alilazimika kuomba msamaha na kulipa fidia kwa msaidizi wake wa zamani, baada ya kumwita "ng'ombe mwongo".
Wakosoaji wanasema serikali pia imekuwa ikijikokota sana na haina ufanisi katika kushughulikia shutuma kwamba pana taasubi za kiume na ubaguzi kwa msingi wa jinsia katika utamaduni wa bunge - shida wanayosema imekithiri katika vyama vyote vya kisiasa.
Chama cha Upinzani cha Labor kimesema kitatathmini tena mitindo yake baada ya kutokea kwa madai kadhaa kutoka kwa watu ambao hawakutaka kutajwa wakidai kudhulumiwa kimapenzi na baadhi ya wanachama wa kiume wa chama hicho.