Nigeria: Watu saba wafariki baada ya ndege ya jeshi kupata ajali karibu na uwanja wa ndege wa Abuja

People and rescuers gather at the site where a Nigerian air force plane crashed while approaching the Abuja airport runway, according to the aviation minister, in Abuja, Nigeria February 21, 2021.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watu walikusanyika katika eneo la ajali Jumapili asubuhi
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Watu saba wamefariki baada ya ndege ya jeshi la Nigeria kuanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege, katika mji mkuu wa Abuja, asubuhi ya Jumapili, kwa mujibu wa maafisa.

Ndege hiyo ya jeshi la anga la Nigeria iliripoti kukumbwa na hitilafu katika injini yake, msemaji wa Air Vice Marshal Ibikunle Daramola, aliandika katika Twitter yake.

Aliongeza kuwa ndege hiyo ilikuwa njiani kuelekea Minna, kaskazini mwa jimbo la Niger.

Mkuu wa wafanyakazi wa shirika la ndege hiyo ameagiza uchunguzi kufanywa mara moja.

Katika msururu wa ujumbe wa Twitter, vikosi vya angani vimetoa wito kwa watu "kuwa watulivu na kusubiri matokeo ya uchunguzi".

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

1px transparent line
Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

1px transparent line

Msemaji wa jeshi la anga la Nigeria amesema abiria wote wamefariki.

Walioshuhudia ajali hiyo waliripoti kuona ndege ikizunguka katika eneo ilipotokea ajali kabla ya kuanguka na kushika moto karibu na barabara ya ndege ya uwanja huo. Wanasema walisikia mlio mkubwa kabla ya ndege hiyo kulipuka na kushika moto.

Mashuhuda mwingine ameiambia shirika la habari la Reuters kwamba harufu ya ndege iliyochomeka na kemikali ilisheheni sehemu ilipotokea ajali hiyo, nje kidogo ya au la uwanja wa ndege.