Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mlolongo wa matukio toka kulazwa mpaka kufariki kwa Maalim Seif
Januari 30, Chama cha ACT-Wazalendo kilitoa taarifa kwa umma kuwa Mwenyekiti wao na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amelazwa baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Hakuna taarifa rasmi kutoka serikalini iliyofuata juu ya kuugua na kula sea kwa Maalim Seif.
Januari 31, Maalim Sief anatuma ujumbe wake wa mwisho kwa Umma kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, akithibitisha kulazwa kwake na kusema anaendelea vyema.
Ukimya unatawala baada ya hapo, hakuna taarifa iliyofuata kutoka ACT wala serikalini juu ya hali ya Maalim.
Februari 9, Maalim Seif anahamishwa kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya hali yake kutetereka.
Hakuna taarifa rasmi kwa Umma juu ya kinachoendelea.
Ni maafisa wachache wa serikali na ACT ambao wanajua kinachoendelea.
Februari 12, Watu wa karibu wa Maalim waeleza kuwa hali yake iliimarika na kukata na matumaini ya kupona.
Februari 16, Tetesi zatanda mitandaoni nchini Tanzania kuwa Maalim Seif amefariki dunia.
Taarifa hizo hata hivyo zilikanushwa na mitandao ya kijamii ya ACT.
Februari 17, Maalim Seif afariki dunia takriban wiki tatu toka iliporitiwa kuambukizwa corona. Hata hivyo taarifa rasmi juu ya sababu ya kifo chake hazijatolewa.