Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bodi ya makaburi ya wazungu yaomba msamaha kwa kuzuia mtu mweusi kuzikwa kwenye makaburi yao
Bodi ya makaburi ya Louisiana, nchini Marekani yameomba msamaha baada ya kukataa kumzika afisa wa polisi mweusi wa eneo hilo kwasababu ya miongozo ambayo imekuwa ikifuatwa kwa miongo kadhaa inayosema wazungu pekee ndio wanaoruhusiwa kuzikwa eneo hilo.
Bodi inayosimamia eneo hilo la makaburi ya Oaklin Springs ilikutana wiki hii kubadilisha mkataba wake kufuatia hasira ya raia juu ya sheria yao inayosema "wazungu pekee ndiyo watakaozikwa katika eneo hilo".
Mjane wa afisa huyo alisema tukio la mume wake Darrell Semien kunyimwa sehemu ya kuzikwa eti kwasababu ni mweusi ni "fedheha".
Mwenyekiti wa bodi hiyo alisema kuwa hawakuwa na ufahamu wa sera hiyo ya kikatili.
Kipi kilichotokea?
Semien, 55 alikuwa naibu wa kaunti katika eneo la Oberlin, mji ambao uko maili 200 magharibi mwa New Orleans. Afisa huyo aliaga dunia wiki iliyopita kwa ugonjwa wa saratani.
Mke wake Karla Semien, na watoto wake walijaribu kununua kipande cha ardhi katika makaburi hayo ya Oaklin Springs, ambapo mfanyakazi mmoja aliwaambia kwamba eneo hilo la makaburi ni kwa ajili ya wazungu pekee.
"Nina hata ushahidi kwenye faili unaoonesha kuwa wazungu pekee ndio wanaoruhusiwa kuzikwa katika eneo hili," Bi. Semien aliandika kwenye mtandao wa Facebook siku ya Jumanne, na kuongeza kuwa hakuamini kwamba matukio kama haya bado yanaweza kutokea hata mwaka 2021.
"Ilikuwa fedheha sana, na aibu," Semien alisema akizungumza na shirika la habari la CBS News, mshirika wa BBC nchini Marekani.
"Ilikuwa ukosefu wa utu kwake kwamba hatuwezi kumzika eneo hilo kwasababu yeye ni mtu mweusi."
Ni sheria mbaya na ya kipuuzi
Mwenyekiti wa bodi ya makaburi, H. Creig Vizena, amesema sheria hiyo ya zamani ilikuwa "mbaya sana na ya kipuuzi" na kuwaambia waandishi wa habari wa Marekani kuwa yeye au wajumbe wengine wa bodi walikuwa wanalifahamu hilo.
Alitoa rai kwa wanaosimamia makaburi mengine kusini mwa Marekani kuangalia tena sheria hiyo yenye ubaguzi uliopitiliza.
Wafanyakazi wa makaburi hayo wamekanusha kukataa kumpa nafasi shangazi yake mwenyekiti huyo, " gazeti la eneo hilo, Vizena liliandika kwa mujibu wa katiba.
Miongo ya haki za raia
Matukio ya namna hiyo yanatokea hata baada ya zaidi ya miaka 50 tangu sheria ya haki za raia kupitishwa.
Sheria hiyo ilipitishwa mwaka 1964, ikiwa inapiga marufuku ubaguzi katika mazishi na kusisitiza majimbo yote ya kusini kufuta sera hizo zinazohamasisha ubaguzi.
Polisi aliyefariki alikuwa anafanya kazi katika kituo cha polisi cha eneo hilo kwa zaidi ya miaka 15 kwa mujibu wa wosia uliosomwa.
Alikuwa analelewa na mlezi aliyekuwa anawalea watoto 72 kwa kipindi cha miaka 16 iliyopita.
Familia ilikataa ofa waliyopewa kutoka Vizena, kutumia mita 8,000-ya eneo la makaburi hayo kwa matumizi yao binafsi, na kusema ni bora wampumzishe mpendwa wao katika eneo jingine mbali na makazi yao.