Virusi vya corona : Ladha na harufu ya kuchukiza vinavyowakera baadhi ya watu waliopatwa na corona

Clare Freer, when eating out was a pleasure

Chanzo cha picha, Clare Freer

Maelezo ya picha, Clare Freer, wakati alipokua bado akifurahia chakula na mvinyo kabla ya kuugua Covid-19
Iliyochapishwa

Wtu wengi wenye virusi vya Covid-19 hupoteza kwa muda ladha ya vitu na harufu, wakati wanapokuwa wakipona , mara nyingi hisia hiyo hurejea- lakini baadhi wanahisi kuwa vitu vinakuwa na harufu tofauti kabisa, na vitu ambavyo vingepaswa kuwa na harufu nzuri, kama vile chakula, sabuni, na wapenzi wao, hugeuka na kuwa na harufu mbaya. Idadi ya watu wanaopatwa na hali hii inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama parosmia, inaendelea kuongezeka, lakini wanasayansi wanasema hawana uhakika ni kwanini hali hii inatokea, au ni kwa jinsi gani wanaweza kuwatibu wenye tatizo hili.

Clare Freer ni mmoja wao. Amekuwa akilia kwa huzuni kila mara anapojaribu kuipigia chakula familia yake ya watu wanne.

"Harufu ya chakula hunifanya nihisi kizunguzungu . Ninapopika huwa nahisi harufu ya uozo imejaa ndani ya nyumba mara tu chakula kinapoanza kuiva kwenye jiko au kwenye oveni na hua siwezi kuvumilia ,"anasema.

Clare mwenye umri wa miaka 47-kutoka Sutton Coldfield nchini Uingereza ameishi na hali ya kuhisi chakula kinanuka kama uozo kwa miezi saba sasa na wengi waliopatwa na corona wanahisi harufu mbaya ya kunuka kila siku.

Vitunguu, kahawa, nyama, matunda, pombe, dawa ya mswaki, bidhaa za usafi na pafume vyote vinamfanya ajihisi kutapika. Maji pia yana athari sawa, jambo linalomfanya ashindwe hata kufua nguo.

"Siwezi hata kumbusu mume wangu tena ananuka vibaya ," anasema Clare.

Clare alipatwa na virusi vya corona mwezi machi mwaka jana na, kama ilivyokuwa kwa watu wengi, alipoteza uwezo wa kutambua harufu kutokana na ugonjwa huu. Uwezo huu ulirejea kwa kipindi kifupi mwezi Mei, lakini kufikia mwezi Juni Claire alianza kuchukia vyakula alivyovipenda zaidi, kwasababu vilikuwa na harufu mbayana kila mara chakula kilipopikwa alihisi kana kwamba kitu cha kemikali yenye harufu kali au kitu fulani kimeungua.

Tangu katikati ya mwaka janaamekuwa akila mkate na jibini kwasababu hivyo ndivyo ninavyoweza kuvivumilia . "Sina nguvuna huhisi maumivu kila sehemu ya mwili ," anasema. Pia imemuathiri kisaikolojia na kimawazo ; anaseam hulia mara nyingi.

"Licha ya kwamba amekuwa akihisi harufu mbaya kila mara , Clare anasema: Niliweza kuendelea na maisha kama kawaida na kula na kunywa ,"

Clare enjoying a pamper day with her eldest daughter - perfume now smells revolting to her

Chanzo cha picha, Clare Freer

Maelezo ya picha, Clare akiwa pamoja na binti yake-lakini sasa anahisi pafumu inanuka

Daktari wa Clare anasema hajawahi kupata mgonjwa mwingine mwenye tatizo kama la Clare. Akiwa mwenye wasi wasi mkubwa kuhusina na hali yake, Clare aliingia kwenye mitandao kutafuta majibu na akapata kikundi cha Facebook chenye wajumbe 6,000 kilichoanzishwa na shirika la watu waliopoteza uwezo wa kuhisi harufu , kwa jina AbScent.

Karibu wajumbe wote wa kikundi hicho walianza kupoteza uwezo wa kuhisi harufu kutokana na Covid-19, na baada ya hapo waendelea kuishi na hali hii.

"Harufu ambazo hujitokeza miongoni mwa watu waliopoteza uwezo wa kuhisi harufu ni pamoja: mizoga, uozo, nyama iliyooza, na kinyesi ," anasema muasisi wa shirika la AbScent-Chrissi Kelly, ambaye alianzisha kikundi cha Facebookmwezi Juni baada ya kile alichokielezea kama "mawimbi " ya visa vya Covid-19 ya kupoteza uwezo wa utambuzi wa harufu. Mara nyingi watu wenye hali hii huhangaika kuelezea harufu wanayoihisi kwasababu mara nyingi huwa hawajawahi kuhisi harufu kama hiyo kabla, na kuamua kutumia maneno ambayo yanawasilisha vitu vinavyochukiza.

takriban 65% ya watu wenye virusi vya corona hupoteza hisia za harufu na inakadiriwa kuwa takriban 10% yao huugua hali ya kubadilika kwa harufu za vitu mbalimbali, pale unapohisi kitu ambacho hakipo karibu nawe.

Huku Clare Freer akizikumbuka na kuzitamani siku ambazo alipenda harufu ya mume wake alipokuwa akitoka bafuni kuoga, ustin Hyde mwenye umri wa miaka 41 kutoka eneo la Cheltenham hajawahi kuhisi harufu ya mtoto wake mchanga wa kike aliyezaliwa Machi 2020.

Justin Hyde

Chanzo cha picha, Justin Hyde

Maelezo ya picha, Justin sasa hawezi kufurahia kutembelea baa kama mwanzoni kwasababu hawezi kuhisi harufu ya pombe yoyote

Ilianza kurejea kidogo mwezi Julai, lakini kahawa nikaanza kuhisi kahawa inanuka harufu ya ajabu-na haraka mambo yakawa mabaya zaidi.

"Takriban harufu zote za vitu zilianza kunuka kiajabu ," anasema . "Mayai vinza kwa kawaida hunikera sana na hilo linanifanya nisifurahie bia yangu au mvinyo kwasababu kwa sasa zina ladha ambayo ninaiita ladha ya Covid ."

Amegundua kuwa chakula kisicho na nyama, ikiwa ni pamoja na mboga zilizopikwa kwa binzali zinakuwa walau na ladha kidogo, lakini hawezi tena kwenda baa, wala kula mayai au viazi vya kukaangwa.

"Anasa zote hizo tunazoziona kama kitu ch kawaida zimepotea tangu nilipopata Covid," anasema . "Nijihisi kuvunjika moyo na kama kama sio mimi ."

Ushauri kuhusu jinsi ya kukabiliana na hali ya kukosa uwezo wa kutambua ladha na harufu:

  • Kula vyakula vya uvuguvugu au baridi
  • Epuka vyakula vya kukaangwa, nyama za kuchoma, vitunguu, mayai, vitunguu saumu na chokoleti ,
  • Jaribu vyakula kama wali, noodles, mkate ambao haujachomwa, mboga zilizopikwa kwa mvuke na maziwa chachu( mtindi) au yogati

Chanzo: AbScent

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?