Virusi vya corona: 'Waliopata chanjo bado wanaweza kusambaza corona' Uingereza

Iliyochapishwa

Watu waliopata chanjo bado wanaweza kuambukiza wengine virusi vya corona na hivyo basi, wameombwa kuendelea kutekeleza hatua za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo, naibu wa afisa mkuu wa matibabu Uingereza amesema.

Akizungumza na gazeti la Sunday Telegraph, Profesa Jonathan Van-Tam amesisitiza kuwa wanasayansi "bado hawajui athari ya chanjo katika usambaaji wa ugonjwa huo".

Ameongeza kuwa chanjo inatoa matumaini lakini kiwango cha maambukizi ni lazima kipungue na hakuna njia mbili.

Uingereza imesema asilimia 75 ya watu wenye umri zaidi ya 80 wamepata chanjo hiyo.

Aina zote za chanjo zinazotumika ya Pfizer-BioNTech na ya AstraZeneca kutoka Oxford inatakikana angalau mtu apate dozi mbili na sasa hivi wanaofuatiliwa hali zao ni wale waliopata dozi ya kwanza.

Profesa Van-Tam amesema "hakuna chanjo ambayo imewahi kufanya kazi kwa asilimia 100, kwahiyo hakuna uhakika wa kwamba chanjo zinazotumika zina kinga thabiti.

Inawezekana ukapata maambukizi ya virusi vya corona katika kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya kupata chanjo, na ni vizuri kujipatia wiki kama mbili ili kinga ijiimarishe kabisa hasa kwa watu wazima.

"Hata ukishapata dozi zote za chanjo, bado unaweza kupata maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa mtu mwingine na mzunguko huo ukaendelea," Profesa Van-Tam amesema.

"Ikiwa watu wataacha kufuata kanuni ziizowekwa bado tu mutasambaza virusi hivyo na kuweka wengine ambao pia wanahitaji chanjo katika hatari ambao wako mbali kufikiwa."

Madaktari waandamizi wametoa wito kwa maafisa wa afya Uingereza kupunguza muda wa kusubiri hadi chanjo ya pili ya Pfizer-BioNTech

Je virusi hivi vipya ni vipi?

Wasiwasi wa wataalamu sasa hivi umejikita katika aina chache ya virusi vipya vya maambukizi ya corona:

  • Virusi vya Uingereza vimeenea sana Uingereza na kusambaa kwa zaidi ya nchi zingine 50.
  • Virusi vya Afrika Kusini ambavyo pia vimepatikana katika nchi zisizopungua 20 ikiwemo Uingereza.
  • Virusi vya Brazil.

Sio ajabu kwamba kumejitokeza virusi vipya kwasababu virusi vyote hujibadilisha wakati vinaendelea kuzaliana ili kusambaa na kuendeleza uwepo wao zaidi

Sasa hivi kuna maelfu ya virusi vipya vya corona vinavyosambaa.

Je virusi hivyo ni hatari kiasi gani?

Inashukiwa kuwa virusi vya Uingereza, Afrika Kusini na Brazil huenda ndio vinavyoambukiza zaidi au vilivyorahisi mtu kuvipata kuliko vile vya awali.

Vitusi vyote hivyo protini yake imebadilika- ikiwa ni sehemu ya virusi yenye kuhusishwa na seli za binadamu.

Matokeo yake, virusi hivyo vinaonekana kuwa na uwezo wa juu wa kuambukiza seli na kusambaa.