Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Aditya Singh: Mwanaume apatikana 'akiishi katika uwanja wa ndege' kwa kuhofia corona
Mwanaume aliyekuwa na hofu kubwa ya kusafiri kwa ndege kutokana na janga la virusi vya corona aliishi bila kugundulika katika eneo salama katika uwanja wa kimataifa wa Chicago' kwa miezi mitatu, wamesema waendesha mashitaka nchini Marekani.
Aditya Singh, mwenye umri wa miaka 36, alikamatwa Jumapili baada ya mfanyakazi mmoja wa ndege kumtaka atoe kitambulisho chake.
Alimuonesha kitambulisho cha kazi (badge) ambayo inadaiwa kuwa kilikuwa ni cha meneja mmoja katika uwanja huo ambaye aliripotiwa kuwa kitambulisho chake kilipote.
Polisi wanasema Bw Singh aliwasili kutoka Los Angeles na kufika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa O'Hare tarehe 19 Oktoba mwaja jana.
Anaripotiwa kupatikana na kitambulisho cha muhudumu (badge) katika uwanja wa ndege na alikuwa "anaogopa kwenda nyumbani kwasababu ya Covid", alisema naibu Mwanasheria mkuu wa jimbo Kathleen Hagerty, katika jarida la Chicago Trubune.
Aliweza kuishi kwa msaada aliopewa na wasafiri wengine, alimwambia hakimu katika kesi dhidi yake.
Jaji wa kaunti Susana Ortiz alieleza kushangwazwa sana na tukio hilo.
"Kwa hiyo, kama ninakuelewa vizuri, ni kwamba unaniambia kuwa mtu ambaye haruhusiwi, ambaye sio muajiriwa anadaiwa kuishi katika eneo salama la uwanja wa ndege wa kimataifa wa O'Hare kuanzia tarehe 19 Oktoba, 2020 hadi tarehe 16 Januari 2021, na hakugundulika?
Ninataka kukuelewa kwa usahihi," alimwambia mwendesha mashitaka ambaye alikuwa akiainisha mashitaka Jumapili.
Bw Singh anaishi katika kitongoji cha Los Angeles na hana historia ya uhalifu , kwa mujibu wa wakili wa umma Courtney Smallwood. Haifahamiki ni kwanini alikuwa Chicago.
Ameshitakiwa kwa uhalifu kwa kuingia eneo linalodhibitiwa la uwanja wa ndege bila idhini na wizi wa upotoshaji . Amezuiwa kuingia katika uwanja wa ndege kama ataweza kulipa dhamana ya dola 1000.
"Mahakama imebaini jambo hili kuwa la kuogofya kwa kipindi ambacho inadaiwa aliishi " Judge Ortiz alisema
"Kwa misingi kuwa uwanja wa ndege unapaswa kuwa sehemu salama kabisa ili watu wahisi kuwa salama wanaposafiri, sidhani hatua hizo zinazodaiwa zinamfanya kuwa hatari katika jamii ."
Idara ya safari za anga ya Chicago , inayosimamia viwanja vya ndege vya jiji hilo, imesema katika taraifa yake kuwa: "Huku suala hili likiwa bado linachunguzwa, tumeweza kubaini kwamba mwanaume huyo hakuwa mtu wa hatari kwa usalama wa uwanja wa ndege au umma wa wasafiri ."