Fatemeh Khishvand: Watumiaji mtandao wa Instagram wanaoikera serikali ya Iran

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kwamba mtumiaji wa mtandao wa INstagram Fatemeh Khishvand ametumika kama mfano na utawala wa Iran.

Chanzo cha picha, InStagram

Maelezo ya picha, Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kwamba mtumiaji wa mtandao wa INstagram Fatemeh Khishvand ametumika kama mfano na utawala wa Iran.
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Alipokuwa akikuwa nchini Iran Fatemeh Khishvand alikua na ndoto ya kuwa mtu maarufu , akichapisha picha aina ya selfi katika mtandao wa Instagram kwa lengo la kutaka kuonekana.

Picha zake hatahivyo zilikuwa picha za kupotosha zenye sura ilioharibika .

Akitumia jina lisilo lake la Sahar Tabar, picha hizo zilivutia sana vyombo vya habari vya kimataifa zilipoonekana kwa mara ya kwanza 2017.

Katika baadhi yazo , bi Khishvand alifanana na muigizaji wa Marekani Angelina Jolie.

Hatua hii ilisababisha uvumi kwamba kijana huyo alikua amefanyiwa upasuaji wa mapambo mara 50 ili kufanana na nyota huyo wa Hollywood, lakini kama alivyoelezea , alivutiwa na muigizaji wa filamu ya Corpse Bride kutoka kwa utunzi wa kitabu cha Tim Burton.

Muda mfupi alikuwa tayari amewavutia zaidi ya wafuasi 500,000 katika mtandao wake wa Instagram , akijipatia umaarufu ambao amekuwa akiutafuta miaka yote.

Lakini umaarufu huo ulimuweka mashakani.

Nchini Iran , ni hatari kuchapisha katika mitandao ya kijamii.

Utawala wa taifa hilo wa madhehebu ya Shia huweka sheria kali kuhusu kile ambacho kinaweza kuchapishwa na kile ambacho hakiwezi.

Kwao picha za bi Khishvand zilionekana kama uhalifu na sio picha za msichana aliye mwerevu.

Hivyobasi mwezi Oktoba 2019, picha hizo zilionekana kama uhalifu na bi Khishvand alikamatwa na kushtakiwa na makosa kadhaa ikiwemo kukufuru , kuchochea ghasia kutusi vazi la kiislamu na kuchochea ufisadi miongoni mwa vijana.

Akaunti yake ya Instagram ilifutilia mbali na kwa zaidi ya mwaka mmoja alitumikia kifungo jela bila dhamana.

Baadaye mahakama ya mapinduzi inayosifika kwa usiri na maamuzi yake yanayoshinikizwa kisiasa dhidi ya wapinzani - ilitoa hukumu ya miaka 10 gerezani mwezi Disemba mwaka uliopita.

Bi Khishvand alivutia wafuasi baada ya kujifannaisha na jitu linalofanana na muigizaji wa marekani Angelina Jolie

Chanzo cha picha, Instagram

Maelezo ya picha, Bi Khishvand alivutia wafuasi baada ya kujifannaisha na jitu linalofanana na muigizaji wa marekani Angelina Jolie

''Hukumu hiyo kali ilivutia shutuma kali. Taifa la Iran lina historia ya kuwakamata wanawake kwa kucheza densi , kuimba, kwa kuvua vazi lake , kwa kuingia uwanjani, kwa uanamitindo , lakini wakati huo kwa kutumia picha bandia'', Masih Alinejad mwandishi maarufu nchini Iran na mwanaharakati alisema katika video ya mtandao wa twitter.

Kama bi Alinejad alivyopendekeza, kesi ya bi Khishvand inaonekana kuwa njia mpya ya ukandamizaji wa Iran kuhusu watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Data ya uhalifu unaotokana na mitandao nchini Iran haijulikani lakini kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la haki za binadamu nchini Iran, takriban watu 332 wamekamatwa kwa vitendo vyao katika intaneti tangu Disemba 2016.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kati yao 109 walikuwa wakitumia mtandao wa Instagram, lilisema kundi hilo.

"Pia kumekuwa ni mawimbi ya washawishi wa Instagram ambao huitwa kwa mahojiano na serikali ya Iran mara kwa mara.

Mojawapo ni raia sita wa Iran ambao 2014 , walichapwa viboko na hukumu yao ya kifungo jela kufutwa kwa muda kwa kuonekana katika kanda ya video wakicheza densi ya wimbo wa Pharrell William kwa jina Happy.

Kundi jingine lilikuwa 2018, wakati kijana mmoja mjenga misuli alikamatwa kwa kuchapisha kanda ya video iliomuonesha akidensi wimbo wa muziki wa Pop .

Seyed Ahmad Moinshirazi, 42, anasema kwamba yeye na mkewe Shabnam Shahrokhi, 38, wamezoea ukandamizaji wa utawala wa Iran.

Shabnam Shahrokhi na Seyed Ahmad Moinshiraz

Chanzo cha picha, @PICASSOMO ON INSTAGRAM

Maelezo ya picha, Shabnam Shahrokhi na Seyed Ahmad Moinshiraz

Walikuwa watu wenye ushawishi mkubwa katika mtandao wa Instagram

Bwana Moinshirazi alisema kwamba 2018 alikabiliwa na kampeni ya vitisho kutoka kwa maafisa wa mtandaoni , ambacho kilimuita ili kumuhoji na kutaka ushirikiano wake.

Wakati wa mahojiano yaliochukua takriban saa moja , bi Moinshirazi alisema kwamba alitishiwa mara kwa mara na mashtaka ya upelelezi na kutakiwa kuondoa baadhi ya machapisho yake katika mtandao huo kwa mfano yale yaliomuonesha mkewe bila kitambaa cha kufunika kichwa kwa jina hijab.

''Walisema kwamba machapisho kama hayo yalikuwa yakiharibu utamaduni wa Iran na kuvutia ule wa mataifa ya magharibi'' , alisema bwana Moinshirazi, mpiganaji wa masumbwi na mateke{ kickboxer} aliyestaafu kwa jina maarufu Picasso Moin akizungumza na BBC.

Machapisho hayo yaliondolewa kama ilivyohitajika , lakini unyanyasaji ukaendelea hatua iliosababisha kukamatwa kwa wanandoa hao na kuachiliwa kwa dhamana ya $200,000 mwaka 2019.

''Waendesha mashtaka walikasirika'' , alisema bwana Moinshirazi .

Wanandoa hao wamekuwa wakisambaza kanda za video za wawili hao wakifanya mazoezi

Chanzo cha picha, @PICASSOMO ON INSTAGRAM

Ndio maana wanandoa hao walipewa hukumu yao licha ya kutokuwepo mahakamani wakifungwa miaka 16 ,viboko 74 au walipe faini kati ya adhabu hizo mbili.

Kwa sasa hatahivyo bi Khishvand ameonewa huruma .

Mwisho wa mwezi Disemba 2020, aliachiliwa kwa dhamana huku akikata rufaa kuhusu hukumu yake ya kwenda jela.