Matokeo ya uchaguzi Uganda 2021: Rais Museveni akabiliwa na upinzani kutoka kwa Bobi Wine

Iliyochapishwa

Raia wa Uganda hii leo wanashiriki katika shughuli ya kihistoria ya kumchagua rais na wawakilishi wa bunge lao .

BBCSwahili itaendelea kukupatia matangazo mubashara ya matokeo hayo kuanzia jioni hii leo punde tu shughuli ya kupiga kura itakapokamilika.

Matokeo ya maeneo bunge yataanza kutangazwa muda tu baada ya shughuli ya upigaji kura kukamilika huku yale ya urais yakitarajiwa siku chache zijazo.

Cha msingi katika uchaguzi huu

  • Takriban raia milioni 18.1 wanashiriki katika uchaguzi huu ikiwemo wagombea 11 wanaowania urais.
  • Mmoja kati ya wagombea hao ni mwanamke kwa Jina Nancy Kalembe .
  • Rais Yoweri Museveni amehudumu kwa kipindi cha mihula mitano
  • Asilimia 50 na kura moja zitahitajika kwa mgombea kuzuia kuingia katika raundi ya pili.
  • Wabunge 529 pia watachaguliwa katika uchaguzi huo.
  • Ni haki ya kikatiba kwa mtu yeyote kupinga matokeo ya uchaguzi Uganda

Wakati huohuo Shughuli ya kupiga kura ilianza mwendo wa saa moja alfajiri licha ya kwamba baadhi ya maeneo yalikuwa hayajapata vifaa vya kupigia kura.

Hatua hiyo inajiri baada ya Intaneti kuminywa saa chache kabla ya uchaguzi huo kuanza.

Bobi Wine ndiye wa kwanza kuthibitishwa kupiga kura katika eneo la Freedom Square.

Mapema leo Milolongo mirefu ilishuhudiwa katika vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini Uganda.

Raia waliokuwa na hamu ya kupiga kura walifika katika vituo hivyo mapema zaidi kabla ya vituo hivyo kufunguliwa huku wakionekana kutaka kushiriki katika shughuli hiyo ya kihistoria.