Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Uganda 2021: Marekani ina wasiwasi na hatua ya Uganda 'kuminya uhuru'
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umeeleza mashaka yake juu ya kuminywa kwa uhuru wa kijamii nchini humo ikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la nchini humo Daily Monitor, limeandika kwa mujibu wa Balozi wa Marekani nchini Uganda Natalie E. Brown, Marekani ina wasiwasi na masharti yanayowekewa mashirika ya kiraia (CSOs), Tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa vibali kwa waangalizi wa uchaguzi wa ndani na muingilio wa programu ya kuelimisha wapiga kura inayoendeshwa na mashirika ya wasiopendelea yoyote katika uchaguzi ambayo yanafadhiliwa na washirika wa kimataifa wanaopendelea demokrasia Uganda, ambao wamekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya utayari wa Uganda katika utekelezaji wa uchaguzi wenye uwazi na unaojumuisha kila mmoja.
Bi. Brown ameishutumu mamlaka za Uganda kuendelea kufungia akaunti za benki za mashirika ya kiraia kwa misingi yenye kutiliwa mashaka, kuzuia kazi yao muhimu ya kuelimisha wapiga kura, kuzuia waangalizi wa uchaguzi wa ndani, mabaraza ya hadhara pamoja na kufuatilia na kuzuia ghasia zenye kuhusishwa na uchaguzi.
"Bado tuna wasiwasi hasa juu ya vile taasisi za Uganda zinaendelea kufungia shughuli za mashirika ya kidunia yasiopendelea upande wowote kwenye uchaguzi ambao unaofadhiliwa na Marekani, Umoja wa Ulaya na washirika wengine wa kimataifa ambao walikuwa wanasaidia raia wa Uganda kufikia viwango vyao vya uchaguzi inavyohitajika kikatiba,"amesema.
Bi. Brown pia alizungumzia uhusiano wa kidemokrasia na dipilomasia kati ya Marekani na utaratibu wa kupiga kura ambao umekuwepo kwa miaka 60.
"Tuko pamoja na raia wote wa Uganda wanaotaka kuwa na demokrasia na kuendeleza ustawi kwa wote," amesema.
Marekani, ameongeza, "imesihi mamlaka husika kuhakikisha kuwa mchakato huo wa uadilifu unakamilishwa ili mashirika haya, ambayo yanasaidia raia wa Uganda kuwa karibu na kufurahia uchaguzi huru, wa usawa na wenye uwazi kuendelea na kazi yao. Demokrasia haiwezi kuchukuliwa hivi hivi."
"Kama marafiki na washirika wa muda mrefu, tuna wasiwasi na jinsi inavyofunga ushirikiano wake ikiwemo kuzuia akaunti za benki za mashairika ya kiraia nchini Uganda ambayo inaendesha kazi zake kwa manufaa ya raia wa Uganda," Bi. Brown ameongeza.
Marekani, inachukuliwa kuwa moja wa nchi zenye demokrasia duniani ilipitia mtihani mgumu Januari 6, baada ya wafuasi wa wanaompendelea Trump kukiuka sheria za usalama zilizopo na kuvamia bunge wakati linaendelea na kikao cha kuidhinisha ushindi wa rais mteule Joe Biden.
Chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) kimekuwa kikifanya kampeni kabla ya uchaguzi kikidai kuwa raia wa kigeni wamekuwa wakiunga mkono upinzani nchini humo.
Waziri anayesimamia kazi kwa ujumla, Bi. Mary Karooro Okurut Jumamosi alisema, "Wamarekani wasije hapa na kujaribu kutufunza kuhusu demokrasia. Wamarekani hawawezi kuja hapa na kutuvurugia amani yetu," akirejejelea uvamizi wa bunge ulitokea.
Wakati huohuo, taarifa ya Bi.Brown inawadia baada ya kukisiwa kuwa huenda mawasiliano yakakatizwa kama ilivyokuwa mwaka 2016 kipindi cha uchaguzi.