Uchaguzi Uganda 2021 : Idadi ya waliopoteza maisha yafikia 38

Iliyochapishwa

Watu 28 wamekufa wamepoteza maisha nchini Uganda wakati wa maandamano, na zaidi ya watu 500 wamekamatwa, kwa mujibu wa polisi.

Wagombea kadhaa wa urais wamesitisha kampeni zao, wakitaka Bobi Wine aachiwe huru

Bobi Wine, jina lake halisi Robert Kyagulanyi, alikamatwa siku ya Jumatano kwa kukiuka masharti ya Covid, polisi walisema.

Mgombea huyo, 38 ameshutumiwa kukusanya makundi makubwa ya watu wakati wa kampeni Mashariki mwa nchi hiyo

Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wagombea 11 wanaopambana na Rais Yoweri Museveni , ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Uchaguzi utafanyika tarehe 14 mwezi Januari mwakani.

Katika siku ya pili ya maandamano nchini humo, maafisa usalama walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za moto kuwatawanya watu jijini Kampala nchini humo.

Waandamanaji wamekuwa wakichoma magurudumu na takataka na kufunga barabara jijini Kampala. Biashara zimefungwa na askari wengi wameonekana barabarani

Akaunti ya Twitter ya Bobi Wine imeonesha watu wasio na sare wakipitapita mjini, wakifyatu risasi hewani.

Mshtuko na ghadhabu dhidi ya polisi

Na Patience Atuhaire, Kampala

Hizi ni vurugu mbaya kuwahi kutokea mitaani nchini Uganda tangu Bobi Wine alipochaguliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais.

Alhamisi asubuhi , BBC ilishuhudia maafisa wa usalama wakiingia kwenye maduka makubwa katikati ya jiji la Kampala kuwatoa watu nje, au kufyatua mabomu ya machozi ili kuwafurumusha nje. Wafanyabiashara na wateja wao walikuwa wakitoka nje wakiwa wamenyoosha mikono juu.

Vurugu nyingi zinarekodiwa na Waganda wa kawaida na kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii. Waganda wameelezea hasira na mshtuko kwa kiwango cha nguvu inayotumiwa na polisi - na kwa maisha yaliyopotea.

Upinzani unasema utekelezaji wa vizuizi vya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona unatumika kwa kubagua.

Rais wa sasa Yoweri Museveni ameendelea kufanya kampeni bila kukatizwa - wakati hajahutubia umati, wafuasi wake wamekuwa wakikusanyika kumkaribisha katika miji mbalimbali.

Msemaji wa serikali ya Uganda , Ofwono Opondo, amesema polisi wamechukua hatua stahili . Amewanyooshea kidole waandamanaji kwa kutotafuta "njia za amani" za kueleza na "kutatua" changamoto kwa kutumia njia za kisheria.