Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona : Watu weusi wanaweza kuambukizwa corona mara 2 zaidi ya wazungu
Watu weusi wanakabiliwa na hatari ya kupata virusi vya corona mara mbili zaidi ya wazungu, kwa mujibu wa utafiti uliyofanyiwa watu milioni 18.
Utafiti huo pia umebaini kuwa Wahindi wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi mara moja na nusu ikilnganishwa na wazungu - na huenda wakahitaji uangalizi wa dharura wa kimatibabu.
Watafiti wanasema matokeo ya uchunguzi wao una "umuhimu wa dharura kwa afya ya umma" na kuibua maswali kuhusu jinsi chanjo inaweza kupeanwa kwa kuzingatia makundi yaliyo kwenye hatari ya kupata maambukizi ili yapatiwe kipaumbele.
'Ubaguzi wa kimuundo'
Ushahidi umekuwa ukiongezeka kuhususiana na madai kwamba watu kutoka jamii ya wachache wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa Covid-19.
Lakini wanasayansi hawajabaini ikiwa hatari ya maambukizi inajikita katika uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa au kuwa mgonjwa zaidi kutokana na virusi.
Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Leicester na Nottingham waliangazia data kutoka kwa tafiti nane nchini Uingereza na 42 kutoka Marekani.
Ushahidi wa awali uliashiria kuwa Wahindi wako katika hatari ya kufa kutokana na ugonjwa huo wakilinganishwa na makundi mengine.
Lakini mtafiti mkuu Dkt Manish Pareek samesema kulikuwa na ushahidi mdogo kuonesha hatari hiyo ilichangiwa na sababu za kimaumbile.
'Watu kutoka makabila madogo wanakabiliwa na uwezekano wa kufanya kazi katika sekta za kutoa huduma za afya ya jamii na wanaishi katika makazi ya pamoja ambayo wakati mwingine yanajumuisha vizazi kadhaa', aliongeza kusema.
Mtafiti mkuu Shirley Sze anasema: "Ushahidi wa kuongezeka kwa hatari ya ongezeko la maambukizi miongoni mwa makundi ya watu wachache ni muhimu wa dharura unaostahili kuangaziwa katika afya ya umma.
"Lazima tufanye kazi ili tupunguze viwango vya maambukizi miongoni mwa watu walio kwenye makundi hatari kwa kuwawezesha kupata huduma za afya wakati unaofaa na kushughulikia tofauti za kijamii na kimuundo zinazochangia ukosefu wa usawa katika utoaji wa huduma za afya."
Watafiti wanaashiria kuwa "ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kimuundo pia unaweza kuchangia hatari kubwa ya matokeo mabaya majaribio ya chanjo ndani ya jamii ya watu wachache".
Hayo yanajiri baada ya mshauri wa kisayansi wa serikali awali kupendekeza kuwa ubaguzi wa rangi haukuelezea hatari iliyoongezeka kwa watu kutoka jamii za watu wachache.
Akizungumza mwezi uliopita katika hafla ya kutoa ripoti ya serikali kuhusu ukosefu wa usawa katika kushughulikia ugonjwa wa Covid Dkt Rhagib alisema, kabila halistahili kutumiwa kubaini ikiwa watu wako katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi.
Ameongeza kwamba kuangazia watu wote waliyo na changsmoto zingine za kimaisha kama vile, ajira na makazi kutasaidia watu wengi -kutoka makundi yote ya kijamii.