Matokeo ya uchaguzi Marekani: Kile ambacho Trump na Biden bado wanahitaji kupata ushindi

Chanzo cha picha, Getty Images
Usiku wa uchaguzi nchini Marekani unaelekea kugeuka wiki ya uchaguzi. Hivi ndivyo wagombea wanahitaji kutokea ili kushinda Ikulu.
Kura ya maoni kabla ya siku ya uchaguzi zinaashiria uwezekano wa yeyote kushindi kuanzia kwa Joe Biden hadi ushindi mwembamba wa Donald Trump ambapo huenda akapoteza wingi wa kura kimataifa lakini kwa mara nyingine tena akashinda katika majimbo yanayokabiliwa na ushindani mkali apate kura ya wajumbe.
Baada ya shughuli ya kuhesabu kura iliyoendelea usiku kucha hadi mapema asubuhi ya ya Jumatano, ushindi wa kishindo wa Biden unatiliwa shaka. Hata akishinda itakuwa ushindi mwembamba . Kilichosalia ni suala na ni nani atakayeshinda na atashinda vipi - na itachukua muda gani kujua hilo.
Donald Trump tayari amejitangazia ushindi na kuwashutumu wapinzani wake kwa kufanya udanganyifu katika uchaguzi. Hii hata hivyo hiyo sio hali halisi ilivyo. Bado kuna mamilioni ya kura zilizopigwa kisheria ambazo bado zinahesabiwa.
Ushindani huo wa kitaifa sasa umesalia kuamuliwa na matokeo katika majimbo ya : Arizona, Georgia, Wisconsin, Michigan na Pennsylvania.
Nani atakayeshinda katika majimbo yaliyo na ushindani mkali?
Arizona inaonekana kuegemea upande wa Biden, kumaanisha Democrat watahitajika kushinda majimbo mawili kati ya matatu yaliyopewa jina la "blue wall" mwaka 2016 ambayo ni - Wisconsin, Michigan na Pennsylvania - kupata ushindi.
Biden yuko nyuma katika majimbo hayo matatu, lakini kura ambazo hazijahesabiwa zitawafaidi Democrat - ambazo pengine huenda zikamsaidia kumsongeza mbele.
Kuna zaidi ya kura milioni 1.4 zilizopigwa kwa njia ya posta ambazo hazijahesabiwa Pennsylvania, na huenda ikachukua siku kadhaa kukamilisha shughuli ya kuzihesabu. Miji mikubwa ya Michigan (Detroit) na Wisconsin (Milwaukee) pia haijatoa matokeo kamili, na huenda ikasaidia Democrats.
Huku hayo yakijiri Georgia inaalia kuwa kura ya turufu. Mapema siku ya Jumanne ilionekana kuegemea upande wa Trump lakini hilo halikutokea. Matokeo kutoka Atlanta ambayo ni rafiki kwa Biden- imechelewa kutangazwa baada ya bomba la maji kupasuka karibu na eneo la kuhesabiwa kura.
Ushindi wa Democratic katika eneo la Georgia utamaanisha Biden anahitaji kunyakua moja kati ya majimbo ya kati na magharibi.
Makabiliano ya kisheria yananukia
Kile kilichohofiwa kutokea kimeanza kujitokeza, huku Biden akidai kuelekea kupata ushindi naye Trump akitoa madai ya wizi wa kura na udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi.
Hivi ni vichocheo vya makabiliano ya kisheria ya muda mrefu, ambavyo vitawaacha wafuasi wa upande utakaoshindwa na machungu na hisia ya kudanganywa.

Japo matokeo ya ya mwisho bado haijulikaniu, kile kilicho wazi katika usiku wa uchaguzi ni kwamba Marekani inaelekea kugawanyika vikali.
Wapiga kura wa Marekani hawakumchukulia kwa uzito Bw Trump. Wala hawakumuidhinisha kwa kiwango kikubwa kama alivyotarajia rais.
Badala yake, ulingo wa makabiliano umefunguliwa- na malumbano ya kisiasa utaendelea kushuhudiwa katika uchaguzi huu












