Uchaguzi wa Marekani 2020: Trump, Biden wachuana vikali

Chanzo cha picha, Getty Images
Matokeo ya awali ya urais nchini Marekani kati ya Donald Trump na hasimu wake wa Democrat Joe Biden yanaonesha mchuano kuwa mkali katika majimbo kadhaa.
Donald Trump anaongoza katika jimbo la Florida kwa karibu kura zote zilizohesabiwa.
Lakini majimbo mengine ya Georgia, Pennsylvania, Wisconsin, Michigan, Arizona, Ohio, Texas, na North Carolina chochote kinatarajiwa.
Zaidi ya watu milioni 100 walikwisha piga kura zao za mapema.
Marekani inaonekana kuwa idadi ya waliojitokeza zaidi katika karne.
Udhibiti wa Congress pia uko hatarini. Pamoja na Ikulu ya White House, Republican wanawania kupata idadi kubwa ya viti vya Seneti.
Bunge la wawakilishi linatarajiwa kuwa katika mikono ya Democratic.
Matokeo yakoje mpaka sasa?

Katika majimbo ya Pennsylvania, Michigan, Wisconsin na Ohio yanaonekana yanaweza kwenda kwa upande wowote katika mbio hizi za kuelekea ikulu.
Majimbo kama Arizona na Texas, ambayo yalikuwa ngome ya Republican, pia yanaweza kunyakuliwa na yeyote. Ushindi wa Biden jimbo la Texas utakuwa tetemeko la kisiasa.
Kura zinazochuana zinaendelea kuhesabiwa pia katika majimbo ya East Coast, Georgia na North Carolina.
Florida na Pennsylvania kwa pamoja yanasemekana kuwa lazima ushindi uende kwa Bwana Trump, ikiwa atachaguliwa awamu ya pili.

Chanzo cha picha, Reuters
________________________________________
Hakuna jambo lolote la kushangaza lililojitokeza katika majimbo mengine, BBC inatabiri kuwa Trump atayashikilia majimbo kama Alabama, Indiana, North Dakota,South akota, Kentucky, Tennessee, Oklahoma, Arkansas na West Virginia, yote kama yanavyotarajiwa.
Pia BBC inatabiri kuwa Bwana Biden atakama jimbo la makazi yake Delaware, sambamba na NewYork, Colorado, Vermont, Maryland, Massachusetts, New Jersey na Washington DC .
CBS News, Mshirika wa BBC nchini Marekani, inatabiri kuwa South Carolina, Nebraska, Kansas, Louisiana na Wyoming yanaelekea kwa Trump.
________________________________________

Chanzo cha picha, Reuters
CBS pia inatabiri kuwa Minnesota, New Mexico, Maine, Connecticut, Illinois, Rhode Islaand New Hampshire zinaelekea kwa Bw.Biden.
Trump alipoteza kwa kura chache jimboni Minnesota mwaka 2016 na kampeni yake ina matumaini kuwa atalinyakua jimbo hilo hilo kipindi hiki.
Kura zitakamilika kuhesabiwa leo Jumatano, majira ya saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kura ya maoni inasema kuwa Bw.Biden anaongoza kwa kura za wanawake kwa 57% kwa 42%, wapiga kura weusi (87% kwa 11%), walio na umri wa chini ya miaka 29 (64% kwa 33%) na miongoni mwa wapiga kura wenye shahada au bila shahada ya chuo kikuu.
Trump anaelekea kupata faida kwa wapiga kura wenye miaka 65 na zaidi kwa (51% kwa 48%).
Kura ya maoni imempa ushindi Biden, lakini yameonesha kuwa mchuano ni mkali hasa katika majimbo yanatarajiwa kuamua matokeo kati ya wawili hao.

Chanzo cha picha, EPA
Bw.Trump ambaye anatarajia kurejea ikulu, anatarajiwa kuhutubia taifa baadae jioni.
Biden alikuwa nyumbani na familia yake jijini Washington, Delaware, na wasaidizi wake wachache, kwa mujibu wa CBS.
Utabiri umeegemea mchanganyiko wa data za kura ya maoni na kura halisi zilizopigwa.
Katika uchaguzi wa Marekani , wapiga kura huamua katika majimbo .














