Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Qian Xuesen: Mwanasayansi aliyefukuzwa Marekani licha ya kuisaidia kufika mwezini kwa mara ya kwanza
Mwanasayansi wa China aliyesaidia nchi mbili zenye nguvu zaidi duniani kufika kwenye mwezi lakini sasa hivi anatambulika katika nchi moja tu. Nini kilichotokea?
Huko Shanghai kuna makumbusho yenye bidhaa za kale 70,000 ambazo zote ni za mtu mmoja tu aliyejulikana kama, "mwanasayansi wa watu" Qian Xuesen.
Qian ndio mwanzilishi wa mradi wa makombora na anga za juu China. Utafiti wake ulisaidia ubunifu wa roketi ambao uliwezesha China kupeleka Setelaiti ya kwanza kwenye anga la mbali, na makombora ambayo yalikuwa sehemu ya silaha za nyuklia na anachukuliwa kama shujaa wa taifa.
Lakini katika nchi nyingine zenye nguvu zaidi alikosomea na kufanya kazi kwa mwongo mmoja, mchango wake hautambuliki kabisa.
Qian baada ya kuonesha kipaji chake awali, alitunukiwa ufadhili wa masomo katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts Marekani.
Qian alizaliwa 1911 wakati utawala wa China wa Kifalme ulikuwa unakaribia kubadilika na kuwa wa Jamhuri.
Baada ya kuhitimu chuo cha Massachusetts aliingia chuo kingine cha Teknolojia cha California aliposoma na mwanasayansi tajika duniani Theodore von Karman.
Alikuwa ofisi moja na mwanasanyansi mwingine mashuhuri Frank Malina.
Kuna siku ambayo Qian alijikuta kwenye mjadala wa mahesabu na Bwana Malina kuhusu utafiti wa namna ya kusukuma roketi.
Lakini wakati huo hakuna aliyechukulia mazungumzo hayo kwa uzito hadi kulipotokea vita vya pili vya dunia.
Kundi hilo la wanasayansi lilivutia jeshi la Marekani ambalo lililipa pesa ili utafiti wa kusaidia ndege kupaa na vifaa vya kuwezesha hilo viliwekwa kwenye mbawa za ndege ili kuziwezesha kupata hewa kwenye barabara ya ndege.
Qian alipewa cheti cha mtafiti wa silaha na kupewa kazi katika serikali ya Marekani kama mshauri wa Bodi ya Sayansi.
Na hadi wakati vita vya pili vya dunia vimalizika alikuwa miongoni mwa wataalamu maarufu kuhusu masuala ya ndege kutumwa na alitumwa pamoja na Theodore von Karman kwenye ujumbe maalum Ujerumani lengo likiwa ni kupeleleza wahandisi waKinazi.
Lakini kufikia mwisho wa mwongo huo taaluma ya Qian iliyokuwa inang'aa ilizima ghafla pale China na Marekani zilipoanza kuwa maadui.
Nchini China mwenyekiti Mao alitangaza kuundwa kwa Jamhuri ya Kikomunisti mwaka 1949, na mara moja sana Marekani ikaichukulia China kama adui", amesema Chris Jespersen.
Mara kukachaguliwa mkurugenzi mpya katika oparesheni za ndege ambaye aliamini kwamba kuna watu wanaofanya upelelezi katika maabara yao huko Marekani.
Wakati vita baridi vinaendelea, wakati huo ndio Shirika la Ujasusi la Marekani lilipodai kuwa Qian na wanasayansi wengine, Frank Malina na wengine wa Kikomunisti ni tishio kwa usalama wa taifa la Marekani.
Makosa aliofunguliwa Qian ni pamoja na kuonesha kuwa alihudhuria mkutano ulioshukiwa ulikuwa wa chama cha China cha Kikomunisti ingawa alikanusha madai hayo na kusema yeye sio mwanachama,
Hata hivyo, utafiti mpya ulionesha kwamba alijiunga na chama hicho wakati mmoja na Frank Malina mwaka 1938.
Zuoyue Wang, profesa wa historia wa chuo kikuu cha Ufundi cha California, Pomona, anasema hakuna ushahidi ulioonesha kwamba Qian aliwahi kufanya upelelezi kwa ajili ya China ama alikuwa afisa wa kiintelijensia alipokuwa Marekani.
Hata hivyo alipokonywa leseni yake na kuhukumiwa kifungo cha nyumbani. Wanasayansi wenzani akiwemo Theodore von Karman waliandikia serikali kuomba Qian aachiliwe huru kwasababu hakuwa na hatia lakini hakuna aliyesikiliza ombi hilo.
Mwana 1955, wakati Qian alikuwa ametumikia kifungo cha nyumbani kwa miaka mitano, Rais Eisenhower alifanya maamuzi ya kumfurusha nchini humo na kumrejesha kwao China kwa lazima.
Na hatimae mwanasayansi huyo aliondoka Marekani akiwa na mke wake na watoto wake wawili waliozaliwa Marekani kwa kutumia boti.
Wakati huo aliwaambia wanahabari kwamba hatawahi kurejea tena kuingiza guu lake Marekani na mwanasayansi huyo akatimiza ahadi yake.
"Alikuwa miongoni mwa wanasayansi maarufu sana Marekani. Alikuwa amechangia pakubwa katika nchi hiyo kimaendeleo ya kisayansi na pia kuna uwezekano mkubwa angeifanyia Marekani uvumbuzi wa ajabu. Kwa hiyo sio tu kwamba ilimdhalilisha lakini pia ilimsaliti," anasema mwanahabari na mwandishi, Tianyu Fang.
Qian alipokelewa China kama shujaa lakini hakujumuishwa moja kwa moja kwenye chama cha Kikomunisti.
Na alipojiunga na chama hicho rasmi mwaka 1958 alijitahidi sana kutoenda kinyume na utawala uliokuwepo.
Na hatimae alifanikiwa kujiendeleza katika taaluma yake.
Wakati anawasili China kulikuwa na uelewa mdogo kuhusu masuala ya sayansi ya roketi, lakini miaka 15 baadae aliongoza uzinduzi wa satelaiti ya kwanza ya China kwenda kwenye anga za mbali.