Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Charlie Hebdo: Uturuki yaapa kuchukua hatua juu ya kibonzo cha Erdogan
Uturuki imeapa kuchukua hatu za "kisheria, na kidiplomasia '' kuhusiana na katuni ya Rais Tayyip Erdogan iliyochapishwa katika jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo.
Kibonzo hicho kinamuonesha rais wa Uturuki akinyanyua nguo ya mwanamke aliyekuwa amejifunika kitambaa kichwani.
Vyombo vya habari vya taifa hilo vinasema waendesha mashitaka wa Uturuki wameanzisha uchunguzi rasmi kuhusu jarida la Charlie Hebdo.
Hali ya wasiwasi imetanda kati ya Ufaransa na Uturuki baada ya Rais Emmanuel Macron kuahidi kuchukua msimamo mkali dhidi ya Waislamu wenye itikadi kali.
Bw Erdogan ametoa wito wa kususiwa kwa bidhaa za Ufaransa na amesema kuwa Bw Macron anahitaji "kufanyiwa uchunguzi wa akili".
Mzozo huo umeendea kote duniani, na kusababisha maandamano dhidi ya Ufaransa na kususiwa kwa bidhaa zake katika nchi kadhaa za kiisalamu ikiwa ni pamoja na Bangladesh, Kuwait, Jordan na Libya.
Mtafaruku huo pia ulifuatia ahadi ya Bw Macron ya kulinda mfumo usioegamia dini yoyote baada ya mauaji ya kikatili ya Mwalimu Mfaransa aliyewaonesha wanafunzi vibonzo vya Mtume Muhammad darasani.
Rais alisema kuwa mwalimu , Samuel Paty, "aliuawa kwasababu waislamu wenye itikadi kali wanataka hali yetu ya baadaye ", lakini Ufaransa "hatutaacha katuni zetu ".
Michoro ya mtume Muhammad inaaminiwa kuwa ni mwiko katika Uislamu, na ni kuwadhalilisha Waislamu.
Lakini utambulisho wa Ufaransa ni kwamba haiegamii dini yoyote. Kuzuwia uhuru wa kujieleza ili kulinda hisia za jamii moja kunakiuka umoja, taifa linasema.
Utururuki ilijibu nini kuhusu kibonzo
Kibponzo hicho kimesababisha hasira kubwa ndani ya serikali ya Uturuki.
Mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Fahrettin Altun alisema: "Charlie Hebdo lilichapisha tu msururu wa kile kinachoitwa vibonzo vyenye michoro ya picha vzinazodaiwa kwa ni za rais wetu. Tunalaani juhudi hizi zinazokera za jarida hili za kusambaza utamaduni a ubaguzi na chuki ."
Makamu wa rais Fuat Oktay aliitolea wito jamii ya kimataifa kupaza sauti yake dhidi ya "ukosefu huu wa heshima ".
"Huwezi kumfanya mjinga kila mtu ka kujificha nyuma ya uhuru wa mawazo ," alisema kwenye Twitter.
Katika kujibu, jarida linaloegamia upande wa serikali ya Uturuki Misvak lilituma vibonzo kadhaa vya kumkosoa Bw Macron na Charlie Hebdo kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Charlie Hebdo sio geni kwa taarifa za utata.
mwaka 2015, watu 12 waliuawa katika shambulio dhidi ya ofisi za jarida hilo mjini Paris. Lililengwa na waislamu wenye itikadi kalikwa kuchapisha vibonzo vya Mtume Muhammad.
Mwaka huo huo, Urusi ilikosoa vikali jarida hilo kwa vibonzo viwili vya ndege ya Sinai ambayo ilifanya ajali na kuwauwa watu 224, wengi wao walikuwa ni Warusi.
Mwaka 2016, kibonzo kilichowaonesha wahanga wa tetemeko la ardhi la Italia kama sahani iliyojaa tambi kilisababisha hasira.
Ni zipi habari za hivi karibuni kuhuzu kisasi dhidi ya Ufaransa?
Ghadhabu inaendelea kuongezeka kote katika ulimwengu wa kiarabu dhidi ya Bw Macron kuhusu mtizamo wake juu ya Uislamu na Mtume Muhammad. Hasira hii imepelekea maandamano, miito ya kususia bidhaa za Ufaransa na onyo kwa raia wa Ufaransa.
nchini Bangladesh, mamia ya watu walishiriki katika maandamano ya kuipinga Ufaransa nje ya msikiti wa Kitaifa wa Baitul Mukarram Jumatano. Waandamanaji walichoma sanamu na picha zilizotengenezwa kwa mfano wa Bw Macron.
Kikundi cha kiimani nchini Malaysia kilitoa wito wa kuondolewa madukani kwa bidhaa kutoka Ufaransa . Baraza la ushauri la Malaysia (MCC) lilisema kuwa ususiaji huo "ulituma ujumbe mkubwa kwa Ufaransa ".
Bidhaa za Ufaransa tayari zimekwishaondolewa katika masoko makubwa- supermarket katika Jordan, Qatar, Kuwait na baadhi ya nchi za Mashariki ya kati.
Unaweza pia kusoma:
Ombi la ku fanya uhalifu vitendo vya "kuupinga Uislamu'' lilitoka kwa Grand Imam wa Chuo kikuu cha al-Azhar nchini Egypt. Rais wa nchi hiyo , Abdul Fattah al-Sisi, alisema Jumatano kuwa uhuru wa kujieleza lazima usitishwe kama unawaudhi watu zaidi ya Bilioni 1.5.
Huku kukia na hofu juu ya usalama, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imewatahadharisha raia wake walioko Indonesia, Iraq na Mauritania -nchi ambako maandamano yamefanyika -na amewataka wawe waangalifu.