Trump amepanga kuiondoa Sudan katika orodha ya mataifa yanayodhamini ugaidi

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi iwapo italipa fidia ya dola milioni 335 (£259m).
Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amejibu kuwa fedha hizo zimeshatolewa tayari lakini hakukuwa na majibu ya haraka kutoka Marekani.
Sudan imekuwa katika orodha ya wafadhili wa ugaidi tangu mwaka 1993 wakati kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden alipoishi huko kama mgeni wa serikali.
Fidia hiyo inahusisha mabomu yaliolipuliwa na al-Qaeda mwaka 1998 katika balozi za Marekani barani Afrika.
Shambulio hilo lililotokea Tanzania na Kenya lilouwa watu zaidi ya 220 na fidia hiyo inapaswa kulipwa kwa wahanga na familia za waliopoteza ndugu zao", bwana Trump alisema.
Unaweza pia kusoma:
Uhusiano wa Marekani na Sudan umeimarika tangu rais Omar al-Bashir alipoweza kukabiliana na maandamano makubwa mwaka jana.
Bwana Bashir aliweza kukabiliana na mgogoro ambao umekuwa ukilikabili taifa hilo la Afrika kwa miaka 30.
Kuondolewa kwa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi itakuwa habari njema sana katika nchi hiyo ambayo chakula , mafuta na dawa ni ghali na bado vitu vinaendelea kuwa ghali na kushtua wengi, mwandishi wa BBC Anne Soy anasema.

Trump amesema nini haswa?
Katika kurasa yake ya Tweeter, Donald Trump ameandika: "Habari njema! Serikali mpya ya Sudan, ambayo inachukua jitihada thabiti, imekubali kulipa fidia ya dola milioni 335 kwa wahanga wa shambulio la kigaidi na familia zao.
"Muda ambao ntaiondoa Sudan katika orodha ya mataifa yanayowafadhili ugaidi.
Basi haki itakuwa imetendeka kwa Wamarekani na itakuwa ni hatua kubwa kwa Sudan!"
Rais wa Marekani ana mamlaka ya kuliondoa taifa katika orodha ya wafadhili wa ugaidi.
Sudan ni miongoni mwa mataifa manne ambayo yapo kwenye orodha hiyo - pamoja na Korea Kaskazini , Iran, na Syria.
Sudan ipo katika nafasi gani?
Mara baada ya ujumbe huo wa Twitter Bwana Hamdok alitangaza kuwa tayari ametoa fedha , TV ya taifa imeripoti.
Hicho ndicho kigezo cha mwisho ambacho walipewa ili kuondolewa katika orodha ya wafadhili wa ugaidi.
Bwana Hamdok aliosema Sudan inategemea kupokea taarifa rasmi kutoka serikali ya Marekani.Kuwa katika orodha hiyo kumesababisha athari nyingi katika taifa hilo.
Agosti 7, mwaka 1998, ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam na Nairobi , gari lililokuwa na bomu lilisababisha mlipuko.
Zaidi ya watu 200 waliuawa mjini Nairobi na watu wapatao 11 waliuawa Dar es Salaam, Tanzania. Maelfu ya watu walijeruhiwa na wengi walikuwa raia.
Kufuatia tangazo la rais wa Marekani la mpango wa kuiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi, wahanga wengi wa shambulio la bomu la mwaka 1998 katika balozi za Marekani wamekataa kupokea fidia hiyo.
Mahakama ya Marekani ahiitaji kuiondoa Sudan katika orodha hiyo ili kupata fursa ya kupata ufadhili wa kimataifa na kuingia katika mkataba kufuatia kuondolewa kwake.
Sudan ilikataa kuzungumza moja kwa moja na wahanga waliokuwa wanafanya kazi katika ubalozi wa Marekani na wakiwa na matumaini kuwa wanaweza kumaliza kumaliza suala hilo wakati Marekani haina mamlaka ya kutatua mgogoro huo kisheria.
Zaidi ya wahanga 500 kati ya 700 wamesaini barua ya kukataa fidia iliyotolewa, wakidai kuwa hawawezi kuwasaliti wahanga wengi walioungua vibaya katika shambulio lile.
Na Marekani haina mamlaka ya kutatua madai ya mataifa ya kigeni , ila wahanga ndio wana haki na wajibu wa kuafikiana katika suala hilo
Wanasema wahanga ndio wanapaswa kusema nini wanahitaji kama fidia ambayo itakuwa sawa kwao jambo ambalo Sudan imelikataa kulifanya.












