Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Paka mkubwa mwenye miaka 2000 agundulika kwenye michoro ya Nazca, Peru
Mchoro wa paka mkubwa umegundulika katika jangwa la Nazca nchini Peru.
Mistari ya Nazca, eneo la urithi wa dunia, ni eneo la mitindo ya michoro ya ardhini-kitaalamu geoglyphs-iliyoundwa miaka karibu 2,000 iliyopita.
Wanasayansi wanaamini kuwa paka , michoro ya mnyama ya Nazca, iliundwa kwa sababu ya migandamizo kwenye sakafu ya jangwa.
Paka kisha hakutambuliwa hadi mipango ilipopangwa hivi karibuni kama njia mpya inayoongoza jukwaa la uchunguzi.
Jukwaa hilo linatoa nafasi nzuri kwa wageni kuona michoro mingine mingi.
Katika taarifa, Wizara ya utamaduni imesema: "Mchoro huo haukuonekana sana na ulikuwa karibu kutoweka, kwa sababu iko kwenye mteremko mkali ambao unakabiliwa na athari za mmomonyoko wa asili."
Iliongeza kuwa michoro hiyo, ambayo ina urefu wa mita 37, imesafishwa na kuhifadhiwa juma lililopita.
Johny Isla, Mwanaikolojia Mkuu nchini Peru katika eneo la michoro ya Nazca , alilimbia shirika la habari la Efe kuwa paka aliishi kabla ya tarehe ya utamaduni wa Nazca - ambayo iliunda michoro mingi kutoka 200 hadi 700 BK.
Paka huyo, alisema, aliishi kuanzia miaka 500 kabla ya Kristo mpaka 200 AD wakati wa kipindi cha Paracas.
''Tunajua hilo kutokana na kulinganisha picha ,'' alisema .''Michoro ya Paracas, kwa mfano, inaonesha ndege, paka na watu ambao wanaweza kulinganishwa kirahisi kwenye michoro hiyo.''