Msemaji wa Ikulu ya Marekani Kayleigh McEnany akutwa na virusi vya corona

HABARI ZA HIVI PUNDE
Iliyochapishwa

Msemaji wa Ikulu ya Marekani akutwa na virusi vya corona.

Afisa habari wa Ikulu ya Marekani Kayleigh McEnany ni pia ni msaidizi wa karibu wa Rais Trump kukutwa na virusi vya corona

Katika ukurasa wa twitter aliandika: ''Baada ya kukutwa sina maambukizi baada ya kupima mara kwa mara, ikiwemo kila siku tangu Alhamisi, Nimekutwa na maambukizi ya Covid-19 siku ya Jumatatu asubuhi huku nikiwa sina dalili zozote za kuugua.''

Aliongeza kuwa hakuna wanahabari wanaofikiriwa kukaribiana naye kulingana na kitengo cha matibabu cha Ikulu.

"Kwa kuongezea, kwa kweli sikuwa na ufahamu kuhusu kupimwa kwa Hope Hicks kabla ya kufanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu mnamo Alhamisi," alisema akimaanisha msaidizi wa Trump ambaye alikuwa mfanyakazi wa kwanza wa Ikulu kupima kabla ya kugundulika na maambukizi.

McEnany ameongeza kuwa atajitenga na "ataendelea kufanya kazi kwa niaba ya watu wa Marekani".