Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini mapinduzi ya Mali yameathiri mapambano dhidi ya wana-jihad?
Mwezi mmoja baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, viongozi wa jeshi wanasisitiza kuwa mapambano yao dhidi ya makundi ya kijihadi yanaendelea, lakini suala la kurejesha demokrasia bado linaonekana kuwa tete, ameandika mchambuzi wa Afrika Magharibi Paul Melly.
Hatua ya mwisho itakayotoa mustakabali wa Mali kupitia uongozi wa mpito kuelekea uchaguzi mkuu mpya wiki kadhaa baada ya wanajeshi kuchukua madaraka mjini Bamako, na kumlazimisha Rais Ibrahim Boubacar Keïta kujiuzulu haijafikiwa, japo waziri wa ulinzi Ban Ndaw ametangazwa kuwa kiongozi wa mpito .
Wanajeshi hao wanaamini wataushawishi muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi Ecowas kukubali mpango wao, baada ya mazungumzo ya wikendi kuwaondolea shaka wapinzani.
Lakini kutoka nje, hatua hiyo imatuma ujumbe wa wazi kwa washirika wa kimataifa ambao wana maelfu ya wanajeshi waliopelekwa naeneo ya kaskazini mwa Mali kukabiliana na mzozo wa kiusalama wakati wakishambuliwa na makundi ya kijihadi wakati maeneo ya kati yanahofia kuzuka kwa mapigano ya kikabila na vurugu
Meja kanali Ismaël Wagué, msemaji wa jeshi - la kitaifa lilojitangazia kukomboa wanachi (CNSP) - anasisitiza kuwa vikosi vya kulinda usalama vya Umoja wa Mataifa nchini Mali, vikosi vya kupambana na vikosi vipya maalum vya Ulaya vinavyoendesha oparesheni katika eneo hilo vilikuwa ''vinashirikiana kuleta uthabiti".
Zaidi ya mwaka au karibu mwaka mmoja uliopita kumekuwa na ishara kwamba raia wa Mali wanachukizwa na uwepo wa vikosi vya Ufaransa katika nchi yao, licha ya jukumu wanalotekeleza kama mshirika muhimu na hata wakati mwingine kuonekana kuchua jukumu la vikosi vya taifa.
Lakini Kanali Wagué anajiepusha na hoja hizo amabazo zinazoibua taharuki kitaifa.
Aliweka wazi kwamba viongozi wapya wa kijeshi wako tayari kuedelea kufanya kazi kwa karibu na vikosi vya kimataifa - sawa na vile wanavyotarajia kuafikiana na Ecowas katika mpango wao utakaotoa muelekeo wa kisiasa wa siku zijazo.
Japo makubaliano ya mwisho na muungano wa kikanda juu ya masharti ya mpito yanaonekana kulega lega bado tishio kutoka kwa makundi ya kijihadi linasalia.
Kwa hivyo harakati za kijesho katika eneo la kaskazini mwa nchi zinaendelea - na inasadikiwa kuwa bado ni oparesheni hatari.
Wanajeshi wawili zaidi wa Ufaransa waliuawa kutokana na bomu la kutegwa kando ya barabara katibu na mji wa Taoudenni Septemba 05, ikiwa ni tukio la hivi karibuni katika mzozo huo ambao umesababisha vifo vya wanajeshi 45 wa Ufaransa na kuwajeruhi wengine wengi kutoka vikosi vya Mali na vile vya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2011.
Changamoto kubwa kwa jeshi la Mali
Wakati wanajeshi wengi wameuawa katika mashambulio madogo, pia wamekabiliwa kuwa mashambulio makubwa ambayo yamesababisha makumi wao kufariki, hasa wakati kambi zao nchini Mali zinaposhambuliwa.
Kisa cha kwanza ni kale cha - the "mauaji ya Aguelhok" January 2012, ambapo wanamgambo wa kijihadi wa Tuareg walipowaua wanajeshi 100 baada ya kuteka kambi moja ndogo katika eneo la jangwani - ambayo ilichangia hali ya kutoaminiana miongoni mwa maafisa wa kijeshi na matokeo yake yakawa uasi uliosababisha mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka huo.
Zaidi ya miaka saba baadae, na licha ya mango wa muda mrefu wa Muungano wa Ulaya kuwa na vikosi vya nchini humo ili kuwapa msaada na kmotisha bado majeshi hayo yanakabiliwa na mashambulio. makati mara kwa mara.
Kundi la Islamic State katika eneo kuu la Sahara (ISGS), ambalo linashirikiana na lile la kigaidi mashariki ya kati limeade kuhusika na mashambulio hayo
Mwaka jana kati ya Septemba 30 September na Oktoba mosi, hadi maafisa 85 wa kijeshi walifariki wakati wanamgambo wa ISGS waliposhambulia kambi ya Boulikessi katika mpaka wa Burkina Faso .
Na baadae mwezi Novemba mosi 2019, wanajeshi wengine 49 waliuawa na wanamgambo wa ISGS assault walioshambulia kambi ya Indélimane, karibu na mpaka wa Niger mashariki mwa nchi hiyo.
Ukosefu wa vifaa na mafundisho ya kijeshi umetajwa kuchangia majanga kama hayo
Lakini pia inasemekana kuchangiwa na ukosefu wa uongozi mzuri wa kisiasa kutoka kwa rais Keïta mjini Bamako na hali ya kujihisi kutelekezwa na serikali ambayo ilisababisha kuchelewa kusainiwa kwa mkataba wa amani wa mwaka 2015 uliofikiwa kati ya serikali na wanamgambo wa kaskazini Tuareg wanaotaka kujitenga.
Kuchelewesha harakati za kuvunja nguvu za wapiganaji wanaotaka kujitenga na kun'gatua madaraka na fedha hadi katika ngazi ya kimaeneo imechochea hali ya kukata tamaa ambayo inaweza kuendeleza ugaidi.
Hali hiyo huenda imekuwa chanzo kikuu cha mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 18 - ambayo viongozi wake walikuwa maafisa kadhaa walio na ujuzi na wanaofahamu mazingira magumu yanayowakabili wanajeshi katika eneo la kaskazini.
Katika kipindi kifupi kijacho, vikosi vya Mali vinaweza kuendelea na operesheni yao wakishirikiana na washirika wakuu wa kimataifa - ambao wanajumuisha vikosi vya Ufaransa Barkhane, majeshi ya wanachama wenzao kutoka nchi tano za eneo la Sahel (Mali, Mauritania, Burkina Faso, Niger na Chad), kikosi kipya malum cha Muungano wa Ulaya kilichopelekwa sehemu ya Takuba pamoja na vikosi vya kulinda usalama vya Umoja wa Mataifa Minusma.
Jukumu kudu la vikosi hivyo ni kudumisha ustawi wa nchi badala ya kuyatimua makundi ya kijihadi - lakini hatua hiyo haijasaidia kudhibiti usalama katika opareshini hiyo hatari duniani kwa Umoja wa Mataifa, ikizingatiwa kuwa wanajeshi 220 wameuawa tangu walipopelekwa huko 2013.
Kushughulikia malalamiko ya wenyeji
Lakini changamoto kuu inayokabili vikosi hivi vyote, vya kikanda na kitaifa ni kurudisha hali ya utulivu katika maeneo ya kaskazini na kati ya Mali kendo na kukabiliana na makundi ya wanamgambo.
Barkhane kwa mfano imefanya msururu wa mashambulio dhidi ya makundi ya kijihadi, ambapo makamanda kadhaa wakuu wanaojulikana, akiwemo Abdelmalek Droukdel, kiongozi wa al-Qaeda Juni 3 mwaka huu alipoingia nchini Mali kutoka kaskazini mwa Algeria.
Lakini mashambulio kama hayo yamechangia kuongezeka kwa uhasama kati ya wapiganaji wa kijihadi na vikosi via usalama katika kanda nzima ya kaskazini, kuanzia maeneo ya mto Niger na delta upande wa ndani karibu na Mauritania hadi mpaka wa mashariki ya mbali wa Niger.
Yaliyofikiwa kwenye mkataba wa amani wa Tuareg 2015
•Jamii ya kaskazini ya Tuareg imekuwa ikilalamikia kutengwa tangu uhuru mwaka 1960
•Wanamgambo wa kiislam walishirikiana na waasi wa Tuareg mwaka 2012 kuteka miji kadhaa
•Miji hiyo ilikombolewa mwaka 2013 kufuatia usaidizi wa kijeshi kutoka Ufaransa - na miaka miwili baadae mkataba uliotiwa saini ukiahidi maendeleo na ugatuzi wa madaraka katika eneo la kaskazini mwa Mali
•Lakini sio wapiganaji wote wanotaka kujitenga wamedhibitiwa kama ilivyokubaliwa na pia suala la kugatua madaraka limecheleweshwa hali inayoendelea kuzua mgogoro
•Hii imechangia ukosefu wa usalama na kufanya makundi ya kijihadi kuimarika
Na ingawa makamanda wachache - kama Abu Walid al-Sahrawi ambaye anatokea Sahara Magharibi ya ISGS - ambao ni wageni, wengi wao ni raia wa Mali.
Hata hivyo, wanamgambo wamekuwa wakitumia malalamiko ya wakaazi kujipatia umaarufu.
Msaada muhimu wa kimataifa
Vikosi vya usalama pekee havitatatua changamoto zinazokabili nchi hiyo.
Uongozi mzuri na utakaoangazia maendeleo hasa katika maeneo ambayo serikali imesitisha kutoa huduma muhimu unahitajika.
Bila Shaka usalama bado utakuwa sehemu ya mpango huo, kwa sababu bila ya kuwa na huduma muhimu kama vile haki, elimu na afya ya jamii haiwezi kutolewa na maafisa ikiwa hawatahakikishiwa usalama wao.
Lakini maendeleo ya kweli yanahitaji uongozi halali utakao tambulika kimataifa na utakaobuniwa kupitia mchakato ambao utadumisha yaliyofikiwa katika mkataba wa amani wa mwaka 2015.
Na hii ndio sababu mazungumzo yanayoendelea Bamako kuhusu uongozi wa mpito unaungwa mkono na Ecowas - na kuiondoa Mali kwenye vikwazo na kufungua milango ya misaada ya kimataifa - ni hatua muhimu.