Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamke aanguka kutoka kwa gari Uingereza akinasa video ya Snapchat
Mwanamke mmoja ameanguka kutoka kwa gari katika barabara kuu ya kwenda Westharm,Uingereza baada ya mlango wa gari aliyokuwa akitegemea kuchukua video ya Snapchat kufunguka.
Mwanamke huyo hakujeruhiwa vibaya lakini polisi wanasema "aliponea kifo".
Alitibiwa katika eneo la tukio na wahudumu wa afya. Hakuna mtu aliyekamatwa, polisi walisema.
Katika ujumbe uliowekwa kwenye Twitter, polisi wakitengo cha usalama bara barani walisema: "Kiti cha abiria upande wa mbele kilikuwa kikining'inia nje ya gari wakati mwanamke huyo alipokuwa akichukua video ya Snapchat katika barabara ya M25. Baadae alianguka barabarani kutoka kwa gari hilo.
"Ana bahati sana hakujeruhiwa vibaya au kufariki. #sinalakusema"
Msemaji wa polisi katika eneo hilo alisema: "Maafisa waliitwa katika barabara kuu ya M25 mapema asubuhi kufuatia ripoti kwamba abiria ameanguka kutoka kwa gari lililokuwa likienda.