Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni kwanini watu hawa huamua kutoweka na kutoonekana tena?
Katika maeneo yote ya dunia, kuanzia Marekani , Ujerumani, hadi Uingereza, kuna watu ambao kila mwaka wanaamua kutoweka na kutotaka kabisa wapatikane, wanaamua kuacha nyumba zao, kazi na hata familia ili kuanza maisha yao ya pili.
Hufanya hivyo bila hata kuangalia nyuma. Nchini Japan watu hao hufahamika kama jouhatsu .
Neno hilo linamaanisha "kuyeyuka", lakini pia hutumika kuwaelezea watu wanaopotea kwa makusudi au ambao hawajulikani walipo, wakati mwingine ka miaka, au miongo.
"Nilichoshwa na mahusiano na binadamu. Nikachukua kijisanduku kidogo na nikatoweka , " anasema Sugimoto, mwenye umri wa miaka 42, ambaye katika taarifa hii anatumia jina lake la pili la familia tu.
"Nilitoroka nikaenda mbali ."
Anasema kwamba kila katika mji mdogo wa kwao alimfahamu kutokana na familia yake pamoja na biashara yake iliyoshamiri, ambayo Sugimoto alitarajiwa ataiendeleza.
Lakini kulazimishwa kufanya kazi hiyo kulimfanya ajihisi mwenye machungu kiasi kwamba siku moja ghafla aliamua kuondoka na kutoamua kurudi kamwe na hakumwambia mtu yeyote ni api anakokwenda.
Kuanzia madeni, hadi ukosefu wa mapenzi ya kutosha katika ndoa, mambo yanayowachochea jouhatsu ku "yeyuka " ni tofauti.
Lakini wengi, kando na sababu zinazowafanya watoweke, huziendea kampuni ambazo huwasaidia katika mchakato wa kupotea.
Mchakato huu huitwa huduma za "kuhama usiku ", na mawasiliano baina ya mtowekaji au jouhatsu na kampuni inayomuhamisha huwa ni ya siri sana.
Makampuni haya huwasaidia watu kutoweka na kuondokana kabisa na maisha yao ya awali, kukata mawasiliano ya aina zote na husaidiwa kupata makazi katika maeneo yaliyojulikana.
"Kwa kawaida, sababu za kuhama huwa ni chanya, kama vile kwenda Chuo Kikuu, kupata kazi mpya au kuoa na kuolewa.
Lakini kuna kuhama kunakotokana na majonzi, wakati sababu inapokuwa kushindwa kuendelea na chuo, kupoteza kazi au unapotaka kutoroka jamii yako . "
Mfano ni Sho Hatori, ambaye alianzisha kampuni ya kusaidia kuwapoteza watu au "kampuni ya kuwahamisha watu usiku" miaka ya 1990 wakati uchumi wa Japan ulipoporomoka
Maisha ya pili
Wakati alipoanzisha kampuni hiyo, aliamini kuwa sababu zinazowafanya watu kuamua kuyakimbia matatizo ya maisha yao ni kufilisika , lakini hakuchelewa kugundua kuwa pia kulikuwa na ''sababu za kijamii''
"Tulichokifanya ni kuwasaidia watu kuanza maisha ya pili ," anasema.
Mtaalamu wa masuala ya kijamii Hiroki Nakamori amekuwa akifanya utafiri kuhusu suala la jouhatsu kwa zaidi ya muongo.
Anasema neno hilo lilianza kutumiaka katika miaka ya 1960 kuwaelezea watu walioamua kupotea.
Viwango vya talaka vilikuwa bado ni vya chini sana nchini , kwahiyo watu wakaamua kuondoka na kuwaacha wame au wake zao kuliko kuendelea kulumbana kutokana na matatizo ya kifedha na kupitia mchakato wa kesi za talaka.
"Nchini Japan ni rahisi sana kutoweka na usijuliane ulipo "kuliko katika nchi nyingine, anasema Nakamori.
Taarifa za kibinafsi ni kitu ambacho kinalindwa kwa hali na mali.
Watu waliopotea/ kutoweka wanaweza kutoa pesa zao katika mashine za ATM bila kugundulika, na watu wa familia hawawezi kuziona videoambazo waliwarekodi ndugu au jamaa zao wanapokuwa wametoweka.
"Polisi hawawezi kuingilia kati, labda kuwe na sababu nyingine, kama vile uhalifu au ajali. Kile ambacho familia inaweza kukifanya tu ni kufanya upelelezi wao wa kibinafsi . Au kusubiri tu. Hilo tu.
Maisha ya wanaopotea
Kwa wengi miongoni mwa Jouhatsu , licha ya kwamba waliacha maisha yao ya kwanza nyuma, majonzi na majuto huambatana nao.
"Nimekuwa wakati wote ninahisi kosa fulani ," anasema Sugimoto, mfanyabiashara ambaye alimtoroka mke na watoto wake katika mji mdogo.
"Sijawaona watoto wangu ni mwaka sasa. Niliwadanganya kuwa ninakwenda katika safari ya kikazi . "
Majuto yake tu, anasema, ni kuwaacha.
Aina za wateja wanaopote
" Nina aina tofauti za wateja," anasema na kuongeza kuwa "Kuna watu waliotoroka matatizo makubwa ya unyanyasaji wa kinyumbani na wengine hufanya hivyo kutokana na kiburi chao au maslahi ya kibinafsi. Siwahukumu. Siwaambii , 'Suala lako si baya kiasi cha kukufanya utengane na familia yako kwa kupotea. Kila mtu ana matatizo yake ."
Kwa watu kama Sugimoto, kampuni inamsaidia kukabiliana na matatizo yake ya kibinafsi.
Lakini hata kama anaweza kutoweka, hilo halimaanishi kwamba maisha yake ya awali hayataendelea kuwepo.
"Ni mtoto wangu wa kiume wa kwanza pekee anayefahamu ukweli. Ana umri wa miaka13 ," anasema.
"Maneno ambayo siwezi kamwe kuyasahau ni : 'Kile ambacho baba anakifanya katika maisha yeke kinamuhusu yeye binafsi , na siwezi kukibadilisha .' Anasikika kama mtu aliyekomaa zaidi kuniliko, si kweli?"