Mercy Baguma: Mwanamke aliyefariki huku mwanawe mchanga akilia Glasgow azikwa Uganda

Mercy vigil
Maelezo ya picha, Mkesha wa kumkumbuka Baguma ulifanyika katika mji wa Glasgow, Uskochi siku ya Jumapili
Iliyochapishwa

Mercy Baguma, aliyefariki nchini Uingereza ambapo alikuwa anatafuta hifadhi , amezikwa karibu na nyumbani kwao huko Uganada.

Mwezi Agosti , mwili wake ulipatikana ndani ya nyumba moja mjini Glasgow karibu na mwanawe aliyekuwa akilia.

Haijulikani Bi Baguma alifariki vipi. Lakini tukio hilo lilivutia wito wa kufanyia mabadiliko mfumo mzima wa kujtafuta hifadhi nchini Uingereza.

Shirika la PAIH ambalo lilikuwa likimsaidia , lilisema kwamba alikuwa masikini kwasababu alikuwa hawezi kupata kazi kwasababu haki yake ya kufanya kazi Uingereza ilikuwa imeisha.

Eric Nnanna, babake mwana wa Baguma mwenye umri wa mwaka mmoja Adriel aliwapigia polisi simu siku nne baada ya kupoteza mawasiliano naye.

Alikuwa na wasiwasi baada ya kusikia sauti ya mwanawe akilia ndani ya nyumba hiyo iliofungwa kwa ndani.

Mtoto alikuwa pekee kwa siku tatu

Maafisa wa polisi walifungua mlango kwa lazima na kugundua mwili wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 katika ukumbi wa nyumba hiyo huku Adrien akipatikana hai.

Kifo chake kimeelezewa na maafisa wa polisi kama kisichoelezeka na kisicho na shauku kubwa.

Inafikiriwa kwamba Adriel amekuwa pekee kwa siku tatu bila chakula , kulingana PAIH.

Shirika hilo la wahisani lilisaidia katika kuchangisha fedha ili Baguma aweze kurudishwa nyumbani pamoja na gharama za maziko yake.

Fedha zilichangishwa kumsaidia mtoto wake

Alizikwa katika eneo la Bugiri nchini Uganda , umbali wa kilomita 150 mashariki mwa mji mkuu wa Kampala.

PAIH lilisema kwamba $97,000 zilizosalia zitawekwa katika wakfu wa Adriel.

Shirika hilo limetaka uchunguzi kufanywa kuhusu kifo chake na raia wengine wanaotafuta hifadhi mjini Glasgow mbali na majumba yanayowahifadhi wanaotafuta hifadhi katika mji huo wa Uskochi.

Waziri wa kwanza nchini Uskochi Nicola Sturgeon alisema kwamba mabadiliko makubwa ya mfumo wa kutafuta hifadhi nchini humo unahitajika ili kuwasaidia 'wanadamu wenzetu'.

Wizara ya masuala ya ndani nchini Uingereza imesema kwamba itachunguza kisa cha Baguma.

Anaaminika kuwasili Uingereza kama mwanafunzi miaka 15 iliopita, kulingana na gazeti la The Guardian limeripoti.

Bwana Nnanna ambaye anatoka Nigeria , alikutana na msichana huyo aliyekuwa mrembo 2017, aliambia gazeti la Glasgow Times.