Vita vya Afghan:'Mazungumzo ya kihistoria ya amani kati ya Afghan, Talban yaanza

Iliyochapishwa

Mazungumzo ya kwanza ya amani kati ya serikali ya Afghanistani na Taliban yameanza Qatar, baada ya kucheleweshwa kwa miezi kadhaa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameuita mkutano huo kuwa wa kihistoria wakati akielekea Doha katika sherehe za ufunguzi.

Mazungumzo hayo yalipaswa kuanza baada ya Marekani na Taliban kusaini mkataba wa amani mwezi Februari.

Lakini utata ulikuja katika hatua ya kukubali kubadilishana wafungwa , wakati vurugu huko Afghanistan iliyochukua miongo minne kuwa katika kumalizika.

Ujumbe wa raia wa Afghan kuondoka Kabul kuelekea Doha ulitolewa Ijumaa - 11 Septemba, miaka 19 iliyopita shambulio baya la Marekani kutokea na kusababisha mwisho wa utawala wa Taliban.

Mkuu wa mazungumzo hayo bwana Abdullah Abdullah, alisema wanatafuta haki na amani.

Bwana Pompeo alizungumza katika mkutano kuwa anaamini kuwa Marekani italinda haki ya kila mtu nchini Afghanistan "Hii ni namna nzuri ya kusitisha ghasia na kwa manufaa ya kizazi hiki na kizazi kijacho".

Siku ya Alhamisi , Taliban ilithibitisha kuwa itahudhuria baada ya kundi la mwisho la wafungwa sita kuachiwa huru.

Katika mkutano kiongozi wa Taliban bwana Mullah Baradar Akhund ametaka Afghanistan kuwa na mfumo wa kiislamu ambao utakubalika katika jamii zote na kuwafanya watu waishi kwa upendo na kindugu.

Tutarajie nini katika mazugumzo hayo

Haya ni mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya Taliban na wawakilishi wa serikali ya Afghanistan.

Wanamgambo hao hadi sasa walikuwa wamekataa kukutana na serikali, wakiwaita dhaifu na "vibaraka" wa Marekani.

Pande mbili zinalenga upatanisho wa kisiasa na kumaliza vurugu zilizochukua miongo kadhaa.

Mazungumzo hayo yalikusudiwa kuanza Machi lakini yalicheleweshwa mara kwa mara na mzozo juu ya mabadilishano ya wafungwa yaliyokubaliwa katika makubaliano ya Februari ya Marekani na Taliban, pamoja na vurugu nchini.

Mkataba wa kihistoria uliozongwa na wasiwasi

Makubaliano hayo ya kihistoria yamekua yakiendelea kwa miaka mingi kwa sababu pande zote zimekuwa zikitafuta kunufaika.

Mkataba huo umetokana na dhamira ya Marekani ya kurejesha vikosi vyake nyumbani huku baadhi ya Wataliban wakitambua kwamba mazungumzo ndio njia nzuri ya kurejea Kabul.

Ni moja ya hatua muhimu iliyopigwa licha ya uwepo wa hali ya wasiwasi kwa kiasi kikubwa kuhusu hatma ya mkataba huo.

Wakati ambapo kile kinachoonekana kuwa mbadala ni vita visivyokuwa na mwisho, raia wengi wa Afghanistan wako tayari kuchagua amani hata kama bado hali haieleweki.

Viongozi wa Taliban wanasema kwamba wamebadilika ingawa bado utawala wao mbaya miaka ya 90 bado unakumbukwa na wengi hasa wanawake wa Afghanistan.

Mchakato huu utakuwa jaribio kwa Taliban lakini pia kwa viongozi wa nyuma waandamaizi wa Afghanistan, na kizazi kipya ambacho kimepitia mengi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na kinatarajiwa kuwa siku za baadaye zenye mabadiliko.

Historia ya vita ya Afghan ni ipi?

Vita hii ilianza wakati ambao Marekani ilianzisha mapigano ya anga mwezi mmoja baada ya shambulizi la Septemba 11, 2001 kutokea na baada ya Taliban kukataa kumsalimisha mwanaume aliyekuwa akiongoza mapigano ya kigaidi, Osama bin Laden.

Ingawa jeshi lake lilikabadilika na kuwa kikosi cha waasi na kuendeleza mashambulizi ya mauaji kila kukicha dhidi ya serikali ya Afghanstan.

Muungano wa kimataifa ulisitisha oparesheni yake mwaka 2014, na kusalia tu ukitoa mafunzo kwa wanajeshi wa rain Afghan.

Lakini Marekani iliendelea na operesheni zake ikiwemo mashambulizi ya anga.

Hata hivyo, kundi la Taliban pia limekuwa likiendeleza uwepo wake na mwaka jana BBC ilibaini kwamba lilikuwa linaendesha shuguli zake katika asilimi 70 ya maeneo ya Afghanstani.

Kwanini vita hivyo vimechukua muda mrefu?

Kuna sababu nyingi sana, lakini yanajumuisha upinzani mkali kutoka kwa taliban, uwezo wa vikosi vya Afghan na uongozi na nchi zingine kuonyesha kuendelea kuwa na vikosi vya Afghanistan kwa muda mrefu.

Katika kipindi cha miaka 18, kundi la Taliban limekuwa nyuma.

Mwishoni wa 2009, rais wa Marekani Barack Obama alitangaza kuongeza wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan na kufikia idadi kubwa zaidi ya 100,000.

Idai hiyo ilisaidia kuondoa Wataliban katika baadhi ya sehemu za kusini mwa Afghanistan, lakini haikuwa imedhamiriwa kwamba hilo litachukua muda mrefu.