Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Macron asitisha uwindaji wa ndege kwa kutumia gundi
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameagiza wawindaji Ufaransa Kusini kusitisha tabia tatanishi ya kutegesha ndege kwa kuweka gundi kwenye matawi.
Marufuku hiyo inafuata onyo kwa Ufaransa kutoka kwa Tume ya Ulaya kwamba inaweza kukabiliwa na hatua za kisheria ndani ya Umoja wa Ulaya ikiwa tabia hiyo itaendelea.
Ufaransa bado inatekeleza mbinu ya kuwinda ndege kwa kutumia gundi mbinu ambayo ilitumiwa kushika mikesha na ndege weusi.
Njia hiyo ya uwindaji inatekelezwa katika maeneo matano kote Marseille na Nice.
Uamuzi wa Rais Macron umekuja wakati yeye na Waziri wa mabadiliko ya ikolojia Barbara Pompili kukutana na mkuu wa jumuia ya wawindaji Willy Schraen, katika kasri la Élysée jijini Paris siku ya Jumatano.
Mbinu hiyo imesitishwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia, wakati maoni ya kisheria kutoka kwa Mahakama ya Haki Ulaya (ECJ) kuhusiana na sheria hii.
Wanamazingira wanasema kuwa njia hiyo ni ya kikatili, yenye kudhuru sio tu ndege waimbaji lakini pia ndege wengine.
Tume ya Ulaya Julai - ambayo inasimamia utekelezaji wa sheria hiyo - iliipa Ufaransa miezi mitatu kutatua suala hilo, na kuonya kwamba kushindwa kutimiza Sheria ya Uingiliaji wa Ndege 2009 ya Umoja wa Ulaya kunaweza kumaanisha kwamba kesi iwasilishwe kwa Mahakama ya Haki Ulaya.
Onyo la Tume limesema kwamba Ufaransa "imeidhinisha njia kadhaa za kunasa ndege, kama vile ya kutumia gundi kwa ndege aina ya mkesha, nyavu, vitego vya kunasa ndege na njiwa ambazo zimekatazwa na mahakama hiyo.
Tume hiyo imesema karibu asilimia 32 ya makundi ya ndege Ulaya sasa hivi hawako salama na Ufaransa, ambapo aina 64 zinaweza kuwindwa ni 20 tu walio salama.