Maandamano Jacob Blake: Makabiliano mapya yazuka Marekani baada ya kushambuliwa kwa Jacob Blake

Iliyochapishwa

Majumba na magari yamechomwa moto katika usiku wa pili wa maandamano kufuatia kupigwa risasi kwa mtu mweusi kwa jina Jacob Blake siku ya Jumpili.

Jacob Blake, 29, yupo katika hali nzuri baada ya kupigwa risasi mara kadhaa alipokuwa anafungua mlango kuingia ndani ya gari katika mji wa Kenosha.

Gavana Tony Evers amekitaka kikosi cha kitaifa kuwasaidia maafisa wa polisi.

Mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd huko Minnesota mwezi Mei yalisababisha maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji unaotekelezwa na polisi.

Maandamano kote nchini Marekani na miji mingi kimataifa yaliangazia jinsi Wamarekani weusi wanavyonyanyaswa na maafisa wa polisi hatua iliozua maswali mengi khusu ubaguzi katika jamii .

Kanda ya video kuhusu mauaji hayo ya Kenosha, iliochukuliwa barabarani na kusamabazwa katika mitandao ya kijamii, ilimuonesha Bwana Blake akitegemea gari huku afisa mmoja akivuta shati lake na milio ya risasi ikisikika.

Sheria ya kutotoka nje imewekwa mjini Kenosha kuanzia saa mbili usiku na itaendelea hadi saa moja alfajiri siku ya Jumanne- sheria hiyo hata hivyo imepuuzwa na waandamanaji.

Kinachoendelea mtaani

Mwanahabari wa BBC, Aleem Maqbool, Kenosha

Ilianza kama ukumbusho kwa wengi katika miji na majiji nchini Marekani baada ya kifo cha George Floyd huku mamia ya vijana mjini Kenosha wakivunja amri ya kutotembea usiku na kukabiliana na polisi waliokuwa wamejipanga nje ya mahakama.

Maandamano hapa wakati huu, yanayohusu kutaka haki kwa Jacob Blake, awali yalizuiwa na kutawanywa kwa gesi ya kutoa machozi na mabomu ya kutoa sauti, lakini watu waliendelea.

Hata hivi sasa mapema asubuhi bado wanakabiliwa na maafisa wakiwa na ngao kuwazuia waandamanaji. ''Hatuondoki'', walikuwa wakiimba.

Katika mitaa iliyokuwa ikiwazunguka tuliona magari yakiwa yamechomwa moto, majengo yakiwa yameharibiwa na taa za mitaani zikiwa zimeangushwa.

Kijana mmoja muandamanaji aliniambia. '' Nimechoka kuwa na hofu ya kuuawa na polisi. Usiku huu watatusikiliza.''

Polisi na serikali wamesema nini?

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Gavana Evers amesema ''ombi la kupata maafisa wa ulinzi ilikua ni kusaidia kusimamia sheria ''kulinda miundombinu'' na kuhakikisha kuwa watu wanaandamana kwa usalama.

Alisema kuwa anasambaza maafisa karibu 125 wa kulinda usalama Jumatatu usiku.

Mapema asubuhi baaadhi ya waandamanaji walijaribu kuingia kwenye jengo la usalama la mji wa Kenosha, wakitaka maafisa waliohusika katika tukio la kufyatua risasi wakamatwe.

Mlango ulivunjwa kabla ya maafisa kutumia dawa ya kupuliza yenye pilipili kusambaratisha kundi la watu.

Mamia ya watu pia waliandamana mpaka makao makuu ya polisi usiku wa Jumapili wakikemea tukio hilo.

Gavana Evers amekemea tukio hilo, akisema kuwa Bwana Blake hakuwa ''mtu wa kwanza kufyatuliwa risasi au kujeruhiwa au kuuawa mikononi mwa polisi.''

But the Democratic governor has faced criticism for this response.

Lakini gavana huyo amekosolewa kutokana na kauli yake, mkuu wa polisi mjini Kenosha Pete Deates, amesema kuwa kauli ya Evers ''haikuwa ya kuwajibika'' na kusema kuwa watu wanapaswa kusubiri mpaka pale ukweli utakapojulikana.

Bwana Evers pia amesema kuwa kutakuwa na kipindi maalumu kwa wabunge ifikapo tarehe 31 Agosti kujadili sheria zilizotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu uwazi na uwajibikaji wa watu baada ya kuuawa kwa George Floyd.

Wabunge walishindwa ''kuchukua hatua'' katika kipindi cha miezi miwili tangu ''mabadiliko ya sera'', gavana aliandika katika ukurasa wa twitter.

Tunachokifahamu kuhusu shambulio hilo?

Idara ya polisi imesema kuwa afisa wa polisi ''aliyehusika kwenye tukio la kufaytua risasi'' lililotokea siku ya Jumapili.

Na kuongeza kuwa maafisa ''walitoa msaada wa haraka'' kwa bwana Blake, ambaye alifikishwa hospitali mjini Milwaukee akiwa katika hali mbaya.

Katika picha ya video, maafisa watatu walionekana wakimuonesha silaha mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina Blake wakati akielekea kwenye gari aina ya SUV iliyokuwa imeegeshwa.

Alipofungua mlango na kutaka kuingia ndani, alioneka ofisa mmoja akimkamata shati na kumfyatulia risasi. Milio saba ya risasi ilisikika kwenye video hiyo huku mashuhuda wakipiga kelele.

It was then he started recording. Mr Blake is shown walking around the front of the SUV. The two officers closest to Mr Blake at this point on the video are white males.

Polisi wamesema maafisa hawajaeleza kilichosababisha hata wakafyatua risasi. Haijulikani ni nani aliwaita polisi na kilichotokea kabla ya video kuanza kurekodiwa.

Polisi mjini Kenosha hawana kamera wanazovaa ingawa wana vipaza sauti.

Mwenza wa Bw. Blake, Laquisha Booker, ameiambia chaneli ya NBC kuwa watoto watatu walikuwa nyuma ya gari hiyo wakati huo wa kufyatuliwa risasi.

Mwanasheria wa haki za raia Ben Crump, ambaye anawakilisha familia za George Floyd na wengine ambao wamechukua hatua dhidi ya polisi, ametangaza kuwa anaiwakilisha familia ya Blake.

Bwana Blake, ambaye anafanya kazi ya ulinzi sasa ametoka kwenye chumba cha upasuaji na anaendelea vizuri.

Idara ya sheria ya Wisconsin inachunguza tukio hilo mjini Kenosha, mji ullio na watu karibu 100,000 ulio Kusini-Magharibi mwa Ziwa Michigan.

Maafisa waliohusika katika tukio hilo wamepatiwa likizo wakati hatua za kiuchunguzi zikienedela.