Maandamano Belarus: Maandamano yatarajiwa huku Lukashenko akiendelea kukaidia wito wa kujiuzulu
Maandamano mapya yanatarajiwa tena Belarus baada ya maelfu ya watu kuandamana wakidai rais wa muda mrefu Alexander Lukashenko aondoke madarakani.
Viongozi wa upinzani walitoa wito wa maandamano huku hasira zikiendelea kuongezeka juu ya taarifa za polisi kutumia nguvu kupita kiasi pamoja na madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa Agosti 9.
Lakini Rais ambaye anadai alipata ushindi wa kishindo bado anakaidi wito wa kijiuzulu.
Jumapili, alitoa wito kwa wafuasi wake kutetea nchi yao na uhuru wao.
Hata hivyo, waandamanaji walijitokeza kwa wingi huku wenyeji, kulingana na tovuti ya habari inayojitegemea ya -Tut.by, ikisema kwamba maandamano hayo ndio makubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya Belarus".
Ghadhabu imekuwa ikiongezeka tangu Tume ya uchaguzi iliposema kuwa Bwana Lukashenko, ambaye amekuwa madarakani tangu 1994, ameshinda uchaguzi kwa asilimia 80.1 ya kura zote zilizopigwa huku kiongozi wa chama kikuu cha upindani Svetlana Tikhanovskaya akijinyakulia asilimia 10.12 ya kura zilizopigwa.

Bi.Tikhanovskaya, ambaye aitorokea Lithuania baada ya kukataa matokeo hadharani, anasisitiza kwamba maeneo ambapo kura zilihesabiwa vizuri alishinda kwa kati ya 60 na 70.
Katika ujumbe kwa njia ya video Jumatatu, alisema kwamba yuko tayari kuwa kiongozi wa taifa ili kurejesha amani na hali ya kawaida, kuachilia wafungwa wa kisiasa na kujitayarisha kwa uchaguzi mpya.
Wakati huohuo, baadhi ya watu 6,700 wamekamatwa tangu kuanza kwa maandamano, na wengi wamezungumzia mateso waliopitia mikononi mwa maafisa wa usalama.
Wafanyakazi wa umma wameshiriki mgomo Jumatatu huku chombo cha habari kikionesha chumba cha kusomea habari bila wafanyakazi.

Wiki jana, wafanyakazi katika makampuni yanayoendeshwa na serikali waliungana na waandamanaji wengine huku maandamano zaidi yakipangwa kufanyika wiki hii, kama njia moja wapo ya kuongeza shinikizo kwa Bwana Lukashenko, amesema mwanahabari wa BBC, Kiev correspondent, Jonah Fisher.

Chanzo cha picha, Reuters
Nini kimetokea Jumapili?
Mikutano ya upinzani ilifanyika katika mji mkuu huku vyombo vya habari vya eneo vikisema kwamba karibu watu 31,000 walishiriki kwenye mkutano wa kuunga mkono serikali. Waziri wa mambo ya ndani anakadiria kwamba idadi hiyo ilikuwa karibu 65,000 huku mwanahabari wa shirika la habari la AFP akisema idadi hiyo ilikuwa karibu 10,000.
Alizungumza na wafuasi wake, Bwana Lukashenko amesema Belarus "itakufa kama taifa" ikiwa uchaguzi utarejelewa tena.
"Mumekuja hapa ili kwa mara ya kwanza tangu kipindi cha robo karne mutete nchi yenu, uhuru wenu, wake zenu, dada zenu na watoto wenu," amesema.

Chanzo cha picha, Reuters
Aliongeza kwamba upinzani unaweza "kutambaa kama panya anavyopita haraka kwenye shimo"
Kulikuwa na taarifa kwamba wafanyakazi wa umma wanalazimishwa kuhudhuria mkutano huo ama wakabiliana na hatari ya kupoteza ajira.
Kwa siku kadhaa, wafanyakazi wa umma wamekuwa wakiungana na wafanyakazi wengine wanaoandamana kumpinga rais.
Wakati rais anazungumza, karibu watu 220,000 walikuwa wamekusanyika kumpinga rais karibu na eneo la kumbukumbu ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, kulingana na tovuti ya habari ya Tut.by.
Baada ya wito uliotolewa wikendi na Bi. Tikhanovskaya wa kuandamana kuna maafisa wa sasa wa polisi na wale wa zamani ambao wamejiuzulu.

Chanzo cha picha, Reuters
Balozi wa Belarus nchini Slovakia, Igor Leshchenya, ametangaza kuunga mkono waandamanaji lakini akaeleza BBC kwamba serikali imeonekana kutokuwa tayari kumsikiliza.
Jumamosi, alisema Rais Vladimir Putin alikuwa ameahidi kile alichokiita usaidizi thabiti iwapo nchi hiyo itakumbana na tishio la kijeshi kutoka nje ya nchi.
Viongozi hao wawili walifanya tena mazungumzo Jumapili ambapo Urusi ilisema wamezungumza kuhusu hali ilivyo Belarus na kutilia maanani shinikizo kutoka nje kwa nchi hiyo.
Bwana Putin alimwambia Bwana Lukashenko Urusi iko tayari kuisaidia Belarus kwa misingi ya muungano wa kijeshi ikiwa kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.
Kiongozi wa Belarus pia alizungumzia wasiwasi wake juu ya kile kinachoendelezwa na wanajeshi wa Nato katika nchi jirani za Poland na Lithuania.













