Virusi vya Corona: Rais wa Urusi anavyokejeliwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya chanjo yake

A woman in a facemask is injected with a vaccine by a medical professional in full PPE and a visor

Chanzo cha picha, Sechenov Medical University Press Office

Maelezo ya picha, Watu wanajitolea kote duniani kufanyiwa majaribio ya chanjo za virusi vya corona, ikiwa ni pamoja na Urusi
Iliyochapishwa

Tangazo kwamba inaanza kutumia chanjo yake iliyotengenezwa nchini humo ya virusi vya Covid-19, si kwamba taarifa hiyo ilisababisha hofu ya kimataifa juu ya usalama wake tu, bali imeibua kiwango kikubwa cha kimataifa cha taarifa potofu na mzaha au kejeli kwenye jukwaa la mitandao ya habari ya kijamii.

Tumekuwa tukiangalia baadhi ya jumbe ambazo zimesambazwa kwa sana kwenye mitandao hii

Putin shujaa mbwa 'superhero'

Kumekua na picha nyingi za kejeli juu ya tangazo la Urusi , ambazo zimesambazwa kwa lugha mbali mbali . Baadhi zinamuonesha jinsi rais wa Urusi alivyo shujaa , sawa na vibonzo vya Spiderman au Ironman, akiokoa dunia.

Picha ambayo imekua maarufu kwa kushirikishwa inamuonesha Bwana Putin akiendesha dubu huku akiwa na sindano kubwa mgongoni mwake.

Sehemu ya picha hii ya kejeli, inadailwa kuwa Putin mwenyewe ndiye aliyeishirikisha kwa umma, madai ambayo sio sahihi.

An image of Vladimir Putin superimposed onto a bear with a large syringe slung on his back
Maelezo ya picha, Picha nyingi za kejeli zimekuwa zikimuonesha Putin kama shujaa mkuu 'superhero'

Ujumbe mwingine ulioshirikishwa sana kwenye mitandao ya kijamii ni ule wakusherehekea tangazo la chanjo ya Urusi uliotumwa kwenye ukurasa wa Facebook ikimuunga mkono Bwana Putin, na umeshirikishwa kwa watu zaidi ya mara 200,000

Sio ukurasa rasmi wa rais wa Urusi, ambaye anaaminiwa kuiepuka mitandao ya kijamii.

Lakini wengi miongoni mwa maelfu ya watu walioandika maoni yao kwenye ujumbe huo kwa lugha mbalimbali ni wazi wanaamini kuwa ujumbe huo ni wa Bwana Putin.

A post from a President Putin fan page on Facebook with the message: "Once the Soviet satellite paved the way for humanity into space, now the Russian vaccine will pave the way to the future without Covid-19, masks and social isolation." Labelled "no evidence"
Maelezo ya picha, Ujumbe hu sio hautoki kwa rais wa Urusi

Ujumbe huu uliosambaa sana unalinganisha setilaiti ya kwanza ya Usovieti ambayo "ilitoa fursa kwa binadamu kwenda katik aanga za mbali " huku chanjo ya Urusi ambayo "itafungua njia ya hali ya baadae bila Covid-19, barakoa na watu kutokaribiana ."

Kuongezeka kwa hofu ya kimataifa kwamba huenda usalama wa chanjo hiyo haukuzingatiwa katika kuitengeneza kumelifanya Shirika la afya duniani WHO kuitaka Urusi ifuate miongozo ya kimataifa juu ya utengenezaji na uidhinishwaji wa chanjo

Heshima iliyotiwa chumvi

Ujumbe mwingine ambao pia ulithihirika kuwa maarufu kwenye ukurasa wa Facebook unadai kuwa Urusi "imeinusuru mara mbili dunia na chanjo zake ".

Screenshot of a post on Facebook that says: "Russia has repeatedly saved the world with its vaccines - it was in Russia where vaccines against cholera, polio, diphtheria, whooping cough, measles and other dangerous diseases were invented." We labelled "misleading"

"THuu ni utiwaji wa chumvi wa kauli kupita kiasi " anasema Dkt Dora Vargha, mwanahistoria na mtaalamu wa udhibiti wa magonjwa ya enzi ya vita baridi vya dunia.

Ujumbe unaonyesha orodha ya chanjo kadhaa ambazo "ziligunduliwa " nchini Urusi, miongoni mwake zikiwa ni zile za kipindupindu na kupooza.

Ukweli ni kwamba ni mwanasayansi Mfaransa Louis Pasteur ambaye alivumbua chanjo ya kwanza ya kipindupindu- kutokana na aina ya ugonjwa huo ambao uliwaathiri kuku.

Baadae mwaka 1985, Jaime Ferran, daktari Muhispania, alitengeneza chanjo ambayo binadamu alichanjwa dhidi ya kipindupindu kwa mara ya kwanza.

Mtaalamu wa virusi mmarekani Dkt Jonas Salk, alitengeneza chanjo yenye ufanisi dhidi ya ugonjwa wa kupooza-polio -mwaka 1955.

Hii ilifuatiwa muda mfupi na mafanikio mengine ya enzi ya Vita baridi ya dunia -chanjo ya kwanza inayomezwa ya kupooza , ambayo bado inatumiwa kutokomeza ugonjwa huo leo kote duniani.

Imekuwa ikielezewa kama chanjo iliyotengenezwa na Mmarekani na Mrusi, au Usovieti

Dkt Vargha anasema chanjo hiyo inapaswa kuangaliwa kama matokeo ya juhudi za pamoja kati ya Dkt Albert Sabin, Mmarekani, Mikhail Chumakov, mwanasayansi Mrusi.

Taarifa ya Chanjo ya corona ilivyoripotiwa ndani kwenyewe Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kwamba chanjo iliyotengenezwa ndani ya Urusi kwa ajili ya ugonjwa wa Covid-19 imeidhinishwa kwa matumizi baada ya kufanyiwa majaribio kwa binadamu chini ya miezi miwili.

Bwana Putin amesema kwamba chanjo hiyo imepita vigezo vyote vilivyowekwa na kuongeza kwamba binti yake tayari amepatiwa

.Chanjo ya Covid-19 imeidhinishwa Urusi

Maafisa walisema kuwa mpango wa kuanza kutoa chanjo hiyo kwa umma kuanzia Oktoba.

Akiitaja chanjo hiyo kuwa ya kwanza Duniani, Rais Putin alisemaa chanjo iliyotengenezwa na taasisi ya Moscow ya Gamaleya, inatoa "kinga endelevu" dhidi ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya Mikhail Murashko alisema chanjo hiyo imethibitisha kuwa salama na yenye ufanisi", na kupongeza kwamba ni hatua kubwa kuelekea ushindi kwa mwanadamu dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Ukosoaji wa duka kubwa la dawa

Ujumbe wa Kiitalia unadaiwa kuwa chanzo chake kilikuwa ni nukuu tata kwa rais Putin , lakini haunekani kuwa ulitumwa kokote kule, hata vyombo vya habari vya Urusi.

, Picha ambayo imekuwa ikipendwa ama kuwa na 'likes' ulizungumziwa na kushirikishwa zaidi ya mara 35,000 kwenye Facebook ukisema : "Makampuni ya madawa yametuomba kuchelewesha utoaji wa chanjo! Sio kuhusu uchumi. Urusi haifikirii juu ya pesa inapokuja katika suala la maisha ya mamilioni ya watu ."

Fake quote attributed to President Putin in Italian saying: "Pharmaceutical companies have asked us to delay the release of the vaccine! It's not about economics. Russia does not think about money when it comes to the lives of millions of people"
Maelezo ya picha, Taarifa hii sio sahihi

Nukuu hiyo huenda ikawa imetafsiriwa kimakosa kutoka kwa ukurasa sawa wa mashabiki wa Putin ambao tuliutazama awali . Ujumbe ulikua na ukosoaji sawa na huu dhidi ya makampuni ya dawa na sifa kwa maadili ya Urusi . Hatahivyo, kama ilivyokwisha kubainika, akaunti hii ya mashabiki sio ya Putin, na hajanukuliwa kokote kule akitoa kauli hizi.

Jumbe zote zinaonyesha ukosoaji wa mipango ya Urusi ya kuidhinisha mapema chanjo kwasababu makampuni ya madawa yana njaa ya kupata faida.

Hii inapuuza hofu kubwa za wanasayansi walizonazo juu ya hatua ya Urusi kuidhinisha mapema chanjo , ambayo haijatangaza matokeo ya utafiti wake juu ya chanjo hiyo hadi sasa, mkiwemo data juu ya usalama wake.

A post claiming that the woman in the video getting the Russian-made vaccine is Putin's daughter. We labelled this "false"

Jumbe nyingine zimeamua kumzungumzia mwana wa kike wa Rais Putin, ambaye alisema alipokea chanjo hiyo.

Bana Putin hakumtaja ni nani miongoni mwa watoto wake wa kike aliyepewa chanjo hiyo , lakini alisema athari moja tu aliyopata ni kupanda kidogo kwa joto la mwili kwa muda mfupi.

Video imekua ikisambaa nchini India sambamba na madai kuwa video hiyo inamuonesha mtoto wa kike wa Putin ambaye alipokea chanjo hiyo.

Ukweli ni kwamba picha hii ni ya mmoja wa washiriki wa jaribio la chanjo , lakini amekuwa akitambuliwa na vyombo vya habari vya Urusi kama mwanafunzi wa chuo cha mafunzo ya udaktari cha kijeshi cha Urusi na sio binti yake Bwana .

Coronavirus