Mlipuko Beirut: Kwanini meli iliowasili na Amonium Nitrate ilikuwa na Bendera ya Moldova?

Barco con bandera de Moldavia

Chanzo cha picha, EPA/TONY VRAILAS

Maelezo ya picha, 2013, meli ya Moldovan iliyokuwa imebeba kemikali ya ammonium nitrate iliwasili bandari ya Beirut.
Iliyochapishwa

Tani 2,750 za Ammonium nitrate zimetambuliwa kama chanzo cha mlipuko wa Beirut, mji mkuu wa Lebanon, ambao uliiwaacha watu 137,000 wakiwa wamefariki na wengine 5000 wakiwa wamejeruhiwa.

Ni kiwango hicho cha kemikali ya Ammonium Nitrate ambacho kilisafirishwa na meli ya MV Rhosus ambayo 2013 iliwasili na matatizo ya kiufundi katika bandari ya Beirut.

Ni Wakati huo ambao kemikali hiyo hatari ilichukuliwa na serikali ya Beirut.

Ilikuwa meli iliokodishwa na Urusi iliokuwa na bendera ya Moldova.

Na kwanini Moldova iwapo ni taifa ambalo halina pwani ya bahari?.

Taifa hili la Ulaya ni miongoni mwa mataifa yanayodaiwa kukodisha bendera yake katika bahari kuu, ikiitwa bendera ya kujisadidia.

Hivyobasi imeelezwa kwamba Moldova, taifa ambalo halina pwani lina ishara katika bendera yake zinazofanya kazi katika bahari tofauti.

Kulingana na Shirika la uchukuzi wa kimataifa, ni kitendo kinachofanywa na mataifa kama vile, Bahamas, Bolivia, Kisiwa cha Cayman na Lebanon yenyewe huku Panama ikiwa mshirika wake mkuu.

Un buque carguero con una bandera de Panamá

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meli nyingi za mizigo zimesajiliwa Panama.

Ni jambo ambalo limekuwepo sana kwa meli kusajiliwa na kupatiwa bendera za nchi ambayo sio ya mmiliki wake.

Kwanini meli nyingi zina bendera za Panama?

Kwa kila meli ya kubeba mizigo lazima isajiliwe na taifa ambalo linajulikana kama nchi yenye bendera. Panama, visiwa vya Marshal na Liberia ndio mataifa yenye bendera.

Takriban meli 8,600 hupeperusha bendera za Panama. Kwa kutofautisha, Marekani ina takriban meli 3,400 zilizosajiliwa huku China ikiwa na 3,700.

Meli nyingi ambazo hupeperusha bendera humilikiwa na wageni ambao hupendelea kuzuia masharti yaliowekwa na mataifa yao. Panama hutoa usajili wa wazi.

Bendera zao hutoa fursa ya usajili wa rahisi katika mtandao na uwezo wa kuwaajiri wafanyakazi wanaolipwa mishahara ya chini. Pia wamiliki wa kigeni hawalipi kodi.

''Masharti hayo ni pamoja na kodi na huduma inayotolewa'', alisema mtaalamu wa usalama Ioannis Chapsos. Matafiti huyo anasema kwamba Ugiriki ndio mmiliki mkuu wa meli duniani.

Meli zao nyingi hazina bendera za Ugiriki, kwasababu utawala utalazimika kulipa kodi zaidi.

Kutokana na hilo, mataifa yenye bendera - hususan mataifa yenye mtataizo ya kiuchumi - hujipatia fedha nyingi.

Kulingana na shirikisho la kimataifa kuhusu wafanyakazi wa uchukuzi, usajili uliopo chini ya bedera ya kigeni hufanya kuwa vigumu kuwawajibisha wamiliki wa meli hizo kuhusu mgogoro wa mishahara au masharti ya kufanyia kazi.

Hivyobasi tunauliza ni nani wa kulaumiwa?

Baada ya kusajiliwa na bendera, sheria ya taifa hilo ndio inatumika katika meli hiyo , na kila taifa linawajibika kutokana na meli inayotumia bendera yake.

Hii ni pamoja na kuhakikisha kwamba meli zinaafikia viwango vya kimataifa, kupitia ukaguzi wa meli, na kutoa vyeti vya kufanyia kazi, kulingana na shirika la masuala ya baharini duniani IMO, linalomilikiwa na Umoja wa Mataifa.

Kulingana na azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu sheria za baharini, Mataifa yanayomiliki bendera yanapaswa kuchukua sheria kuhakikisha kuwa kuna usalama baharini. Liberia kwa mfano husimamiwa na makampuni ya Marekani yaliopo mjini Washington, DC .

Una bandera de navegación de Bahamas en un buque

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sheria za nchi husika hutekelezwa kwa meli inayopeperusha bendera yake

Sio rahisi kwa taifa linalomiki bendera kutoa usalama kwa meli zote zilizosajiliwa chini yake, kulingana na Chapsos. Na ni vigumu zaidi kwa taifa lenye raslimali chache.