Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mlipuko mkubwa watokea mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kusababisha madhara makubwa
Mlipuko mkubwa umepiga mji mkuu wa Lebanon, Beirut, huku kukiwa hakuna uthibitisho kuhusu mlipuko wa pili
Mlipuko mkubwa umetokea mjini Beirut wakati kukitarajiwa uamuzi kuhusu kesi ya mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani Rafik Hariri mwaka 2005.
Ripoti zinasema kuwa mlipuko mkubwa umetokea kwenye eneo la bandari la mji huo, huku kukiwa hakuna ripoti za kutokea kwa mlipuko wa pili. Mamlaka zinahofu kutokea kwa madhara makubwa.
Video iliyowekwa mtandaoni imeonesha uharibifu mkubwa uliotokana na mlipuko huo.
Mahakama ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya washukiwa wanne wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya bwana Hariri.
Wafuasi wote wanne wa kundi la Hezbollah, wamekuwa wakikana kuhusika na kifo cha Hariri. Uamuzi wa mahakama utatolewa siku ya Ijumaa
Ripoti kuhusu uwezekano wa kutokea mlipuko wa pili katika makazi ya bwana Hariri imetolewa.
Waziri wa afya wa Lebanon Hamad Hasan amezungumzia kuhusu majeruhi wengi na uharibifu mkubwa uliojitokeza.
Shirika la habari la Reuters limenukuu vyanzo vya habari vikisema miili kumi imetolewa kutoka kwenye kifusi.
Vyombo vya habari nchini humo vieonesha watu wakiwa wamenasa kwenye vifusi. Shuhuda akieleza jinsi mlipuko huo wa kwanza ulivyokuwa wa kishindo na sauti kubwa.
Sababu ya mlipuko huo bado haijafahamika.
Ripoti hii imekuja wakati kukiwa na mvutano wa kisiasa nchiniLebanon, huku maandamano yakitokea mitaani dhidi ya serikali kuhusu namna wanavyoshughulikia changamoto za kiuchumi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1975-1990.