'Familia yangu Tanzania imegawanyika sababu ni virusi vya corona'

Church members measure the body temperature of believers during a Palm Sunday mass at the Full Gospel Bible Fellowship Church in Dar es Salaam, Tanzania, on April 5, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Sammy Awami
    • Nafasi, BBC News, Dar es Salaam
  • Iliyochapishwa

Mwanahabari wa BBC Sammy Awami ameandika kwamba mbinu ya rais Magufuli ya kukabiliana na virusi vya corona inayoegemea imani imesababisha wasiwasi katika familia yake.

Tangu kutangazwa kwa mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya corona nchini Tanzania mnamo mwezi Machi, nimekuwa nikipokea ujumbe mwingi tu, watu kunipigia simu kuanzia wafanyakazi wenzangu, marafiki na hata familia wanaoishi nje ya nchi.

Wamekuwa na maswali mengi: Vipi kwa nchi iliolegeza baadhi ya masharti yake kwa kiasi kikubwa Afrika, hadi kufikia sasa imefanikiwa kukwepa kuathirika vibaya na janga hilo ambalo limekumba nchi nyingi duniani.

Ni swali ambali bado linashangaza wengi hata sisi ambao tunaishi nchini humo.

Rais Magufuli alikuwa miongoni mwa viongozi wachache waliokataa kuchukua hatua ya kufunga kabisa shughuli za nchi na kushutumu kile ambacho amekuwa akikitaja kama hofu isiyo na msingi wowote kwa nchi zingine.

Vendors clean tomatoes on Mabibo Street without without wearing masks despite the confirmed COVID-19 coronavirus cases in Dar es Salaam, Tanzania, on April 16, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais John Magufuli alihofia kwamba umaskini ungeongezeka ikiwa shughuli zingefungwa

Lakini licha ya kwamba wakosoaji wake wale walio na wasiwasi mkubwa kuhofia kwamba uamuzi huo ulikuwa mbaya, hadi kufikia sasa nchi hiyo inaonekana imefanikiwa kukabiliana na idadi kubwa ya vifo jambo ambalo lilikuwa linatarajiwa na wengi.

Lakini kile kinachokanganya zaidi ni kwamba hakuna anaejua hili limefanikiwa vipi.

'Maombi ni tiba ya uhakika'

Moja ya kile kinachoendelea ni kwamba hakuna takwimu rasmi zilizotolewa ambazo mtu anaweza kuzitumia kutathimini hali.

Rais Magufuli aliamua kuwa data ndiyo itakosekana badala ya watu kutekeleza hatua ya kusalia ndani.

Mchambuzi Aidan Eyakuze amesema: "Aliweka rasmi nchi hiyo kutekeleza majukumu yake bila ya takwimu."

Madaktari watatu niliozungumza nao ambao hawakutaka kutajwa, walisema kuwa hospitali ziko sawa yaani hazijaanza kushuhudia wagonjwa kupita kiasi.

Wengine watasema kuwa wanaunga mkono serikali kwasababu ya hofu ya kile kitakachotokea iwapo watazungumza.

Rais wa Chama cha Matibabu Tanzania, Dr Elisha Osati, amesema kwamba hakujawahi kuwa na chochote kinachofichwa, lakini sasa anataka kuwania ubunge kupitia chama tawala cha Mapinduzi.

Katika hali ambapo serikali haitoi idadi yake rasmi na wanahabari hawawezi kufikia vituo vya hospitali kufanya uchunguzi wao binafsi ulio huru, ni suala la anachosema daktari dhidi ya wenye mashaka.

Presentational grey line

Pia unaweza kusoma:

Presentational grey line

Huku baadhi ya maafisa wa afya serikalini wakionya umma kwamba virusi hivyo ni hatari na kuwataka kufuata miongozo ya usafi, rais anahamasisha watu kuendelea na shughuli zao na kumuomba Mungu awalinde.

Kama muumini mwenye imani kubwa ya Kikatoliki, aliambia waumini waliokuwa wamekusanyika, maombi ndio chanzo cha uponyaji na kuwa "ugonjwa huo umetokomezwa asante kwa Mungu".

Msimamo wa Rais ulifanya mambo kuwa magumu zaidi kati yangu mimi na familia yangu.

Jamaa zangu wengi ni wafuasi wakubwa wa rais na wote ni waumini wa Kikiristo wa kufa kupona.

'WhatsApp kuwa uwanja wa mapigano'

Kuanzia mwanzo wa mlipuko huo, pale idadi ya wanaopata maambukizi ilipoanza kuongezeka kila siku, nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu usalama wao.

Lakini suala la virusi vya corona lililoingizwa siasa, limefanya iwe vigumu kushawishi baadhi ya wapendwa wangu kwamba wanahitajika kuchukua tahadhari.

Familia katika makundi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp yamekuwa uwanja wa mapigano.

Kundi hilo lilikuwa limejaa wengi wanaomuunga mkono rais na kilichosheheni ni kile kilichoonekana kama kuwasihi watu kutochukua hatua na kuwa na matumani.

Pia walikuwa na wasiwasi kuhusu kupotea kwa ajira zao kunakoweza kutokea ikiwa shughuli zitafungwa.

Na wakati tunaendelea kufahamu kuhusu hatua za kutisha zinazochukuliwa na maafisa polisi katika nchi jirani ili kuhakikisha kwamba raia wanatekeleza masharti yaliyowekwa, hali ilikuwa tofauti.

Kwa mfano, wajomba zangu watatu, ambao wote ni wahubiri.

Kwao, huduma ya kanisa sio kwamba ni jukumu lao la kiimani na kijamii tu, pia ni chanzo chao kikuu cha ajira.

Pia unaweza kusoma:

Coronavirus
Presentational white space

'Nilijitahidi kuelimisha jamaa ambao ni wakubwa kiumri'

Wazazi wangu wanaendesha duka katika mji mkuu wa Dodoma.

Hicho ndio chanzo chao kikuu cha ajira na eneo ambalo hukutana na majirani zao na marafiki kila siku.

Lakini kwasababu umri wao ni mkubwa nilikuwa na wasiwasi kwamba shughuli zao za kila siku zinaweza kuwaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Sammy Awami's parents at their store

Chanzo cha picha, Sammy Awami

Maelezo ya picha, Wazazi wa Sammy Awami wanachukulia eneo lao la biashara kama sehemu ya kukutana na wengine

Kwa hiyo nikaamua kuunda kundi katika mtandao wa WhatsApp na kujumuisha jamaa wangu wenye umri mkubwa ili kujaribu kuwaelimisha kuhusu janga hili, na kuwashawishi kusalia majumbani.

Tofauti na watu wanaoishi katika nchi zingine, wao wanaweza kuchagua wanachotaka.

Je watanisikiliza mimi na kusali nyumbani huku wakipoteza ajira zao? Au watafuata ushauri wa rais wa kuendelea na shughuli zao na kuomba Mola kuwanusuru?

'Kutafuta adui'

Bila shaka wanaamini kwamba virusi hivyo ni vibaya mno. Lakini pia wanaamini maombi - pengine hata zaidi pale ambapo ajira zao zinakuwa hatarini.

Katika nchi ambayo kila mmoja anajishirikisha na dini moja au nyingine, na watu wengi wanafayakazi ili kuweza kukimu mahitaji yao ya kila siku, rais aliimarisha upande wa imani na kupata ajira ili kuendeleza mkakati wake.

Rais, pia alihakikisha kuwa ana adui mpya katika vita vya kukabiliana na janga hili - nchi za Magharibi.

Kila wakati alikuwa akichukulia nchi za Magharibi kama "mabeberu".

Neno lililotumika wakati wa kupigania uhuru ambalo lina maanisha wakoloni. Hili linaendana vizuri na kizazi ambacho sasa hivi ni watu wakubwa kama wazazi wangu na wajomba zangu.

Bwana Magufuli alidai kwamba "mabeberu" na rafiki zao nchini humo wanataka kutumia virusi kama sababu ya kuyumbisha nchi ili isifikie malengo yake ya kiuchumi

Katika moja ya hotuba zake huria alisema kwamba hata inawezekana watu wa nchi za Magharibi wakapanda virusi hivyo katika bidhaa zinazoingizwa kutoka nje almuradi tu wanawadhuru Watanzania.

A Tanzanian woman carries a basket on her head as she walks in front of a graffiti painted by the Wachata artists group to raise awareness about wearing masks to avoid the risk of Covid-19 in Dar es Salaam on26 May 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raia wa Tanzania wameshauriwa kufuata miongozi ya msingi ya usafi

Rais alirejelea enzi za ugonjwa wa surua yaani ukambi na miaka ya awali ya virusi vya ukimwi, na kukumbusha watu wakati ambapo baadhi ya wazazi walikataza watoto wao kutofika kwa majirani kwa hofu ya kuwa vijana wao na binti zao wataambukizwa.

Hadi kufikia sasa sera ya serikali inaonekana kana kwamba: "Ikiwa hakuna anayedondosha mtu wake aliyekufa barabarani basi maisha yaendelee kama kawaida."

Ni mkakati hatari, lakini ambao wengi hapa wako tayari kuukubali, na kuomba serikali iwe imeshika njia stahiki.

Pia unaweza kutazama:

Maelezo ya video, Virusi vya corona: Dereva bajaji wanaotoa mafunzo ya Corona nchini Tanzania