Kwa nini mashine ya kupashia chakula kwa jina microwave sio salama kupikia chakula

microwave

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Licha ya kuwa punda jikoni kwa miongo kadhaa, ni vifaa vichache vya nyumbani vilivyo na usaidizi mkubwa zaidi ya mashine ya kupashia chakula Microwave.

Wale wasioweza kupika ama wasiotaka kupika huichukulika kama mkombozi , huku baadhi ya wapishi wakisema kwamba ina uwezo wa kumaliza sanaa ya upishi.

Hatahivyo kuna mjadala mwengine zaidi ya mzozo uliopo kuhusu mashine hi: Ni wakati gani upishi wa microwave sio salama kwama afya yako?.

Inapotumika vyema hakuna la kukutia wasiwasi kuhusu mionzi inayotumika kupasha moto chakula hicho, kulingana na shirika la afya duniani WHO.

Je ni kweli kwamba chakula hupoteza virutubisho ndani ya Microwave?

Lakini jibu la hofu kuhusu utumizi wa mashine hiyo kupika sio la moja kwa moja, Ikiwemo iwapo chakula kinachopikwa na microwave hupoteza virutubishi ama kupasha chakula kilichopo ndani ya chombo cha plastiki kunaweza kudhuru afya yetu.

Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba mimea hupoteza thamani ya virutubisho vyake ndani ya mashine ya microwave.

Kupotea ama kuongezeka kwa thamani ya virutubishi katika chakula kunategemea muda wa upishi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kupotea ama kuongezeka kwa thamani ya virutubishi katika chakula kunategemea muda wa upishi.

Kupotea ama kuongezeka kwa thamani ya virutubishi katika chakula kunategemea muda wa upishi.

Hatahivyo utafiti wa mwaka 2019 uliochunguza virutubishi katika broccoli ndani ya microwave ulibaini kwama tafiti za awali zilitofautiana kuhusu muda, kiwango cha joto na iwapo broccoli hiyo ilikuwa ndani ya maji.

Utafiti ulibaini kwamba upishi wa muda mfupi wa broccoli kwa kutumia mashine ya microwave kwa dakika moja haupunguzi virutubishi vyake.

Upishi wa kutumia mvuke ama ule wa kutumia microwave unaweza kuongeza virutubishi katika flavonoids, ambavyo ni viungo vinavyohusishwa na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Chini ya masharti ya upishi yaliotumika katika utafiti huu , upishi wa microwave ulionekana kuwa mzuri katika kuhifadhi Flavonoids ikilinganishwa na upishi wa kutumia mvuke, watafiti hao waliandika.

Pia walibaini kwamba upishi wa kutumia maji mengi ndani ya Microwave hupunguza viungo hivyo muhimu.

Virutubisho hupungua kwa kutumia mbinu moja na kuongezeka kwa kutumia mbinu nyengine.

Xianli Wu, mchunguzi mkuu na mwanasayansi katika idara ya kilimo katika kituo cha utafiti wa virutubisho cha Beltsville, anasema kwamba hakuna makubaliano kuhusu mpango wa kuelezea kwa nini upishi wa kutumia microwave unaweza kuongeza viungo ambavyo vinaboresha kinga mwilini.

Huku Vyakula vingine vikiongezwa virutubishi na microwave vingine haiongezewi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Huku Vyakula vingine vikiongezwa virutubishi na microwave vingine haiongezewi.

Lakini hakuna jibu la rahisi iwapo mboga zilizopikwa na microwave zitahifadhi virutubishi vingi zaidi ya mbinu nyengine inayotumika. Hii ni kwasababu kila chakula kina viwango cha virutubishi tofauti, kulingana na Wu.

Ijapokuwa mashine hiyo uhitajika pakubwa, muda unaotumika ni tofauti kwa kila aina ya mboga.

Mvuke katika vyombo vya plastiki

Mara nyingi chakula kinachopikwa ndani ya microwave huwa kipo ndani ya chombo cha plastiki lakini wanasayansi wanaonya kuhusu kula kemikali hatari zinazotokana na platiki hizo.

Zinapokolea moto , kemikali za plastiki hizo huyeyuka na kuingia katika chakula.

Baadhi ya plastiki hazitakiwi kuingizwa katika microwave kwasababu humikliki kemikali zinazoyeyuka ndani ya mashine hiyo na kuingia katika chakula kwenye nyuzi joto zaidi ya 100 kulingana na Juminga Tang , Profesa wa uhandisi wa chakula katika chuo kikuu cha Washington nchini Marekani.

Plastiki nyingi hutuo kemikali kwa jina Phthalates zinapotumika kupasha moto chakula ndani ya microwave

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika utafiti uliofanywa 2011, watafiti walinunua zaidi ya vyombo 400 vya plastiki vya kuweka chakula na kubaini kwamba kemikali nyingi zinazopotea hudhuru hormoni ndani ya mwili wa binadamu.

Mfumo wa Hormoni

Kemikali zinazoongezwa katika plastiki ili kuzifanya kuweza kujipinda hupatikana katika vyombo vya plastiki na chupa za maji.

Kemikali hizo zimebainika kuingilia homoni na mfumo wa chakula.

Zinapoingia mwilini kemikali hizi husababisha pumu na tatizo la kushika mimba. Vilevile kemikali hizo huathiri utendakazi wa homoni ambazo ni muhimu katika utengenezaji wa ubongo wa mtoto.

kemikali ya Phthalates huwekwa katika plastiki ili kuweza kukunjika

Chanzo cha picha, Getty Images

Hatari za mvuke

Inawezekana kwamba hupendelei kutumia vyombo vya plastiki katika microwave , lakini bado kuna hatari kubwa ya kutumia vyakula vinavyopikwa na microwave, ikiwemo kutotapakaa kwa mvuke huo katika chakula kitakachopikwa .

Kwanza tumia microwave kwa kupasha chakula moto badala ya kupikia, kwasababu inapika huku upande mmoja wa chakula ukikosa moto.

Kuna maeneo mengine ambyo yatakuwa moto zaidi ya mengine, anaelezea Frascisco Gonzalez , profesa wa usalama wa chakula katika chuo kikuu cha georgia, USA.

Chakula hupashwa mara moja katika microwave

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chakula hupashwa mara moja katika microwave

Vilevile kupasha chakula moto pia ni hatari. chakula kinapaswa kupashwa moto wenye nyuzi joto za 82ºC kila mahali ili kuweza kuua bakteria hatari, na kwasababu bakteria hukuwa kila mara chakula kinapopoa haufai kupasha chakula zaidi ya mara moja.

Viwango vya juu vya joto ndani ya microwave pia husababisha hatari. Kwa jumla , viwango vya joto sio tatizo lakini baadhi ya tafiti zinasema kwamba kuna hatari inayohusishwa na kupasha moto kwa kutumia microwave vyakula vya stachi ikiwemo nafaka na vile vinavyokuzwa katika mizizi.

Viwango vya juu vya joto katika microwave husababisha kemikali kwa jina acrylamides ambazo hupatikana mara nyingi wakati mtu anapopika viazi.

Hali hiyo huzua hofu kwasababu katika utafiti uliofanyiwa wanyama , kemikali hiyo hudaiwa kudhuru utendekazi wa seli za jeni.

Hakuna ushahidi kama huo katika binadamu. Kuna utafiti unaosema kwamba microwave husababisha kemikali hiyo zaidi ya mbinu nyengine yoyote ya kupikia.

Katika kiwango cha nyuzi joto 100 ° C, kuna nguvu ya kutosha kubadilisha muundo wa moja kwa moja kati ya molekyuli ili kutoa molekyuli yenye nguvu nyingi, ambayo inaweza kuguswa na DNA, na kusababisha kuzaana, "anasema Schwartz.

"Kuzaana kwingi kunaweza kusababisha saratani." Uchunguzi wa wanyama umeonesha kuwa hii inaweza kusababishwa na kemikali za acrylamides.

Njia moja ya kuzuia shida hii ni kuzamisha viazi kwenye maji kabla ya kuziweka kwenye microwave.

Mionzi

Kuhusu mionzi, microwaves ni salama kabisa. Hizi hutumia mionzi ya elektroniki ya kiwango cha chini aina ile ile ambayo balbu na redio hutumia.

Unapoweka chakula ndani ya microwave, huvuta microwave hizo , na kusababisha molekyuli za maji kwenye chakula kusuaguana hatua inayosababisha chakula kupata moto. Mionzi hiyo haidhuru, anasema Tang.

Kuhusu mionzi microwave ziko salama

Chanzo cha picha, Getty Images