Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Watu 572 wapoteza maisha Afrika Kusini saa 24 zilizopita
Kuna wasiwasi kuwa huenda idadi ya waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona ni kubwa zaidi kuliko takwimu zinavyoonesha.
Watu 572 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya corona kwa kipindi cha saa 24 zilizopita.
Lakini watafiti kutoka baraza la utafiti wa tiba nchini Afrika Kusini wamesema kuwa idadi ya waliopoteza maisha ni kubwa zaidi kuliko kawaida- wakisema kuwa maelfu ya vifo vitokanavyo na Covid-19 huenda havikuripotiwa.
Mpaka sasa, takwimu rasmi zinaonesha, karibu watu 6,000 walipoteza maisha kutokana na Covid-19.
Lakini tafiti za majuma kumi yaliyopita zinaonesha kuwa kumekuwa na vifo 17,000 zaidi kuliko kawaida.
Watafiti wanasema kuna vifo 11,000 ambavyo havijaelezwa.
Wanakisia kuwa vingi kati ya hivyo inawezekana kuwa vinahusiana na Covid-19 kama wale waliopoteza maisha wakiwa nyumbani na vifo vingine ambavyo havijaripotiwa.
Lakini kumekuwa na maoni kuwa raia wa Afrika Kusini wanaepuka kwenda hospitali- kwasababu hakuna nafasi, au wasiwasi wa kupata maambukizi.