Virus vya corona: Joe Biden hatafanya mkutano wa kampeni kwa sababu ya virus vya corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Mgombea urais nchini Marekani kupitia chama cha Democrat, Bwana Joe Biden amesema kuwa hatafanya kampeni za uchaguzi wa rais wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.
"Hii ni kampeni ya yake ambayo haijazoeleka, nafikiri katika historia ya siku hizi," Bwana Biden alisema katika mkutano na waandishi wa habari huko Delaware.
Mpinzani wake,rais Donald Trump,ameshuhudia watu wachache wakijitokeza katika mikutano yake ya hadhara huko Tulsa, Oklahoma, Mwezi Juni na kampeni zake zimetangaza kutokuwepo kwa mikutano mingine ya hadhara.
Kura za maoni zinaonesha kuwa Bwana Biden akiongoza karibu mara mbili dhidi ya mpinzani wake bwana Trump wakati uchaguzi wa Novemba, 3 ukikaribia.
Jumanne, Bwana Biden aliwaambia waandishi wa habari: "Sitaenda kufuata utaratibu uliowekwa na sio kwa ajili yangu tu bali kwa taifa kwa ujumla - hivyo ninamaanisha kuwa hakutakuwa na mikutano ya hadhara . "Sitafanya mikutano ya hadhara."

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani chini ya Barack Obama pia alisema hajafanya vipimo bado vya virusi vya corona ambavyo vimeua watu karibu 130,000 nchini Marekani.
Akizungumzia kuhusu mlipuko Bwana Biden amejipatia nafasi kidogo ya kukutana na Umma, kufanya mahojiano kutoka studio za makeshift TV ambayo iko katika nyumba yake, kumepelekea kampeni za Trump kumpa jina la "Biden anayejificha".
Siku ya Jumanne, Bwana Biden ana nia ya rais ambaye anaweza kukabiliana na majanga ya mlipuko.
"Mwezi baada ya mwezi, kama viongozi wa nchi nyingine wamechukua hatua thabiti kukabiliana na virusi vya corona, Donald Trump ametuangusha," Bwana Biden alisema kabla ya rais Trump alipoanza kumkebehi ,kuwa ni rais wa wakati wa vita".
"Inaonekana wakati wetu wa vita na rais anajisalimisha,kwa kupeperusha bendera nyeupe na kuacha mapambano," Bwana Biden alisema.
Tangazo la Democrats limekuja wakati mtafiti mkuu wa magonjwa Dkt Anthony Fauci alipoliambia punge la seneti la Marekani kuwa ''hatashangazwa '' kama kuwa ongezeko la maambukizi nchini humo itafikia 100,000 kwa siku.
''Ni wazi hatujaweza kudhibiti sasa,'' Dkt Fauci alisema, akitahadharisha kuwa raia wengi wa Marekani hawavai barakoa na hawafuati kanuni ya kutochangamana.


Siku ya Jumanne idadi ya watu walioambukizwa ilifika zaidi ya 40,000 kwa siku moja ikiwa ni mara ya one katika kipindi cha siku tano zilizopita
Tangazo la Democrats limekuja wakati mtafiti mkuu wa magonjwa Dkt Anthony Fauci alipoliambia bunge la seneti la Marekani kuwa ''hatashangazwa '' kama ongezeko la maambukizi nchini humo litafikia watu 100,000 kwa siku.












