Virusi vya corona: Wizara ya fedha yatuma dola bilioni 1.4 za corona kwa watu waliokufa

Iliyochapishwa

Wizara ya fedha Marekani imetuma zaidi ya dola bilioni 1.4 (£1.1bn) kimakosa ya sehemu ya pesa za kukabiliana na janga la corona kwa watu waliokufa, wakaguzi wa serikali wamebaini.

Utafiti huo ulikuwa moja ya changamoto zilizobaini katika mapitio rasmi ya msaada unaotolewa na serikali kwasababu ya janga la virusi vya corona.

Tangu Machi, Bunge limeidhinisha dola trilioni 2.6 katika uchumi wa Marekani kama juhudi za kuusaidia kukabiliana na mdororo kutokana na usambaaji wa virusi vya corona.

Lakini haraka ya kutoa pesa hizo kumechangia kufanyika kwa makosa, wakaguzi wa serikali wamesema.

Kwa mfano, ripoti ya Ofisi ya Uwajibikaji ya Serikali ilibaini kwamba Wizara ya Fedha ya Marekani ambayo inasimamia utoaji wa hundi kwa familia za Marekani, haikuangalia rekodi za wakiokufa, hata ingawa baadhi ya maafisa wa kodi wanaofanyia kazi mpango huo wanasema walizungumzia wasiwasi wao kuhusu hatari ya kutokea kwa makosa kwenye utumaji wa barua pepe.

Ripoti hiyo pia imeonya kwamba mpango wa kutoa mkopo kwa bishara ndogondogo ambao ni asilimia 26 ya pesa zilizotengwa kukabiliana na janga la corona, ulikuwa katika hatari kubwa ya kuingiliwa na walaghai, huku Utawala wa Biashara Ndogondogo ukitupiwa lawama kwa kukosa kutoa ushirikiano katika utoaji wa taarifa kuhusu mikopo na mipango yake ya usimamizi.

"Kwasababu ya idadi ya mikopo iliyoidhinishwa, kasi ambayo mikopo hiyo ilipitishwa na ukosefu wa usalama wa kutosha, kuna hatari kubwa baadhi ya programu za walanguzi ziliidhinishwa," wakaguzi wa serikali wamesema.

Pia idara hiyo iliongeza kwamba kuna umuhimu wa kufanyik akwa mabadiliko ya kukabiliana na hatari kama hizo zinazoweza kutokea.

Mjadala mkali kuhusu msaada unaotolewa

Ripoti hiyo inawadia wakati ambapo wabunge huko Marekani wanajadiliaa ikiwa kuna haja ya kuongeza mfuko wa pesa za kukabiliana na janga la corona au la.

Wakati Democrats na wanauchumi wengi - ikiwemo mkuu wa Benki ya Dunia Marekani - wamependekeza kutolewa kwa msaada zaidi, na kuangazia kiwango cha juu cha ukosefu wa jira licha ya kwamba Republicans wamekuwa wakisita kuidhinisha utoaji wa pesa zaidi kukabiliana na corona.

"Tunastahili kuwa makini sana katika kutathmini kile ambacho ni cha msingi kabla ya kusonga mbele," Seneta wa Republican Pat Toomey alisema katika kikao cha hivi karibuni.

Maafisa wa Ikulu wamesema kuna uwezekano wa kutolewa kwa pesa zingine za ziada lakini ni muhimu kufuatalia juhudi za sasa zilipofikia. Hatahiyo, wakosoaji wanasema, miradi ya serikali imekuwa ikipinga juhudi za kufuatiliwa kwa utendaji wa miradi kadhaa.

Aprili, Rais Donald Trump alimuondoa afisa anayesimamia matumizi ya pesa zilizotengwa kukabiliana na janga la corona.

Nydia Velázquez, mbunge wa Democrat kutoka New York alisema ukaguzi huo ulibaini ubadhirifu wa pesa na uzembe pamoja na matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.

"Kama kuna kile kinachojitokeza wazi katika ripoti hii, kuna umuhimu wa uwepo wa uwazi na uwajibikaji," amesema. "Maafisa wa utawala wanastahili kuitikia wito."

Je Marekani imetumia pesa ngapi kwa janga la corona?

Tangu Machi bunge limendinisha takribani dola trilioni 2.6 kukabiliana na janga la corona.

Takriban asilimia 11 au zaidi ya dola bilioni 280 zilidhamiriwa kutumika kwa malipo ya moja kwa moja ya hadi dola 1,200 kwa watu ambao mshahara wao ni chini ya dola 75,000 na dola 500 kwa watoto.

Kiasi kikubwa cha pesa hizo kilichotolewa - takriban asilimia 26 zilitengengwa kutolewa kama mikopo kwa biashara ndogondogo kupitia mpango maalum uliopo.

Hadi kufiia sasa, Marekani imeshatoa zaidi ya dola bilioni 500 kama mikopo kwa wafanyabiashara milioni 4.6.

Wakosoaji wamesema kwamba utoaji wa pesa hizo umeghubikwa na sheria zisizo wazi na ukosefu wa usimamiz mzuri, madai ambayo yameungwa mkono na Ofisi ya Uwajibikaji ya Serikali

"Umuhimu wa kushukhulikia magonjwa makubwa ya na yanayosambaa kwa haraka na mdororo wa uchumi, mashirika yamepewa nafasi ya kutoa kipaumbele na kuchukua hatua za haraka kutoa pesa na kutekelza mipango mipya," ripoti hiyo imesema.